Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Hakuna habari za "kudaiwa" tena mkuu yote uliyosema ni kweli kabisa
 
Wewe kama sio dereva hauwezi kuona kero za bodaboda hawa jamaa ni hatari sana na hakuna wanachojua zaidi ya breki na kukanyaga mafuta Tu...ukiona Hadi bungeni nako wameanza kuwa na mashaka dhidi ya bodaboda ujue hapo kuna shida
Kwa wabunge wapi?
 
Hawa vijana wasipokamatwa na kufungwa basi binaadamu hatutokuwa salama maana leo saibaba kesho mimi na wewe maana ajali hakuna anayepanga , polisi hapo waonyeshe mfano kwamba uhalifu haukubaliki iwe onyo kwa boda wengine kenge kabisa
 
Sawa hao bodaboda wamekosea kuchoma hilo basi ila madereva wa mabasi ni washenzi sana yaani wanacheza rafu barabarani hatari. mimi nikiona basi naweka chombo yangu pembeni namuachia njia nyeupe.
Mimi nimeendesha pikipiki for more than 15 years... Huwa nawaambia bodaboda kila siku wakiwa highway wawe makini sana na madereva wa mabasi maana ndiyo wanaongoza kwa kuvunja sheria za usalama barabarani. Ukishindana na hao madereva unajitafutia mauti au ulemavu, yaani ukiona anakuja bora umpishe uingie porini kwa sababu ni wapumbavu sana. Shida ya bodaboda wengine ni kujiona wana haki sawa barabarani na magari mengine, kitu ambacho si kweli kwa sababu chassis au body ya bodaboda ni yeye mwenyewe. RIP bodaboda... Tukirudi kwenye hao waliochoma Bus nao ni wapumbavu pia kwa sababu itabidi wakimbie, waache kazi zao na familia zao na pia lazima kuna watakaokamatwa wejiingiza kwenye shida ya kujitakia.
 
Unabii wa Lema umeuelewa si ndiyo mkuu? Nakuunga mkono mkuu tena si kwa bodaboda tuu bali hata bajaj na NOA kuzifanya means of public transport.
 
Huo ni unyasaji wa kijinsia hata km umegongwa Sawa lakini haikufaa kufanya Jambo km hilo wanakuaje km vichaa namna hio unachomaje Gari unajua gharama yake wewe?

Hio clip ionyeshe pia waliofanya tukio hilo alafu Jeshi la Polisi lidili nao hao vichaa waliojificha kwenye kichaka cha ubodaboda
 
Jeshi la policcm lilikuwa wapi yote haya yakijiri?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kuna wanaomuita Lema ni nabii. Sasa tunaona kile alichokiita 'laana'!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Dah! Wasambaa wenzangu mmeniabisha kwa kweli! Hapo itabidi mkajifiche tu milimani ili kuepuka kukamatwa na polisi kutokana na huo upuuzi mlio ufanya.

Mbaya zaidi unaweza kukuta makosa yalikuwa ni ya huyo bodaboda mwenzenu! Maana wengi wenu huwa hamzingatii kabisa sheria za usalama barabarani.
 
Wewe kama sio dereva hauwezi kuona kero za bodaboda hawa jamaa ni hatari sana na hakuna wanachojua zaidi ya breki na kukanyaga mafuta Tu...ukiona Hadi bungeni nako wameanza kuwa na mashaka dhidi ya bodaboda ujue hapo kuna shida
Madereva wa magari wengi nao ni shida ktk uendeshaji tumeona,kwa hali ya kawaida hao boda mwenzao angekuwa amekosea wasingefanya chochote wangenyamaza inawezekana huyo gari kubwa alikosea kwa makusudi.Lkn all in all madereva wa magari na pikpik wengi hawafuati taratibu wawapo barabarani.
 
Gari ulitoe wapi wewe acha kujinasibu we ni muuza uji tu stendi kuku wewe
 
Basi likigonga mtu faini yake 30,000 tu kesi imeisha wanabadilisha dereva gari linaondoka
 
Hao ni waalifu kama waalifu wengine wakamatwe na washtakiwe tabia nyingine sio za kuzivumilia kuna siku watakamata gari la kiongozi na kulichoma.
Sasa kama kiongozi wenyewe ndio hawa wanaotajwa kila siku kwenye report za CAG kuna hasara gani wakichomwa??
 
aliekufa angekua nduguyo ungeandika haya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…