Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

tunaendelea kuwasihi mzingatie M3 ambazo ni Miguu, Mikono na Mdomo; Miguu; kukaa umbali wa Mita 1-2 kati ya mtu na mtu na kuepuka misongamano, Mikono; kunawa mikono na sabuni kwa maji tiririka na Mdomo; kuepuka kugusa Mdomo, Pua na Macho na kuvaa Barakoa. Zitto Kabwe
 
Zito ahangaike na watu wa kigoma aache longo longo, kwani wanaposema chukua tahadhali wanamaanisha nni?, ukimwi upo tuanambiwa tuchukue tahadhali, hivyo ukiwa na akili ukienda chumbani kwa uharifu wako hapo mdo akiri zitatumika, hivyo hata corona ukitoka nyumbani ukijuwa unaenda kukutana na watu hivyo tumia akiri kama ulivyoambiwa.
 
lakini tunapokuwa na serikali kaidi, ambayo tayari imeshaamua kwamba tuendelee kuishi na korona kama tunavyoishi na UKIMWI, bila kuwa na jitihada za dhati; serikali ambayo haiamini kabisa kwenye sayansi, na imeamua kufunga maabara ya kupimia korona kama ndio njia ya kupambana na ugonjwa huu; Serikali ambayo kwao, suala la korona ni jambo linaloshughulikiwa na vyombo vya ulinzi na usalama badala ya wataalam wa afya; sisi kama viongozi mbadala tunabaki na maswali mengi bila majibu. Zitto Kabwe
 
Magufuli ni changer kwenye kila eneo.

Watanzania tunamhitaji kwa miaka 50 ijayo

Wapinzani wote say yeeeeiiiiyeeeee
 
Serikali inaweza kutuficha Watanzania kuhusu mikopo ya ajabu ajabu lakini haiwezi kuwaficha mabeberu..wamewaumbua Hadi wanaomba radhi..

Kumbe BOT kupunguza riba kwa mabenki ni sharti moja wapo la mkopo toka Benk ya Dunia..

Nilitaka nishangae hii serikali toka lini ikawa na huruma na Watanzania kiasi hicho.?
Hii nchi inaliwa kimya kimya mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inaweza kutuficha Watanzania kuhusu mikopo ya ajabu ajabu lakini haiwezi kuwaficha mabeberu..wamewaumbua Hadi wanaomba radhi..

Kumbe BOT kupunguza riba kwa mabenki ni sharti moja wapo la mkopo toka Benk ya Dunia..

Nilitaka nishangae hii serikali toka lini ikawa na huruma na Watanzania kiasi hicho.?
This is a monetary issue. Yet a fiscal issue in offing: T.Shs. devaluation!
 
Sasa Mh. Zitto, kama Serikali itaamua kuwajali wananchi tu pasipo kuimarisha na hizo shughuli za uchumi, maisha yataendeleaje sasa na hata baada ya hiyo Corona kuisha?

Mfano umetolea takwimu za hasara iliyotokea kwenye sekta ya utalii, bado kuna walimu wa baadhi ya shule za binafsi hawana mshahara kwa miezi za ya miwili sasa kwa sababu ya hiyo Corona! Sasa Serikali isipochukua hatua ya kuyarudisha maisha ya Watanzania katika hali yake ya kawaida, huoni itashindwa kukusanya kodi na tutapoteana zaidi humu nchini?

Naungana na wewe kuendelea kukumbushana kuchukua tahadhari mbalimbali za kujikinga dhidi ya hivi virus vya Corona! Lakini ni lazima tutambue huu ugonjwa haujaisha, na hivyo tutafute tu namna nyingine ya kupambana nao huku maisha yetu ya kila siku yakiendelea.
 
Back
Top Bottom