Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Korona: Watanzania Tujilinde, Serikali inajali Uchumi kuliko Uhai wenu - Zitto

Hotuba superb! Umetema nyongo za ukweli na uhakika na busara kubwa! kama wana akkili wamesikia!



UCHUMI AU UHAI?

Ndugu Wananchi,

Tuna bahati mbaya sana kwamba Serikali ya Rais Magufuli kutokana na será mbaya za kiuchumi, imeangusha uchumi wa nchi yetu, hivyo baadhi ya mikakati ya kupambana na Korona inaweza ikaua kabisa uchumi na kuliangusha zaidi Taifa. Hivyo, wakati mwingine tunamuelewa pale anapoamua kuwa kama Mbuni kuficha kichwa chake chini ya ardhi wakati kiwiliwili chote kiko nje!. Ni kwa sababu uchumi uko ICU, zile tambo za makusanyo makubwa, akiba ya fedha za kigeni, uchumi kukua, zilikuwa ni ulaghai, kama ulaghai tunaoushuhudia kwenye mapambano ya Korona.

1590062512455.png



1590062552621.png
 
Serikali imeitupilia mbali sayansi unakuta nayeye anahirizi pumuzi inamsaidia kumlinda..😅

Anyway na hivyo ndivyo mlivyo wanasiasa nachokusihi endelea kupigania labda ipo siku utaongoza nchi,nawe tutakuhukumu na kukusema kwa maamuzi utakayochukua na serikali yako.

Marekani hivi sasa wanajivunia kupima watu wengi na kuwagundua na korona! Hili kwao wanaoana ni mafanikio ya weledi wa vipimio vyao lkn still haishushi ugonjwa na haipunguzi vifo..! Na hivi sasa wameanza kupunguza vikwazo vya lockdown!.

Mitazamo yote unayoiona ikichukuliwa bado haiondoshi ugonjwa! Hii inamaanisha ugonjwa husika unahitaji ama tiba au chanjo alasivyo dawa ya kufubaza virusi vya korona.

Hatua iliochukua serikali yetu ndio itaenda kudhihirisha kuwa imekosea ama imepatia,hivyo ni muda wenye majibu stahiki.

Hata hivyo sioni haja ya sisi kuendelea kushika misimamo ya mataifa mengine ikiwa nao wamefeli!!

Jambo moja ninalolijua kuhusu nyinyi wanasiasa huwa mnatumia mambo yanayotokea kama fimbo ya kumchapia mwenzio ili wewe upate credit kwa wananchi!!..

Ni mambo ya kupembua tu ili kuielewa michezo ya kisiasa. Kwa baadhi naweza onekana mjinga kwa nilichoandika ila kwa mweka mada nafikiri anaelewa namaanisha nini!!

Tuendelee kuijenga nchi huku tukizingatia afya zetu.
 
Duh! Mikopo inafichwa kwa walipa kodi na matokeo yake deni la Taifa pia liko underreported by 6 Trillions! Hii ni hatari sana.

—————————————————-


Pili, Serikali ya Tanzania imeandikiwa barua na Benki ya Dunia kujieleza kwanini imechukua mikopo mbalimbali ya kibiashara na kuficha taarifa za mikopo hiyo, kinyume na kanuni za Benki ya Dunia (IDA NCBP).

Tanzania, chini ya Rais Magufuli, ilichukua mikopo ya kibiashara yenye gharama kubwa ya riba kutoka kwenye mabenki ya biashara ya Standard Chartered (USD 1.5 Bilioni), Eastern and Southern African Trade and Development Bank (USD 1 Bilioni) na Credit Suisse (USD 200 milioni).

Mikopo hii yote yenye thamani ya shilingi Trilioni Sita ilifichwa hapa nchini, hatukuijua, Serikali hii iliamua kudanganya ili kuonyesha kuwa deni letu la Taifa ni himilivu, nyie wananchi wa Tanzania mnaolipa deni hilo mlidanganywa, hamkuambiwa kuhusu mkopo huu, na hata sasa Serikali imekiri jambo hilo la mkopo huko kwawanaoitwa Mabeberu na sio kwenu nyie wananchi.
 
''KUTANGULIZA SAYANSI KWENYE MAPAMBANO YA KISAYANSI''

JPM ni mwanasayansi hivyo majibu yake ni kwa mujubu wa taaluma yake. Au zitto anataka mwanasayansi awe mzungu?
 
"Kiongozi mkuu wa act wazalendo"! Hiki cheo kizuri sana, huchaguliwi, huteuliwi, you're just there, KIONGOZI MKUU WA ACT WAZALENDO!
The SUPREME LEADER sounds like the new Niccolò di Bernardo dei Machiavelli of ACT , New Mao, New Stalin, new Johann Adam Weishaupt.

"The Supreme leader .... This role is usually satisfied by a person deemed to be the representative or manifestation of a god or gods on Earth." - Wikipedia

Cheo hiki kwa maana nyingine ni 'umungu' wa hapa duniani au 'umungu' ndani ya chama. Yaani huyo kiongozi yupo badala ya mungu ndani ya chama husika au serikali husika.

Wana ACT msijekulalamika kuhusu Kiongozi Mkuu (Supreme Leader) wenu atakapo onesha yeye ndiyo chama na chama ndiyo yeye, hakosolewi kama Mungu, na maamuzi yake ndiyo ya mwisho, kumbukeni Mungu hapigiwi kura ya kuchaguliwa kushika wadhifa wa kimungu.
 
Badala ya kumshambulia Zitto ni vema mkachambua content ya alichokisema
Kwani kuna uongo wowote katika hayo niliyo andika? Nioneshe huo uongo.

Kuna kosa kutoa maoni yangu? Natumia uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kama Zitto alivyoutumia, sijaona mahali nimemshambulia.
 
Ukweli Zitto sikuamin hata kidogo ulishasema mengi na hayajatokea ww ni mwanasisa mfu japo zamani nilikua nakukubali sana huna jema kwa nchi hii mmebanwa madili hampati kazi kutupa hofu Watanzania kifumpi mmefilisika kisiasa hasa wewe Zitto.
 
Kwani kuna uongo wowote katika hayo niliyo andika? Nioneshe huo uongo.

Kuna kosa kutoa maoni yangu? Natumia uhuru wa kutoa maoni na kujieleza kama Zitto alivyoutumia, sijaona mahali nimemshambulia.
Hajui kwamba hii ni mada ndani ya mada, BTW umeeleza vizuri. The supreme leader, hachaguliwi, he's just there, iwe kisheria ama la lakini "KIONGOZI MKUU" Zitto ana madaraka kuliko waliochaguliwa. BTW hii ni mada kubwa sana, inahitaji uchambuzi
 
Tatizo la wana siasa haswa vyama vya upinzani ktk nchi yetu ya tanzania wanauzungumzia ugonjwa wa corona kama vile wao wanaishi nchi nyingine wakati sote tupo hapahapa tz, hali halisi ya ugonjwa wa corona ktk nchi yetu ilichagizwa zaidi na hofu kuliko uhalisia, lkn baada ya jitihada kubwa kufanywa na serikali wamefanikiwa Kwa kiasi kikubwa kuondoa hofu Kwa wananchi wake na kuhimiza njia ZA kujikinga na Kwa njia hiyo maambukizi Na vifo vimepumngua kwa kiasi kikubwa sana Tz.

Sasa nyinyi wanasiasa mnataka ugonjwa upungue au uongezeke?
Je mnataka kuwahofisha watanzania au nia yenu ni nini?!

Kama kweli vyama vya siasa vina nia njema Na watanzania na wana uchungu Na maisha yetu kuliko serikali basi tungeona kila Mbuge jimboni kwake anatoa elimu ya kujikinga Kwa wapiga kura wake lkn kinyume Na hapo hatuwaelewi
 
Mkuu zitto umefilisika sana kimawazo siku hizi, wewe unataka tuamini takwimu za nani kwani?

Hivi katika familia sauti inayofuatwa ni ya baba na mama au ya jirani?kauli imetoka kwa baba JPM ambaye ndiye mkuu wa nchi ambaye kauli zake kila mtu mwenye akili timamu lazima azifuate.

Cha ajabu wewe ambaye ni jirani unakuja kuanza kutupangia what to do ukiwa na lengo la kujipatia cheap popularity ambazo hazitakusaidieni,naona mumejaribu kila hoja ya lock down na upuuzi wa hapa na pale lakini mmekwama sasa unakuja na hoja mfu ambazo hazima tija kwa sasa.

Poor zitto badilika huu si muda wa kutafuta cheap popularity ,angalia wananchi katika jimbo lako hakuna ulichowafanyia for five years kazi yako imekuwa kukimbizana na. Vyombo vya dola kwa kwa mambo yasiyo tija.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom