nasssen
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 489
- 535
Ndugu wanajamvi,
Kabla ya yote ningependa kutanguliza pongezi na hongera nyingi za kuweza kufika December tukiwa na pumzi. Pasipo kupoteza muda, ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mkasa ulionikumba weekend hii maeneo fulani hapa jijini Dar es Salaam. Kwa ufupi nilikuwa napita tu kwenye njia moja mara nikaona kwa mbele yangu kuna pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na askari mwenye uniform pamoja na abiria aliyejitambulisha kuwa ni askari pia lakini hakuwa kwenye uniform.
Baada ya kusimama nikashangaa naulizwa "kwanini tunakusimamisha na hausimami tangu kule nyuma? Huoni wenzio wote wamesimama? Kwanini unakuwa na kiburi? Unataka kutusababishia shida wewe, yani mkubwa yupo maeneo haya na haturuhusu magari kupita ila wewe umepita! Yakaongelewa maneno mengine mengi ya kufanana na hayo. Mimi nikawajibu tu kwa upole kuwa kusema kweli sikuona mtu yeyote akinisimamisha na sikutambua kabisa kuwa magari yanasimama. Na isitoshe ni njia ambayo huwa haina magari mengi hivyo sikuwa na idea kabisa kuwa kuna kuzuiwa magari kupisha uwepo wa huyo mkubwa.
Mara yule askari ambaye alikuwa na nguo za kiraia akapokea simu na kuitikia kwa heshima kuashiria ni mkubwa wake alikuwa anampigia simu. Akaweka loud speaker na kwa masikio yangu alisikika akisema "umempata huyo mtu? mfunge pingu natuma gari lije kumchukua haraka sana. Ataenda kutoa maelezo kituoni" Yani niliishiwa nguvu ghafla na kula nikijaribu kuongea nao walikuwa wakipigiwa simu mara kwa mara na huyo mkubwa wao na kuwaamuru kuwa nipelekwe mahabusu nitafunguliwa kesi ambapo nitalipishwa faini ya shilingi milioni nane, kupekuliwa nyumbani kwangu, kutaifishwa kwa gari langu, na kwenda jela kwa kipindi kisichopungua 06 months.
Naomba tu nifupishe kwa kusema kuna kiasi kikubwa tu cha pesa kilinitoka kunusuru huo msukosuko kwasababu nilijiuliza mambo mengi:-
1. Kitendo cha mimi kuingizwa mahabusu kuna hati hati ya kupoteza ajira.
2. Kutaifishwa kwa gari ambalo ni la kampuni ni swala jingine kabisa.
3. Kupekuliwa nyumba naweza hata kubambukizwa madawa, silaha au nyara nikaishia jela.
4. Watoto wangu wadogo watalelewa na nani?
5. Reputation yangu itaharibika kwasababu nitakuwa na fingerprints interpol.
6. Hata nikienda mahakamani, kushindana na system ni ndoto ya mchana.
So, kutokana na hayo yote ilibidi tu niingie mfukoni na hata kukopa kidogo ili niweze kumalizana na hao watu nje ya sheria. Ni jambo ambalo linaniumiza sana kwasababu si kwa pesa iliyonitoka ila kwa kukiuka maadali yangu binafsi ya kutoa chochote.
Tanzania ni nchi yangu na ninaipenda lakini kwa haya niliyopitia, Mungu ndiye anajua hisia zangu na hii nchi zipoje kwa sasa.
Kama kuna mdau aliwahi kupitia mkasa kama wangu naomba tupeane uzoefu na kama kuna mwenye mchango wowote ningependa tujadiliane.
Asanteni sana.