Wagumu Tunadumu
JF-Expert Member
- Dec 10, 2022
- 5,276
- 17,354
Hapo kwenye loudspeaker kuna harufu ya utapeli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli,askari huwa wengi barabaran yaan utawaona tuOk. Pole sana. Uliibiwa. Barabara ikifungwa kwa ajili ya kiongozi askari husimama barabarani kabisa, ungeomuona. Hakukuwa na msafara wowote. Ile maaskri kuongea nawe mda mrefu kisha kupigiwa simu na eti mkubwa wao nao wakaweka laudi spika kisha mkubwa atoa vitisho kwa namna ile, walijuwa utapoteza netweki na uchomoe hela.
Pole Sana mkuuNdugu wanajamvi,
Kabla ya yote ningependa kutanguliza pongezi na hongera nyingi za kuweza kufika December tukiwa na pumzi. Pasipo kupoteza muda, ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mkasa ulionikumba weekend hii maeneo fulani hapa jijini Dar es Salaam. Kwa ufupi nilikuwa napita tu kwenye njia moja mara nikaona kwa mbele yangu kuna pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na askari mwenye uniform pamoja na abiria aliyejitambulisha kuwa ni askari pia lakini hakuwa kwenye uniform.
Baada ya kusimama nikashangaa naulizwa "kwanini tunakusimamisha na hausimami tangu kule nyuma? Huoni wenzio wote wamesimama? Kwanini unakuwa na kiburi? Unataka kutusababishia shida wewe, yani mkubwa yupo maeneo haya na haturuhusu magari kupita ila wewe umepita! Yakaongelewa maneno mengine mengi ya kufanana na hayo. Mimi nikawajibu tu kwa upole kuwa kusema kweli sikuona mtu yeyote akinisimamisha na sikutambua kabisa kuwa magari yanasimama. Na isitoshe ni njia ambayo huwa haina magari mengi hivyo sikuwa na idea kabisa kuwa kuna kuzuiwa magari kupisha uwepo wa huyo mkubwa.
Mara yule askari ambaye alikuwa na nguo za kiraia akapokea simu na kuitikia kwa heshima kuashiria ni mkubwa wake alikuwa anampigia simu. Akaweka loud speaker na kwa masikio yangu alisikika akisema "umempata huyo mtu? mfunge pingu natuma gari lije kumchukua haraka sana. Ataenda kutoa maelezo kituoni" Yani niliishiwa nguvu ghafla na kula nikijaribu kuongea nao walikuwa wakipigiwa simu mara kwa mara na huyo mkubwa wao na kuwaamuru kuwa nipelekwe mahabusu nitafunguliwa kesi ambapo nitalipishwa faini ya shilingi milioni nane, kupekuliwa nyumbani kwangu, kutaifishwa kwa gari langu, na kwenda jela kwa kipindi kisichopungua 06 months.
Naomba tu nifupishe kwa kusema kuna kiasi kikubwa tu cha pesa kilinitoka kunusuru huo msukosuko kwasababu nilijiuliza mambo mengi:-
1. Kitendo cha mimi kuingizwa mahabusu kuna hati hati ya kupoteza ajira.
2. Kutaifishwa kwa gari ambalo ni la kampuni ni swala jingine kabisa.
3. Kupekuliwa nyumba naweza hata kubambukizwa madawa, silaha au nyara nikaishia jela.
4. Watoto wangu wadogo watalelewa na nani?
5. Reputation yangu itaharibika kwasababu nitakuwa na fingerprints interpol.
6. Hata nikienda mahakamani, kushindana na system ni ndoto ya mchana.
So, kutokana na hayo yote ilibidi tu niingie mfukoni na hata kukopa kidogo ili niweze kumalizana na hao watu nje ya sheria. Ni jambo ambalo linaniumiza sana kwasababu si kwa pesa iliyonitoka ila kwa kukiuka maadali yangu binafsi ya kutoa chochote.
Tanzania ni nchi yangu na ninaipenda lakini kwa haya niliyopitia, Mungu ndiye anajua hisia zangu na hii nchi zipoje kwa sasa.
Kama kuna mdau aliwahi kupitia mkasa kama wangu naomba tupeane uzoefu na kama kuna mwenye mchango wowote ningependa tujadiliane.
Asanteni sana.
Yaani ameupotezajeh?Aliuwawa
Hopefully maana alipotezaga msafara wa kikwete huko mkoa wa Mara
Acha TU ndani ya DAKIKA sufuri unageuka mtuhumiwa na hakuna wa kukuonea huruma...HAKUNA WA KUKUANGALIA KWA JICHO LA BABA NA MTOTO....JICHO LA MAMA NA MWANAE.
Kosa kubwa Sawa ila mpaka amefikisha 8M hawa watakuwa matapeliNiliwahi kupatwa na kadhia hiyo ya kuingilia msafara, tena bora wewe mimi nilikatiza kabisa wakati msafara unakuja, sikunyanyaswa kiasi hicho ila nilienda mahakamani nikalipa faini ya makosa ya barabarani.
Kiuhalisia hilo ni kosa kubwa na ukweli wanaweza kuhisi ulikuwa unahatarisha usalama wa huyo mkubwa.
Mimi nilifikishwa kituoni kabisa na nilikuwa na ujasiri wa kujibu kwa utulivu mkubwa na baadae siku hiyo hiyo nilitoka na gari yangu nilipewa nikafunguliwa traffic case tu na nikaenda mahakamani nikakubali kosa nikapigwa faini ya 150k nafikir nilisomewa makosa 3.
Ukiniuliza sijui hata nilitumia nguvu gani kuwafanya wawe wapole wenyewe japo nilipokamatwa ilikuwa hatar ila nilitulia bila kujibishana nao zaid ya kukubali lile ni kosa.
😲😲😲Hao matapeli wapo wengi maeneo ya Masaki, Kwa kifupi hapo umeshatapeliwa. Hakuna askari hàpo! Ni MATAPELI
July 2010 Tarime.Nakumbuka Kuna Askari wa usalqma barabarani alipoteza msafara wa Rais alijiua, sijajua Sheria yake ni Kali kiasi Gani Kwa Kosa kama hilo, ngoja tusubiri wanaojua watatuambia,ila Mimi niliogopa sana yule alivyojiua
Ndugu wanajamvi,
Kabla ya yote ningependa kutanguliza pongezi na hongera nyingi za kuweza kufika December tukiwa na pumzi. Pasipo kupoteza muda, ningependa kwenda moja kwa moja kwenye mkasa ulionikumba weekend hii maeneo fulani hapa jijini Dar es Salaam. Kwa ufupi nilikuwa napita tu kwenye njia moja mara nikaona kwa mbele yangu kuna pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na askari mwenye uniform pamoja na abiria aliyejitambulisha kuwa ni askari pia lakini hakuwa kwenye uniform.
Baada ya kusimama nikashangaa naulizwa "kwanini tunakusimamisha na hausimami tangu kule nyuma? Huoni wenzio wote wamesimama? Kwanini unakuwa na kiburi? Unataka kutusababishia shida wewe, yani mkubwa yupo maeneo haya na haturuhusu magari kupita ila wewe umepita! Yakaongelewa maneno mengine mengi ya kufanana na hayo. Mimi nikawajibu tu kwa upole kuwa kusema kweli sikuona mtu yeyote akinisimamisha na sikutambua kabisa kuwa magari yanasimama. Na isitoshe ni njia ambayo huwa haina magari mengi hivyo sikuwa na idea kabisa kuwa kuna kuzuiwa magari kupisha uwepo wa huyo mkubwa.
Mara yule askari ambaye alikuwa na nguo za kiraia akapokea simu na kuitikia kwa heshima kuashiria ni mkubwa wake alikuwa anampigia simu. Akaweka loud speaker na kwa masikio yangu alisikika akisema "umempata huyo mtu? mfunge pingu natuma gari lije kumchukua haraka sana. Ataenda kutoa maelezo kituoni" Yani niliishiwa nguvu ghafla na kula nikijaribu kuongea nao walikuwa wakipigiwa simu mara kwa mara na huyo mkubwa wao na kuwaamuru kuwa nipelekwe mahabusu nitafunguliwa kesi ambapo nitalipishwa faini ya shilingi milioni nane, kupekuliwa nyumbani kwangu, kutaifishwa kwa gari langu, na kwenda jela kwa kipindi kisichopungua 06 months.
Naomba tu nifupishe kwa kusema kuna kiasi kikubwa tu cha pesa kilinitoka kunusuru huo msukosuko kwasababu nilijiuliza mambo mengi:-
1. Kitendo cha mimi kuingizwa mahabusu kuna hati hati ya kupoteza ajira.
2. Kutaifishwa kwa gari ambalo ni la kampuni ni swala jingine kabisa.
3. Kupekuliwa nyumba naweza hata kubambukizwa madawa, silaha au nyara nikaishia jela.
4. Watoto wangu wadogo watalelewa na nani?
5. Reputation yangu itaharibika kwasababu nitakuwa na fingerprints interpol.
6. Hata nikienda mahakamani, kushindana na system ni ndoto ya mchana.
So, kutokana na hayo yote ilibidi tu niingie mfukoni na hata kukopa kidogo ili niweze kumalizana na hao watu nje ya sheria. Ni jambo ambalo linaniumiza sana kwasababu si kwa pesa iliyonitoka ila kwa kukiuka maadali yangu binafsi ya kutoa chochote.
Tanzania ni nchi yangu na ninaipenda lakini kwa haya niliyopitia, Mungu ndiye anajua hisia zangu na hii nchi zipoje kwa sasa.
Kama kuna mdau aliwahi kupitia mkasa kama wangu naomba tupeane uzoefu na kama kuna mwenye mchango wowote ningependa tujadiliane.
Asanteni sana.
We ni muoga...ulipotishwa kuhusu kazi yako ukajinyea...msafara uliuona?Bora ungeenda.kituoni akala mkubwa wao Kama NI kweli hakina jinai hapoKwanza inaonekana ulikua na ndinga la maana sana linaloashiria unaogelea kwenye ukwasi ,wavuta bange wakajua wakikuchekecha hawakosi fungu nene kwako , ungekua na kigari cha kipuuzi ungeishia kutukanwa au kula mambata ,ila kujipachika kwenye katikati ya msafara wa namba moja au wadogo zake wawili apo utachezea hata submachine gun
kumbuka mimi sio mtoa mada mkuu hata hio gar yakuingilia msafara sina piaWe ni muoga...ulipotishwa kuhusu kazi yako ukajinyea...msafara uliuona?Bora ungeenda.kituoni akala mkubwa wao Kama NI kweli hakina jinai hapo