Kosa la kuingilia msafara au kupita sehemu iliyozuiwa kupisha uwepo wa mtu mkubwa serikalini

Ni kweli,askari huwa wengi barabaran yaan utawaona tu

Tena askar huanza kusimamisha magar wakat rais yupo bafuni anaoga
 
Pole Sana mkuu
 
Kosa kubwa Sawa ila mpaka amefikisha 8M hawa watakuwa matapeli
 
Miaka hiyo Niko na ka baby walker na washikaji tunaaelekea Kigali Rwanda nimefika eneo linaitwa kirehe nafikiri, na kilikuwa kipindi cha uchaguzi mkuu ndani ya rwanda kumbe kagame anaenda kupiga kampeni eneo hilo sasa barabarani sioni gari wala askari na sikujua kama gari zimezuiliwa huko mbele ninakoelekea Mara ghafra ilikuja gari Moja nyeusi king'ora juu ikaniashiria nisimame haraka wakashuka jamaa wanne warefu miwani black wakaniuliza unakwenda wapi nikajibu Kigali kuangalia mechi maana siku hiyo ilikuwa game ya taifa stars na amavubi
Kwenye majibizano hayo ndio Msafara ukapita kwa mwendo wa ngiri mkia juu, wale jamaa na gari lao nao wakaunga palepale Msafara ule wakaacha wameniambia nisitoke hapo watarudi fasta, hapo nishatetemeka balaa, nikawasubiri kama robo saa sioni wakinirudia aaah, nikawasha gari nikaendelea na safari
 
Angekuwa wa mkorani mtu kuja jijini mgesema mshamba ila Kwa sababu umetapeliwa na wahuni wenzio sawa tu ongeza juhudi Ili utapeliwe zaidi.

Hakuna kitu kama hicho Mimi sikupi pole Bali hongera Kwa kulisha familia ya matapeli. Ubaya ubwela hakuna mwaisa mshamba
 
umetapeliwa,,,,hakuna kitu kama hicho,,,kitendo cha kupokea simu kwa loud speaker ulitakiwa ustuke
 
Kwa situatio kma yako mimi nisingewapa shilingi na wasingenifunga ata kidogo

Kila mtu aringie na alichonacho bhana
 
Nakumbuka Kuna Askari wa usalqma barabarani alipoteza msafara wa Rais alijiua, sijajua Sheria yake ni Kali kiasi Gani Kwa Kosa kama hilo, ngoja tusubiri wanaojua watatuambia,ila Mimi niliogopa sana yule alivyojiua
July 2010 Tarime.

Kuna ambao wanadai aliuawa kwa siri ili kulinda vibarua vya watu, na inasemekana hakufanya vile kwa lengo la kupoteza bali maelekezo kutoka juu.

Jiulize tangu lini mtu awekwe rumande akiwa na bastola
 

Pole sana.

Kwa kufupi ulitapeliwa.

Ulitakuwa kuwaambia wakwambie kituo kipi cha Polisi uende. Hakuna faini kubwa hivyo za traffic cases. Kwa sasa limezuka wimbi la wezi wanaotumia mtindo huu unaohusisha watu wenye uniforms za kiaskari. Matukio kama hayo ni matatu niliyoyasikia na yametokea Magengeni ukiwa unaelekea Bunju, barabara ya Mbezi Beach (Bagamoyo Road baada ya Mwenge) na maeneo ya Mlimani City kuelekea Ubungo/Mwenge. Na yanatokea wakati kuna msafara wa ukweli ila kabla askari hawajaanza kuzuia magari rasmi kwenye sehemu wanayokusimamisha.

Cha kuzingatia hakikisha usalama wako ila

1. Husiruhusu mtu aingie kwenye gari lako na chunga ufunguo wako wa gari husijechukuliwa ili kukuingiza kwenye vitisho zaidi

2. Waambie muongozane mwende kituo cha polisi kilicho karibu. Ukipata bahati ya kuwaona karibu traffic police wenye uniforms elekea kwa hao kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi.

Matukio ya hivi yapo yapo na polisi wanayajua na wanapambana nayo kwa nguvu nyingi wakipata taarifa. Kuna wahusika kadhaa wamekamatwa kinachotakiwa tuchukue tahadhari.

kitu muhimu tutambue polisi ni mahala salama kwa mtu yeyote hata kama una makosa, utaelimishwa ikilazimu kutozwa faini hata kupelekwa mahakamani ila uhakika wa usalama wako ndo jambo kubwa la kuzingatia.
 
Mimi wangeniua nilivyozaliwa mbishi Kama nywele zangu za kipilipili...labda niwe nilifanya makusudi
 
Ilishanitokea 2016.. nikaliwa 300k.. bahati magufuli alikula vichwa polisi wote (3) waliohusika.. ilikuwa coincidence tu..
 
We ni muoga...ulipotishwa kuhusu kazi yako ukajinyea...msafara uliuona?Bora ungeenda.kituoni akala mkubwa wao Kama NI kweli hakina jinai hapo
 
We ni muoga...ulipotishwa kuhusu kazi yako ukajinyea...msafara uliuona?Bora ungeenda.kituoni akala mkubwa wao Kama NI kweli hakina jinai hapo
kumbuka mimi sio mtoa mada mkuu hata hio gar yakuingilia msafara sina pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…