Kosa langu nini ni Vannesa?

Kosa langu nini ni Vannesa?

Mwisho kupenda kwa dhati miaka 21, Inachukua miez 15 tu au pungufu kumsahau mtu uliempenda.

Wewe siku zinasonga, Wiki na Miaka inaenda bado unamkumbuka tu Vanessa, Nathibisha una Ugonjwa wa Akili
by Dr. WeedLiquorz .
Mkuu hujapatwa wewe . Hujawahi kupendwa alafu kibaya na wewe upende na mwanamke asiye na shida ya hela hanuni ovyo . Mchangamfu , mjanja na mwenye madoido . Utakufa mkuu ukiachwa . Inauma mno
 
Nyie na mapenzi where and whereeee mangi
Hata uwe mangi ulikulia moshi mpaka unafika miaka 40 ukikutana na mrembo mwenye makeke kama Vannesa akakupenda na akajiachia kwako kwa muda wa miezi sita tu lazima utepete . Nibalaa . Ngoja uone mbele ya safari ....
 
Mkuu hujapatwa wewe . Hujawahi kupendwa alafu kibaya na wewe upende na mwanamke asiye na shida ya hela hanuni ovyo . Mchangamfu , mjanja na mwenye madoido . Utakufa mkuu ukiachwa . Inauma mno
Labda sio mimi.
 
Kwaiyo wewe Toka uzaliwe umegonga demu mmoja tu. Pole
Toka nizaliwe mpaka chuo ndio nilikuja kumgonga Vannesa kabla ya hapo hata mazoea kuwa sina na mtoto wa kike . Hata stori za mapenzi na vijana wenzangu kuwa hamna nilikuwa serious sana
 
Yaani katika kusomaga kwangu visa vingi, lazima msichana awe mrembo katika masimulizi.

Utasikia eeh Vanessa wewe
Macho yako yamejaa mng'ao wa ajabu, yakitafakari uzuri wa ulimwengu, yakinivuta ndani ya ulimwengu wako wa siri na ndoto za kutamanika.

Ngozi yako nyororo inaleta hisia za utamu, kama upepo laini wa majira ya joto ukipapasa ngozi yangu.

Sauti yako ni kama muziki wa asili, tamu na unapenya moyo wangu, ikiniacha nikitamani kusikia zaidi.

Shingo yako yenye pingili tamu ni kama shingo ya swala, ikitoa mvuto wa kipekee. Umbo lako linalingana kama sanamu iliyoundwa kwa ustadi na maridadi, ikisanifiwa na mafundi wa mafundi, eeh Molà jalia.

Tabia na utu wa kipekee na upendo wa kweli. Haiba yako ya kike na tabia yako ya kupendeza hutawanya furaha na amani kila mahali unapopita, kama maua yaliyotawanyika katika upeo wa macho ya wengi.

Yaani unamuimagine mwanamke huyu mpaka malaika anakutokea mbeleni 🤣🤣🤣🤣.

Aya, leta vitu ewe mwathiriwa wa Vanessa.
 
alipoanza kusema tu “vannesa alikua na asili ya kihindi” basi nikajua tu hii ni story ya kutunga
Sio ya kutunga mkuu . Niliwahi kuiandika Twitter wakati flani japokuwa kwa ufupi na leo narudia tena . Ni chotara flani mswahili hata lafudhi ya kihindi hana mama yake ni mswahili
 
Yaani katika kusomaga kwangu visa vingi, lazima msichana awe mrembo katika masimulizi.

Utasikia eeh Vanessa wewe
Macho yako yamejaa mng'ao wa ajabu, yakitafakari uzuri wa ulimwengu, yakinivuta ndani ya ulimwengu wako wa siri na ndoto za kutamanika.

Ngozi yako nyororo inaleta hisia za utamu, kama upepo laini wa majira ya joto ukipapasa ngozi yangu.

Sauti yako ni kama muziki wa asili, tamu na unapenya moyo wangu, ikiniacha nikitamani kusikia zaidi.

Shingo yako yenye pingili tamu ni kama shingo ya swala, ikitoa mvuto wa kipekee. Umbo lako linalingana kama sanamu iliyoundwa kwa ustadi na maridadi, ikisanifiwa na mafundi wa mafundi, eeh Molà jalia.

Tabia na utu wa kipekee na upendo wa kweli. Haiba yako ya kike na tabia yako ya kupendeza hutawanya furaha na amani kila mahali unapopita, kama maua yaliyotawanyika katika upeo wa macho ya wengi.

Yaani unamuimagine mwanamke huyu mpaka malaika anakutokea mbeleni [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Aya, leta vitu ewe mwathiriwa wa Vanessa.
Mimi sio mwandishi ila najitahidi tu kuleta yaliyonisibu . Uandishi naona unauweza [emoji23]
 
KOSA LANGU NINI Ni VANNESSA ?

Vannesa kwanini ulinifundisha kupenda na kuniacha nikiumia . Vannesa kosa langu nini?


Mwendelezo Sehemu ya 3.....

Mazoea yaliendelea siku moja alinipa namba yake na mimi nikamwandikia yangu kwa makubaliano ya muda wa kutoka ni mpigie tutoke wote . Ikawa ndio kawaida yetu kutoka wote na hata lunch tulikuwa tunaenda kula wote mara nyingi zaidi yeye akingangania kunilipia na wakati mwingine nikilipa mimi. Tulikolea utani yaani nilibadilika nikawa mtu wa furaha sana. Ila mtihani ulikuwa usiku ndoto nyevu zilijirudia hata mara tatu ndani ya usiku mmoja ni kama hisia zilizokuwa zimefungwa kwa miaka mingi zilifunguliwa . Nilianza kupunguza kusoma maandiko . Mapenzi yalianza kutawala sana akili yangu nilitamani sana ningempata vannesa ila ndio hivyo sikuwa na ujanja wowote hata kuongea tu ilikuwa mtihani .

Sasa ukaribu na Vanessa ukaendelea kukua kila kukicha asubuhi na mapema akawa ananipigia tunakutana tunaenda wote chuo kiukweli pale ilibaki kuambiana tu nakupenda. Sio kwa utani ule kushikana mikono jinsi alivyokuwa akiniangalia huku akitabasamu hapa ni udomo zege tu ulichelewesha mambo

Vannesa alikuwa mtoto wa pekee kwa mama yake. Mama yake ni msambaa wa Tanga ila baba yake alinionesha picha tu ni mtu wa singida ila anauchotara kama sikosei atakuwa na kiasili cha kihindi ndio kamwathiri hata VANNESSA. Baba yake yupo vizuri kifedha japokuwa hawaishi na mama yake ana mke mwingine na watoto wengine . Aliwajengea tu nyumba na kumfungulia mama yake duka la vitambaa kariakoo.

.Sasa ulikata mwezi tokea nikutane na Vannesa mazoea yakivuka mipaka sasa usiku tukawa tunapiga stori na kuchat na siku moja aliniuliza kwenye meseji . Ulishawahi kuwa na mpenzi nikamjibu sikuwahi . Nikamuuliza je wewe akaniambia alishawahi ila wakaachana hapo ndio alinifungua kidogo kuanza kuongelea sana mapenzi. Nikamuuliza kwanini sasa hivi huna mpenzi. Akanijibu Kuna mwanaume handsome sana Natamani sana niwe nae lakini sijui kama ananipenda na mimi nikamwambia hivyo hivyo . Mimi pia kuna mwanamke mrembo sana nampenda sana kwenye maisha yangu sijawahi kupenda ni mara ya kwanza navutiwa nae sana ila naogopa kumwambia kwani naogopa akinikataa nitaumia sana na nitachukia kabisa mapenzi. Huyu mtoto wa kike alijua kunibadilisha kama sio mimi vile . Mwisho yeye akasema kwanini usimwambie tu unaweza kukuta na yeye anakupenda ndio nikakaza moyo na kumwambia ni wewe hapo . Akaniambia hata mimi nakupenda sana nimesubiri hilo mda mrefu sana . Nililipukwa na mlipuko wa furaha tulichat kidogo na kutakiana usiku mwema. Mwanaume nilijikuta nikirukaruka ndani kama kindama kilichoshiba maziwa nilifurahi sana . Nilijiona mtu mpya kabisa nilikuwa nikijirusha kwenye kochi kwa raha nikifanya kazi ya kuosha vyombo ndio nilale nikipiga kimluzi flani hivi. Acha kabisa nilikuwa kwenye kilele cha furaha.

[emoji294][emoji294][emoji294][emoji172][emoji172][emoji172][emoji173]
Kuna wale wanasema eti wachagga hawapendi sio kweli. Ni kukosekana kwa chemistry kwenye mahusiano tu. Wewe ni mkimya unachukua mkimya mwenzio ili nini? . Kila kitu unataka userious ili nini ? . Usioe tabia haijalishi mwanamke anatabia nzuri kiasi gani kama humpendi usimwoe ? Na mwanamke haijalishi huyo mwanaume ana hela kiasi gani kama humpendi usiolewe nae?. Ukitaka ufurahie maisha ni mukutane mnao match . mapenzi hayahitaji nguvu . Haya hitaji pesa ukiona mwanamke umemnyima pesa na anatishia kukuacha mwache aende . Mapenzi ya kweli niya wote kunganganiana sio mmoja . kama upo kwenye penzi ambalo wewe ndio umelibeba mgongoni lishushe litembee kama halitaki liache nenda zako. Wanaume wengi ni watumwa wa kumfurahisha mwanamke nakudhani eti kusex ndio furaha ya mapenzi sio kweli sex ni asilimia 40 tu asilimia 60 ya furaha ya maisha ya mahusiano ni namna mnavyoishi utani kutoana out kupigiana simu na mwembwe nyingine teletele ukipata hizi ukiachwa ndio unapata maumivu ya kweli . Nikuulize wewe na mpenzi wako mshapigana kwa mito au kukimbizana kwa raha ? Msichukuane tu na kuoana kwakuwa wote mnapesa mnakazi mnatabia njema hapana. Mtakuwa mnasindikiza wengine kufurahia maisha hapa duniani.[emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji173][emoji172][emoji294]

[emoji173]Vannesa alikuwa na sifa zote za kufurahisha kukaa nae tu ilikuwa ni furaha kubwa sana.[emoji173]

Sasa Asubuhi kama kawaida alinipigia tukaelekea chuo pamoja . Tulivyokutana nilipoteza confidence kabisa nikawa simwangalii kama kawaida ila yeye aligundua hilo alinizidi sana ujanja akawa ananichangamsha kwa kuniongelesha sana kuhusu mapenzi nikawa na mjibu huku tunatembea amekumbatia mkono wangu. Kwa alivyo mrembo kuwa nafurahia sana na kujiona kama namiliki V8 vile . Nilianza kujiamini kiasi tukaendelea kama wiki hivi sasa

Weekend moja tukatoka na Vannesa tukaenda beach ila nikagoma kabisa kuingia kwenye maji kuoga yenyewe kumwona alivyovaa tu nilipata shida sana boxer ililoa maji maji ya uchu sembuse kuogelea wote nimevaa kiboxer . Sikuvua hata jeans kwa kuhofia aibu hiyo upwiru ulikuwa kwenye kiwango cha kutisha


Itaendelea ........

Kosa langu nini Vannesa???
Sehemu ya 4 soon ....
 
🎵🎤🔊 uliniacha na mtoto wangu mdogo vannesa.
siku zinapita miaka, inakwenda mimi na vannessa.
wewe utakuja nikumbuka aah
wewe utakuja niulizaa aah


umenikumbusha huu wimbo mkuu
 
[emoji444][emoji441][emoji344] uliniacha na mtoto wangu mdogo vannesa.
siku zinapita miaka, inakwenda mimi na vannessa.
wewe utakuja nikumbuka aah
wewe utakuja niulizaa aah


umenikumbusha huu wimbo mkuu
Wimbo wa nani nikausikilize unifariji
 
Mkuu japo hujamaliza story yako yaani ahdi chuo ulikuwa huna hisia na warembo? kama sio vanesa sahv ungekuwa team Lokole and others
 
Back
Top Bottom