Kuacha ualimu serikalini na kuhamia chuo kikuu binafsi

GIANT90

Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
54
Reaction score
45
Habari wadau wa JF.
Nimefundisha sekondari za serikali kwa miaka 12, hivi karibuni nimepata ofa ya ajira chuo kikuu binafsi kama assistant lecturer. Mshahara wangu wa serikali ni mdogo sana na nimepambana kupata nafasi chuo kikuu cha public nimekwama. Mwenye uzoefu naomba tusaidiane ushauri je? Kuacha government na kwenda private would be a logical decision or not?
Karibuni wadau.
 
Mkuu angalia hela
 
Serikali mshahara mdogo ila uhakika.
Chuo binafsi mshahara mkubwa ila kuna kukopwa.
Unaweza ukakaa hadi miezi mitatu na hujalipwa.
Tafuta mwenyeji hapo akupe historia ya ulipaji mishahara.
Kama wanalipa freshi, nenda.
 
Daaah ngoja nifuatilie comment naweza ambulia kitu
 
Inabidi ujue historia ya hicho chuo vizuri.
Je Umesikia yanayoendelea Makumira ?
 
Tamaa ilimponza fisi,Kuna bro wangu naye aliacha kazi serikalini mwaka 2015 akaenda shule private maana aliahidiwa mshahara mnono na posho,alifanya kazi miaka 3 tu wakampiga chini.mambo yalipozidi kuwa magumu akaomba arudi kwenye ajira yake ya serikalini lakini was too late yaani ukitoka ndio nitolee hakuna kurudi,mpaka sasa tuko naye kitaa tunakunywa visungura amechoka amechakaa,Mimi sikushauri uache aisee komaa huko huko serikalini
 
Very Tanzanian. Always sceptical!
 
Unatakiwa ufanye tathmini ya kutosha ikiwemo historia ya chuo namna ya mikataba yake inavyoenda na utendaji kazi wake upoje unakuta unapewa 5 million ila mikataba wake ni mgumu kupita kias serikalin unakula 1.9 m ila unakuwa Huru kupita kias labda uwe kazi kunoga
 
Kama hicho Chuo Kikuu kipo ndani ya Mkoa unaofanyia kazi kwanini usiwe unapiga ndondo (kubaki Serikalini lakini kutumia hicho chuo kama side hustle).

Lakini kama chuo kikuu kipo nje Mkoa unaofanyia kazi tumia likizo wakati mmefunga shule za Gavoo uende ukafundishe huko chuo huku ukiwa unasikilizia utaratibu wao wa malipo kama unasadifu matarajio yako ya kuifanya ndiyo iwe chanzo namba moja cha kipato cha kuendesha maisha yako.
 
Dunia ya sasa tunaangalia marupurupu! Ila private unyanyasaji upo! Serikalini ni mahali pa kudumu bila usumbufu.
 
Angalia aina ya chuo chenyewe. Usijichanganye ukaenda TEKU au Tumaini Makumira. Kuna wenzako wamekuja kutoa ushuhuda humu wa kushindwa kulipwa mishahara kwa wakati.
 
Mwalimu anakosaje shule ya kufundisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…