Kuacha ualimu serikalini na kuhamia chuo kikuu binafsi

Kuacha ualimu serikalini na kuhamia chuo kikuu binafsi

Habari wadau wa JF.
Nimefundisha sekondari za serikali kwa miaka 12, hivi karibuni nimepata ofa ya ajira chuo kikuu binafsi kama assistant lecturer. Mshahara wangu wa serikali ni mdogo sana na nimepambana kupata nafasi chuo kikuu cha public nimekwama. Mwenye uzoefu naomba tusaidiane ushauri je? Kuacha government na kwenda private would be a logical decision or not?
Karibuni wadau.

Naweza kukupa Uzoefu kidogo kwa upande wa private;
Wafanyakazi wanachapa kazi kweli kweli hakuna blaa blaa kule...
Matokeo yana pimwa (result oriented)
Ukisha ingia kupanda mshahara inategemea zaidi na performance yako (kuliko hata kuongeza vyeti)
Muhimu; Tafuta anayefanya kazi chuo husika ujue yafuatayo
1. Ulipwaji wa Mishahara unaenda kwa wakati (Tar 25th- 30th) pengine upate history ya miaka 3.
2. Kama upandaji wa mishahara unazingatia madaraja au wanautaratibu mwingine
3. natumaini uliuliza kama kuna bonases nyingine kama nyumba, usafiri, chai/Chakula etc
4. Lakini uliza pia kama wanatabia ya kusimamisha/kufukuza wakufunzi na nini kinasababisha
Ukiona yote yako sawa, unaweza kusonga mbele....
 
Anatoka Kufundisha Shule mkuu anataka kwenda kufundisha chuo kikuu
Unajibu kwa kunahamisha mada nionekane nachangia tu sifahamu nachochangia.

Screenshot_20261025-194522.jpg
 
baki gvt, tafuta njia ya kukuza kipato bila kutoka hapo,
Angekuwa anaweza angekuwa nacho. Tamisemi ni utumwa. Moja na nusu mpaka Tisa na nusu hiyo njia nyingine ni ipi? Unataka awe mtoto? Au aibe ofisini? Tuwche kudanganyana kama vile ni kitu kirahisi tu. Mazingira alipo? Ni uongo muache kudanganya watu. Hapo ni ataingia mkopo, labda afungue kiduka uchwara. Ambao ni umaskini tu kuskuma siku. Muda wa kutengeneza pesa ni Sasa sio kusubiri pension. Na mwenye uthubutu ndio anayefanikiwa. Kufanya kazi serikalini ni kwa wavivu na waoga wa maisha.
 
Habari wadau wa JF.
Nimefundisha sekondari za serikali kwa miaka 12, hivi karibuni nimepata ofa ya ajira chuo kikuu binafsi kama assistant lecturer. Mshahara wangu wa serikali ni mdogo sana na nimepambana kupata nafasi chuo kikuu cha public nimekwama. Mwenye uzoefu naomba tusaidiane ushauri je? Kuacha government na kwenda private would be a logical decision or not?
Karibuni wadau.
Kuna vitu vitatu vinakosekana hapa ili nikupe ushauri wangu.
1. Ongezeka la mshahara ni shs ngapi.
2. Fani yako, yani masomo unayofundisha.
3. Mkoa ulipo

Hivyo nitakupa ushauri wa ujumla.
1. Hakuna mtu aliye tajirika au kuwa financially stable kwa mshara tu. 2.Mshahara tunautumia kama sehemu ya kipato cha uhakika lakini tufanya hussles nyingine kupata mapato ya ziada.
3. Kama kwa miaka 12 umeshindwa kujitengenezea fursa nyingine ya kupata kipato cha zaidi kutoka nje ya kazi yako, then wewe uko kwenye kundi la kuku wa kisasa. Unasubiri hadi kuwa feeded. Kwa hali hiyo hata ukienda private bado utakwama kiuchumi tu.
4. Lecturers wengi ambao wanako financially stable hawategemei mishahara. Wanapiga kazi nyingine au ujasiriamali nje ya kazi zao.

Ushauri wangu ni kwamba kama unataka finacial freedom jiongeze angalia namna ya kutafuta kipato cha nyongeza cha halaliukiwa hapo hapo shule ya sekondari ya serikali bila kuathiri kazi yako.
 
Habari wadau wa JF.
Nimefundisha sekondari za serikali kwa miaka 12, hivi karibuni nimepata ofa ya ajira chuo kikuu binafsi kama assistant lecturer. Mshahara wangu wa serikali ni mdogo sana na nimepambana kupata nafasi chuo kikuu cha public nimekwama. Mwenye uzoefu naomba tusaidiane ushauri je? Kuacha government na kwenda private would be a logical decision or not?
Karibuni wadau.
Mpaka umetafuta sehemu nyingine ya kufanya kazi na kuongeza kipato ina maana kuna mambo ulishayatafakari.Au unataka upotoshwe?
 
Tamaa ilimponza fisi,Kuna bro wangu naye aliacha kazi serikalini mwaka 2015 akaenda shule private maana aliahidiwa mshahara mnono na posho,alifanya kazi miaka 3 tu wakampiga chini.mambo yalipozidi kuwa magumu akaomba arudi kwenye ajira yake ya serikalini lakini was too late yaani ukitoka ndio nitolee hakuna kurudi,mpaka sasa tuko naye kitaa tunakunywa visungura amechoka amechakaa,Mimi sikushauri uache aisee komaa huko huko serikalini
Naogopa sana kujifunza kwa walioshindwa, kwangu Mimi rejea za watu walioshindwa Huwa kama Changamoto ya kukamilisha lengo langu ila sio kusitisha kusudio langu.
 
Kosa kubwa ambalo watumishi wa umma huwa wanalifanya ni kukopa bank na kuingiza hizo hela kwenye ku finance maisha yao kama kununua kiwanja, kujenga, kununia gari, kununua fanicha, kulipa ada za watoto etc. Vitu ambavyo havizalishi na haviwasaidii kurejesha mikopo. Hivyo wanajikuta kwenye umasikini. Sikuzote za maisha yao.
 
Very true mkuu
 
Habari wadau wa JF.
Nimefundisha sekondari za serikali kwa miaka 12, hivi karibuni nimepata ofa ya ajira chuo kikuu binafsi kama assistant lecturer. Mshahara wangu wa serikali ni mdogo sana na nimepambana kupata nafasi chuo kikuu cha public nimekwama. Mwenye uzoefu naomba tusaidiane ushauri je? Kuacha government na kwenda private would be a logical decision or not?
Karibuni wadau.
Omba ruhusa ya bila Malipo ya mwaka, au miaka miwili kutokana na family issues au magonjwa,

After 2yrs utafanya maamuzi ya kuacha kazi au la
 
Mwalimu anakosaje shule ya kufundisha?
Wewe naye ubongo wako hauko updated,hujui kuwa sasa hivi Kuna walimu zaidi ya 500K wako mtaani wanasubiri ajira, na hakuna shule za kuwaajiri,wewe unaleta porojo za mwalimu unakosaje shule ya kufundisha!!, kama serikali yenye shule zaidi ya shule 6000 imeshindwa kuwajili ,vipi shule za private ambazo hazifiki hata 1000?

Tujitahidi kuuliza maswali ya mantiki
 
Makumira hawalipi?
 
Hapana mkuu! Kuna nini kinaendelea?

K
 
Noma sana
 
Back
Top Bottom