Kuacha ualimu serikalini na kuhamia chuo kikuu binafsi

Sasa hzo pesa alizokuwa analipwa kwa unono alipeleka wapi?
 
Baki serikalini
Miaka uliyokaa kazini ni mingi naamini hata mshahara (Take home) milioni+ ,
Kwanini usitumie uhuru wa serikalini kuwekeza kwenye shughuri zako binafis ukajiongezea kipato ?
Kuliko kwenda private ambapo ajira yake siyo ya kudumu na mshahara hutegemea zaidi wanafunzi.
 
Ni nzuri ila angali kisiwe chuo kinachomilikiwa na KKKT, BAKWATA, Anglican, Moravian au Mwamposa
 
Moderator funga uzi
Usiache kazi Serikalini, mshahara ni uhakika.
 
Risk hapo ni job security.
Hujasema wanakuapa mkataba wa miaka mingapi, shida ya private ipo siku watakusitishia mkataba baada ya muda flani.
Kama wamekwambia ni permanent and pensionable nenda. Ila wakisema kuna ukomo wa mkataba. Kitakupata kitu.

Kama kuna ukomo wa mkataba, waambie wakupe part time, kama utaweza.
 
wengi waliooenda private kutoka serikalini hua mwisho wao ni mbaya sana

SIKUSHAURI MKUU.

Private unaweza ukaliowa vizur mwaka mmoja labda unaofata ukashangaa unaanza danadana unaofata tena wanakukopa mshahara mwishoo hulipwiii... mwisho kabisaa unakua unajitolea.. then mwiisho Tamati unarudi mtaani
 
Kuna jamaa yangu alikuwa tutorial assistant chuo kikuu cha serikali, akapata mchongo wa wamarekani unalipa in dollars, aliandika barua ya kuacha kazi ndani ya 24 hours. Ndani ya mwaka akajenga , akafungua biashara ya apartments, magari matatu ya ghafla, yani tulimshahau, within miaka 2 aliyofanya kazi, maisha yake mpaka Leo yamebadilika sanaa. Ushauri wangu, pima maslahi, je is it worth it? Maana unaweza kung'ang'ana na serikali, na vimikopo ukateseka mpaka uzeeni, au ujilipue ufanye mambo ya msingi ukiwa na nguvu. Pima. Hakikisha maslahi ya huko private ni ata mara 3 ya unapotoka. Ikiwa hivyo sepa haraka. Kachkue pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…