Kuachiwa kwa Mbowe; Nimeamini muda mwingine kuna hisia za kweli na ni ushahidi kuna mawasiliano kati ya nafsi zetu na ulimwengu wa nje

Kuachiwa kwa Mbowe; Nimeamini muda mwingine kuna hisia za kweli na ni ushahidi kuna mawasiliano kati ya nafsi zetu na ulimwengu wa nje

Haki imefuata mkondo Tanzania hatuna gaidi mzawa na hajawahi kuwepo labda vizazi vijavyo.
Screenshot_20220304-120052.png

Mark my words; hii kesi itarudi. Soma sentensi ya mwisho.
 
Habari wadau,

Hapa niko mahali fulani nasubiri kukamilisha jambo fulani na kwakuwa jambo husika linachukua muda, nimeamua kujilaza kwenye benchi nikisubiri kuhudumiwa.

Wakati nikiwa nimejilaza kwenye benchi(nimetoka shift ya usiku), nikiwaza mambo mbalimbali, likanijia wazo la kesi ya Mbowe na hapo hapo nikapata hisia kuwa huenda Mbowe leo ataachiwa.

Baada ya kupata hisia hiyo, nikanyanyuka nikaingia JF na kukutana na breaking news kuwa Mbowe kaachiwa. Hakika nimefurahi mno kwa ushindi huu wa kisiasa alioupata Mbowe,na pia nimeamini hisia za kweli zipo, na zaidi kuna uhusiano wa hisia tunazopata katika nafsi zetu na kinachoendelea katika Ulimwengu wa nje.

Hii si mara yangu ya kwanza kuwaza au kupata hisia juu ya jambo fulani na jambo husika kutokea, ila hili la Mbowe kuachiwa na watesi wake limenigusa mmo na kunifanya ni-share hii experience.

Intuition is real!

Hongera Mbowe na wenzako!

God is great!
Great!!!
 
Kila nikiisoma na kuirudia napata tafsiri tofauti

Umeshaambiwa DPP akishatamka kua hana nia ya kuendelea na kesi tena mashataka yote yamefutwa bila masharti, ni sawa na Mbowe kashinda kuliko ndugu zitto alivotaka watu waombe msamaha maana yake ukiomba msamaha unakua umekiri kosa hivo ni rahisi sana wao kuframe tena kesi na kukushtaki.
 
Pamoja na kufutiwa mashitaka naamini Mbowe na Genge lake la kihalifu watakuwa wameshika adbu.
na wamejifunza kuwa ukichezea Amani ya nchi utashughulikiwa kama mbwa koko.

Ushauri wa bure sasa ni bora akalee wajukuu.
 
Roho ya kwanini inakusaidia nini mkuu?
 
Pamoja na kufutiwa mashitaka naamini Mbowe na Genge lake la kihalifu watakuwa wameshika adbu.
na wamejifunza kuwa ukichezea Amani ya nchi utashughulikiwa kama mbwa koko.

Ushauri wa bure sasa ni bora akalee wajukuu.
Ndio kwanza moto unawaka.
 
Kwa hiyo ikirudi ndio itamfanya kuwa gaidi?
Hapana... Mbowe hajawi kuwa gaidi!
My point ni kuwa hii kesi itaendelea kuibuka huko mbele ya safari.
Soma vizuri hiyo Nolle Prosequi ya DPP hasa sentensi ya mwisho.
 
Back
Top Bottom