Kuagiza gari kutoka UK vs South Africa, Japa & Singapore

Kuagiza gari kutoka UK vs South Africa, Japa & Singapore

SA wana assemble magari mengi sana aina tofauti, SA unaweza pigwa za uso maana kuna magari yao ambapo unaweza pata shida kwenye vipulu, (spare) na hayo ya japan wanayo mengi
Mkuuu South Africa hakuna spare ya gari unayotafuta ukakosa, South Africa kuna kila aina ya gari unayoyaona mtandaoni na uzuri wa huku kuna mafundi wa uwakika
 
Ukitaka ujue Watanzania ni watu wa kukatisha tamaa waulize kitu cha mafanikio kwako...magari yapo SA na bei nzuri wengi wamenunua na wanashangaa mimi nawapa njia si lazima nipate kupitia kwenu nina biashara zangu nafanya wapo wengi humu wamepata magari kupitia kwangu napokua SA na vitu vingine...magari SA ni mengi wauzaji ni CAR dealers hao Wanigeria unakutana nao wapi wao wapo busy na biashara zao..
Yani mtu kama anataka kununua gari kwa mtu mweusi ni mara mia anunue gari ya m. Nigeria hawa jamaa gari kwao service wanaijua sio sawa na mtu mweusi yeye akipiga moto ilimradi garia iwake
Japan mkuu, SA wa Nigeria hawatakuacha salama mkuuu
 
you mean waafrika/makaburu magari yao yana usalama zaidi kuliko ya wazungu huko Ulaya

One learns something new humu JF everyday

in other words safety na kila kitu katika hayo magari waafrika wanaongoza
Mkuuu ukisikia kaburu sio jina dogo hilo kama ambavyo unalisikia uki tanzania jaribu kutembea south Africa ndio utajua neno kaburu (Boer) linamaanisha nini
 
Mkuuu South Africa hakuna spare ya gari unayotafuta ukakosa, South Africa kuna kila aina ya gari unayoyaona mtandaoni na uzuri wa huku kuna mafundi wa uwakika
mmm spare wanazo nyingi sana hata magari wanayo ya kila aina hata matapeli wanao wa uhakika mimi nilikuwa na gari aina ya Fiat 124 nilikuwa natafuta piston rings pamoja na oil seal nilivipata huko mwaka 1991, labled Fiat 124 na oil seal lakini piston rings kipenyo kilikuwa kikubwa ila oil seal ilikuwa yenyewe huko kuna mambo mengi bana. Here were are sharing experiences
 
Naamini magari ya SA ni mazuri hasa gari kubwa, tatizo hamna mfumo mzuri wa uagizaji uliopo wazi na kuaminika zinakuwa ni baishara za kubahatisha kupigwa nje nje au kuuziwa gari ya wizi.
Ulitaka mfumo gani? Ingia www.webuycars.co.za angalia gari, inspection report ukilipenda agiza (Wana huduma ya ku-deliver Kwa truck au meli).
NB: South Africa Wana soko kubwa la magari yao, so nyie wa-Tanganyika mnaonunua magari Kwa manung'uniko hawana muda na nyie
 
mmm spare wanazo nyingi sana hata magari wanayo ya kila aina hata matapeli wanao wa uhakika mimi nilikuwa na gari aina ya Fiat 124 nilikuwa natafuta piston rings pamoja na oil seal nilivipata huko mwaka 1991, labled Fiat 124 na oil seal lakini piston rings kipenyo kilikuwa kikubwa ila oil seal ilikuwa yenyewe huko kuna mambo mengi bana. Here were are sharing experiences
Nikweli penye amani hapakosi vurugu, uzi wa huku spare mpaka magari ya zamani unapata
 
South Afrika kuna magari yote yanayopatikana Duniani kwa maana kwamba wana manufacturing plants kabisa mfano Toyota Fortuner inatengemezwa South Africa.

Ila usidanganywe msamaha ama unafuu wa kodi ukiagiza gari South Africa.

Makubaliano ya SADC ya kusameheana kodi kwa vitu vilivyotengenezwa ndani ya nchi wanachama yanahusu kitu kikiwa brand new tu.

So ukiagiza gari South, brand new, ukapata certificate of origin ukafika nayo TRA hakuna kodi, ila kama ni used car kodi ni sawa na kodi za Japan ama kwingineko.

Watu wasidanganywe, kodi ni jambo la muhimu sana kulikua kabla hujanunua kitu chochote nje ya nchi.
 
Inakuaje gar km crown ya 2014 inauzwa million65 sa je nkiitaji crown ya 2023 si ndo itauzwa million 200

Wauza magar tunaomba mtupe elimu kdg izi garama za magari ni kubwa mno na gar zenyewe ni nzee chakavu
Gar za 2002 to 2014 why zinakua na bei juu wakat ata uko zilikotengenezwa zilishatoka kwenye mzunguko/ mfumo

Na magari huwa yanatengenezwa kwa mwaka wa mbele mfano saiv ni 2023 ila gari za 2024 zishatoka na zinatembelewa
Saiv toyota japan washatengeneza crown ya 2024 ipo na iko sokoni

Nimetolea mfano gari za kijapan na kikorea sabu ndo watanzania weng wanaweza kuzimiliki na kununua
 
Habari za leo waungwana.

Mimi nataka kuagiza used gari kutuka nje na nime narrow down kwenye hizo nchi kwani ndio nimeambiwa magari mengi yanatoka huko

Mazingatio makubwa kwangu ni Uimara, usalama na matengenezo ( japo nimeambiwa gari ambayo haijatumika sana hugharamiki sana matengezo au spares) ushusu na gharama za matunzo

SOUTH AFRICA:
Sijajua kuna siri gani ya haya magari kutoka South Africa lakini sijapata kuona gari yenye namba plate za SA hapa mjini ambayo imechoka au iko kuu kuu...iwe Ford, Toyota Fortuner, Land Rover Discovery au BMW...unaona kabisa gari kama vile imetoka kiwandani....na mara nyingi ambazo nation zina namba plates za jimbo la GAUTENG...

Kila ninapouliza Why South Africa and not UK sipewi majibu yaliyonyooka kwani kila mmoja amekuja na theory yake lakini kwa kifupi wao husema:
  1. Mengi ni magari ya kupigwa hivyo ni cheap
  2. Wepesi wa kuingiza Tanzania kutoka SA. Minimum wiki moja gari ishaingia
  3. Hakuna longo longo kubadãilisha plate
  4. Ushuru ni mdogo kwa sabot country of origin ni SADC
  5. Ubora wa gari ni mzuri Kwani yametengenezwa kwa ajili ya ya terrain ya Africa

JAPAN & SINGAPORE:
Magari ya kutoka huko niyaonayo mengi naona yamepigwa sop sop lakini sio kama ya SA lakini naona ndio yanayoonekana ni affordable kwa mwananchi mengi hapa wenye kipato cha juu na chini na lakini pia nimeona yaliyppata ajali ni kama vile Yai kwa jinsi yanavyobondeka na survival rate kwa ajali nilizoona ni ndogo sana.

UK:
Sijaona mengi ambayo yanayo shine na kuonekana mapya kama ya SA lakini huwa najiuliza hivi Mzungu anaweza kutengeza gari sub standard (ubora na usalama) kwa jili ya soko la UK au Ulaya na kisha akatengeneza gari bora zaidi kwa ajili ya soko la Africa kwa sababu mazingira na bara bara mbovu za Africa?

Naomba nifafanuliwe based on:
  1. Ubora na Usalama
  2. Gharama za kuitunza
  3. Bei (kutokana na Sababu hizo hapo juu)
  4. Ushuru

Ahsanteni sana waungwana
South Africa ni the best. Ukihitaji usaidizi, mtafute Isanga family, naamini hatakuangusha!
 
South Afrika kuna magari yote yanayopatikana Duniani kwa maana kwamba wana manufacturing plants kabisa mfano Toyota Fortuner inatengemezwa South Africa.

Ila usidanganywe msamaha ama unafuu wa kodi ukiagiza gari South Africa.

Makubaliano ya SADC ya kusameheana kodi kwa vitu vilivyotengenezwa ndani ya nchi wanachama yanahusu kitu kikiwa brand new tu.

So ukiagiza gari South, brand new, ukapata certificate of origin ukafika nayo TRA hakuna kodi, ila kama ni used car kodi ni sawa na kodi za Japan ama kwingineko.

Watu wasidanganywe, kodi ni jambo la muhimu sana kulikua kabla hujanunua kitu chochote nje ya nchi.
Duh, humu jukwaani tulikua tunadanganywa kumbe. Asante kwa taarifa mkuu
 
My Take
South Africa:Gari za SA nyingi zimetengenezwa kwenye plant zao wenyewe,na hivyo hata ukipata gari used bado ipo kwenye hali njema.Gari nyingi za SA pia ni full option--kwa mfano hilux ya SA na ya Japan,ya SA ina manjonjo zaidi inakuwa na auto windows,alloy rims,na nyingi turbo huwa ni standard.Gharama za usafirishaji kutoka SA ni nafuu kama ukipata nafasi kwenye lorry--ubebe kama mzigo-clearance unakuja kufanya mwenyewe huku.au kama unapenda adventure uendeshe mwenyewe--roughly 4-6 days(ANGALIZO--SA kuna matapeli haswa---na gari za wizi ni nyingi mno--hukawii kudakwa na interpol gari yako ikabebewa huku).Gari za uhakika utapata kwa pre-owned dealership--nizijuazo ni Automark SA,Naledi Motors,White Rhino motors na Halfway.Ford,CFAO na TOyota nao wanazo ila bei ni mkasi balaa.
UK-Gari za UK nazo ni nzuri na ni rahisi sana kupata manual transmission.Shida kubwa ya gari za UK ni kuoza chasis kutokana na mazingira ya chumvichumvi uingereza.Kama utaagiza gari UK hakikisha una mtu kule atakayekagua chasis na body.Na kama huna hakikisha MOT certificate haizidi miezi 6(zipo za kupika pia--kwahiyo uwe makini).Kama una mtu kule agiza--transfer ya gari hadi Tanzania RORO kwa kukadiria ni 2000£ uweke na ya TRA hapo.
ANGALIZO:Kuna gari za UK haziingiliani spare parts na hizi za kijapani ambazo zipo nyingi hapa nchini.Pia mileage zao zipo kwa miles--usije ingizwa cha kike ukanunua above 80,000miles---litakufia tu mapema
JAPAN:Gari nzuri pia,na zimezoeleka kwa wengi.Ni bahati yako na kuchagua kwako.
Kila la heri.

Gari zenye tow hitch(kama unapenda kuvuta trailer na ni mtu wa shamba---mostly utapata gari zuri kwa bei nzuri UK na SA--Japan ni pazuri kwa saloon cars na gari za bata zaidi.
 
Mfano ukaagiza scania 94D kutoka UK ilikuwa flatbed ukatoa ikabaki chasis kodi itapingua wakati wa kuleta huku na itaingia kwenye category ya flatbed au tractor kwenye tra calculator
 
Nani alikuambia wanigeria wanauza magari wewe na chumvi wamuachie nani?..SA kuna auction nyingi sana za magari na ukitaka kitonga nunua iliyo gongwa kidogo SA ni wakali wa panel beating inyooshe piga rangi upya ikitua bongo ni salute mtu hawezi jua liligongwa. Showroom zimejaa kila kona wewe ukanunue kwa mnigeria siutakuwa chizi. Kama unataka ndinga SA nenda mwenyewe utapata gari kali bei kitonga
Na siyo kila Mnigeria ni tapeli, kama ambavyo si kila Mtanzania ni mkarimu.
 
SA magari mazuri na bei kitonga tatizo zimetembea sana nyingi abv 100k kwenye clock
 
Mpaka wazungu hawamuamini mnigeria wewe ndio unajifanya kiherehere utalizwa hautaamini
Kwa hiyo na Aliko Dangote tumzuie asiendelee na uwekezaji nchini?

Mmoja wa Walimu wangu Chuoni alikuwa Dr. Nwoye. Japo alikuwa Mnigeria, sikuwahi kuona chembe ya utapeli kwake. Sana sana nilimfurahia kwa jinsi alivyokuwa anajua kutunza muda.

Samaki mmoja akioza si wote! Kuna Wanigeria wengi tu ambao hata ukiiangusha wallet iliyosheheni madola hawatajibinafsishia.
 
Back
Top Bottom