Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?




mimi ninaswali MziziMkavu kutokana na hii ujumbe wako nilio quote.....je kwa wale wanakua na nyumba ambazo ni self yaani choo na sehemu ya kulala almost vipo karibu hapa unashauri nini maana shetani nae anapenda kukaa chooni sasa nyumba yako ni self hii sasa si nihatari sn kwakua utakua umewaleta kabisa karibu yako...nini cha kufanya kwa mazingira kama hayo.
 
Kwa sisi Waislam unapokwenda choo kuna dua unasema Hivi (Allahuma ini Audhubika minal khubthi walkhabaithi) Maana yake kwa kiswahili Ewe Mwenyeezi Mungu ninajilinda kwako kutokana na shetani Mwanamke na shetani mwanamme ndipo unaingia kwa kutumia mguu wa kushoto na kutoka unatoka na mguu wa kulia. Ukisha toka unasema hivi (Ghuf-ranaka) na unaufunga mlango kwa kutaja jina la Allah (Bismillahi rahmani rahim) Ukisema hizo dua unapoingia chooni yule shetani awe Mwanamke au Mwanamme anakimbia anakupisha mpaka utoke umalize haja zako huko chooni. Na wakati wa kutoka ukisema hiyo Dua unamzuia asikufuate au kuja vyumba vingine zaidi ya kukaa chooni. Kwa Dua ya Wakristo siijuwi nitajaribu kuitafuta nikipata nitakupa.
 


thanks MziziMkavu kwa ujumbe huu nami nitafuatilia kujua pande zote 2,watu wanaona ni vitu vidogo ila vinamadhara sana kwenye maisha yetu ya kawaida...thanks mkuu
 
Mkuu MziziMkavu ka unamwomba Mungu kabla ya kuingia na kutoka, kutanguliza miguu kuna husikaje?
Mungu hana masharti ya kihivyo, upande wowote yupo, kama kakubali ombi lako anavunja nira zote za mashart ya kutanguliza miguu.

Kama mungu hana mashart mbona mkono unachambia chooni sio unaotumia kula chakula? na kasema mle wa mkono wa kulia na mambo ya haja mkono wa kushoto? acha kujbu ujinga mwenyezi mungu ana hekma kulko wewe.....
 

Usipende kudandia usichokijua bora kusikilizia !

Dua ta chooni haianzi na bismillahi
 
Kuanguka chooni huwapata wale wenye shinikizo la damu.
Ukiwa chooni na umechuchumaa, utasababisha damu isiende sehemu nyinge mfano za miguu, hivyo kusababisha presha.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?
 
Kiimani chooni ni mahala pachafu....ambapo hukaa viumbe wachafu.....na wabaya....ambapo wakati mwingine hukumbana na wanadamu katika shughuli zao...na hayo ndio huwa matokeo yake......

Au wakati mwingine kwenye nyumba za kupanga unakuta mwenye nyuma amehifadhi wadudu wake huko.....ambapo muda mwingine huleta madhara kwa watumiaji wa choo hicho.....

Matukio mengi ya kukumbana na wadudu huwa yanatokea usiku sana....au mchana ile mida ya ibada za kiislamu.....

Wakati mwingine kibaolojia...mtu anaweza akateleza huko chooni akajikuta anaangukia sehemu mbaya ya mwili wake...hasa hivi vyoo vyetu vya kiswahili....ambavyo ni vidogo sana....kiasi kwamba ukikisa balance ukikteleza unajikuta umepigiza kichwa ukutani.....na kupoteza maisha....
 
Asante kwa majibu mazuri mkuu.Je kuna uwezekano pia viumbe hawa wachafu kukaa sehemu nyingine ambazo ni chafu kama dampo au kwenye majalala?
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?

Sasa kama mavi / makimba tu yenyewe ukiwa kule Chooni yanaweza kukufanya uwe Chizi kwa harufu yake kali na iliyotukuka kwanini ikitokea bahati mbaya umeanguka humo humo Chooni usife Mkuu?
 
Wanaoanguka wengi wanamagonjwa ya presha, kitendo cha kukunja miguu kina restrict damu ku flow inavyopaswa, hivyo kuanguka kwe tiles, ambapo anaweza kutana na concuntion ka ile ya Kanumba. Hamna uchawi wala nn.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?
Fanya analysis ya kitaalam upate jibu.
Wengi ni stroke!
Na inasababishwa na msukumo mkubwa wa damu baada ya kujitia maji ya baridi mwilini.
 
Asante kwa majibu mazuri mkuu.Je kuna uwezekano pia viumbe hawa wachafu kukaa sehemu nyingine ambazo ni chafu kama dampo au kwenye majalala?

Sifahamu mahusiano ya moja kwa moja ya wadudu wabaya na huko chooni.....ila ninachojua ni kuwa wengi hupendelea kukaa huko ingawa sijui ni kwa sababu ganj......ndio maana muda mwingine unashauriwa kama umeshamaliza haja zako...basi ni vyema ukatoka huko haraka......

Vile nadhani nadhani huko chooni ni sehemu tulivu kwa kuwa sio muda mwingi unakuwa na msongamano wa watu....tofauti na dampo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…