Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?
Asilimia ya watu wangapi kati ya ngapi?? tuanzie hapa kwanza
 
Vifo vya chooni wala havina uhusiano na ushirikiana au nguvu yoyote ya giza, kikawaida % kubwa ya vifo vya chooni/ bafuni watu huanguka kwa kuteleza na mara nyingi huangukia kichwa upande wa nyuma kubamiza chini yaani eneo la chini kidogo ya kisogo ambapo hata ukiwa umesimama na mtu akakupiga eneo hilo na kitu kizito na kwa nguvu basi uhai wako uko mashakani.
 
Mkuu wadudu gani wabaya wanakaa huko? Kwenye vyoo vyetu vya Kibongo visivyo safishwa Mara nyingi wanaokaa huko Ni Mende, nzi Na funza au panya.Je, hao Ndio wanaweza kumfanya mtu afe? Kaka Jambazi Na Masopakyindi wameeleza sababu za kitaaluma sana ambazo Ndio chanzo.

Sifahamu mahusiano ya moja kwa moja ya wadudu wabaya na huko chooni.....ila ninachojua ni kuwa wengi hupendelea kukaa huko ingawa sijui ni kwa sababu ganj......ndio maana muda mwingine unashauriwa kama umeshamaliza haja zako...basi ni vyema ukatoka huko haraka......

Vile nadhani nadhani huko chooni ni sehemu tulivu kwa kuwa sio muda mwingi unakuwa na msongamano wa watu....tofauti na dampo....
 
Kiimani chooni ni mahala pachafu....ambapo hukaa viumbe wachafu.....na wabaya....ambapo wakati mwingine hukumbana na wanadamu katika shughuli zao...na hayo ndio huwa matokeo yake......

Au wakati mwingine kwenye nyumba za kupanga unakuta mwenye nyuma amehifadhi wadudu wake huko.....ambapo muda mwingine huleta madhara kwa watumiaji wa choo hicho.....

Matukio mengi ya kukumbana na wadudu huwa yanatokea usiku sana....au mchana ile mida ya ibada za kiislamu.....

Wakati mwingine kibaolojia...mtu anaweza akateleza huko chooni akajikuta anaangukia sehemu mbaya ya mwili wake...hasa hivi vyoo vyetu vya kiswahili....ambavyo ni vidogo sana....kiasi kwamba ukikisa balance ukikteleza unajikuta umepigiza kichwa ukutani.....na kupoteza maisha....
hapo nilipo bold umeandika vitu vyakusadikika tuu .ila kwenye swala la kiimani sehemu za uchafu ni langu la kuzimu

Hapo kwenye hoja ya kibailojia ndo penye jbu halisi nikisema halisi maanake ni proved scientifically
 
Wanaoanguka wengi wanamagonjwa ya presha, kitendo cha kukunja miguu kina restrict damu ku flow inavyopaswa, hivyo kuanguka kwe tiles, ambapo anaweza kutana na concuntion ka ile ya Kanumba. Hamna uchawi wala nn.
Nahisi kuna ukweli hapa.
 
Vifo vya chooni wala havina uhusiano na ushirikiana au nguvu yoyote ya giza, kikawaida % kubwa ya vifo vya chooni/ bafuni watu huanguka kwa kuteleza na mara nyingi huangukia kichwa upande wa nyuma kubamiza chini yaani eneo la chini kidogo ya kisogo ambapo hata ukiwa umesimama na mtu akakupiga eneo hilo na kitu kizito na kwa nguvu basi uhai wako uko mashakani.
Asante mkuu.
 
Sasa kama mavi / makimba tu yenyewe ukiwa kule Chooni yanaweza kukufanya uwe Chizi kwa harufu yake kali na iliyotukuka kwanini ikitokea bahati mbaya umeanguka humo humo Chooni usife Mkuu?
Una majibu ya kibabe sana mkuu[emoji87]
 
Hakuma uhusiano wa choo/bafu na hivyo vya watu kufa huko na madudu ambayo mleta uzi ameyataja, sema kwa sababu mtu anakufa ndio maana tunapata taarifa lakini wapo wengi wanaanguka kwa kuteleza bafuni na kuumia vibaya lakini wanapona.
Mapepo na mazindiko yako kila mahali cha msingi Kuwa na imani ktk Kristo Yesu tu
 
Sisi wenye imani ya dini ya kiislam,tumefundishwa kuingia vyooni kwa dua na kutoka kwa dua,nafikiri kuna maana kubwa sana kwenye dua hizi.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?
Choon ni kama ikulu tu si mahali patakatifu.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.Tangu nikiwa mtoto nimekuwa nikisikia matukio ya watu kuanguka chooni na kufa lakini mpaka utu uzima wangu huu bado sijajua sababu.Je hali hii hutokana na matatizo ya kibaiolojia au imani za kishirikina?
Kumbe umesikia hujaona?..mbona me nimeanguka Mara kibao chooni sijafa
 
Kiimani chooni ni mahala pachafu....ambapo hukaa viumbe wachafu.....na wabaya....ambapo wakati mwingine hukumbana na wanadamu katika shughuli zao...na hayo ndio huwa matokeo yake......

Au wakati mwingine kwenye nyumba za kupanga unakuta mwenye nyuma amehifadhi wadudu wake huko.....ambapo muda mwingine huleta madhara kwa watumiaji wa choo hicho.....

Matukio mengi ya kukumbana na wadudu huwa yanatokea usiku sana....au mchana ile mida ya ibada za kiislamu.....

Wakati mwingine kibaolojia...mtu anaweza akateleza huko chooni akajikuta anaangukia sehemu mbaya ya mwili wake...hasa hivi vyoo vyetu vya kiswahili....ambavyo ni vidogo sana....kiasi kwamba ukikisa balance ukikteleza unajikuta umepigiza kichwa ukutani.....na kupoteza maisha....

Hivi kwa nini hii dini inahusishwa sana na haya mambo ya nguvu za giza?
 
Fanya analysis ya kitaalam upate jibu.
Wengi ni stroke!
Na inasababishwa na msukumo mkubwa wa damu baada ya kujitia maji ya baridi mwilini.
Na ndiyo sababu inashauriwa zoezi la kuoga maji baridi liende taratibu na kwa awamu, usianze kwa ghafla tu,ni vyema ukaanza miguuni,ukawa unapanda juu taratibu na kichwani iwe ni sehemu ya mwisho, pia unapotoka kwenye jambo linaloweza kuwa limesababisha mabadiliko ya msukumo wa damu mwilini (mfano mazoezi ya mwili, au mechi za kitandani ni vyema kuruhusu mwili kupoa kwanza kabla ya kwenda kuoga, pia ni vyema kuhakikisha unaepuka kupata choo kigumu kitakachopelekea kujikamua sana wakati wa kukata gogo jambo ambalo hufanya BP kupanda (na hii ni muhimu zaidi kwa watu wenye hypertension),kama pressure tayari ilikuwa juu ukijumlisha na ile inayopanda kwa kujikamua kuna uwezekano wa stroke,Pia unapoamka usiku mkubwa kwenda kujisaidia usiamke kwa ghafla ili kuweza kuruhusu ubongo kupata damu ya kutosha tena,anza kwa kukaa kitanda kwa dk chache,shusha miguu chini halafu subiri kidogo halafu nenda kajisaidie-zoezi hili unaweza kulifanya kama ndani ya dk tatu hivi zinatosha,ukikurupuka na kuwahi chooni tu unaweza kwenda kuangukia chooni kutokana na physiological changes hizo (ukajikuta unaishia kkuamini kuwa usiku mkubwa kuna majini chooni), kunaweza pia kukatokea ajali za kawaida kama kuteleza na kupiga kichwa chini so kujitahidi kuepuka visababishi vya utelezi chooni na bafuni.
Inawezekana na sababu za kiimani zipo lakini hizo hapo juu pia zina mchango kwa asilimia kubwa.
 
nakumbuka nilidondoka chooni mabibo hosteli sema nilitanguliza kiwiko ila kwa kweli ningelifikia kisogo nadhani ningelikuwa marehemu maana ilikuwa chali mbaya
 
Naona Mnalishana Kasa Tu. Kwanza Utelezi Si Sababu Kuu Ya Kuanguka. Na Aliye Na Afya Njema Anaweza Kuanguka Ila Ni Kwa Utelezi Na Bado Akaamka Na Kuendelea Na Haja Zake. Tatizo Kubwa Ni Maradhi Ya Moyo Na Shinikizo La Damu. Mtu Anapochuchumaa Ku.nya Husababisha Mkandamizo Wa Damu Kwenye Mishipa Dhaifu. Anapoamka Presha Huongezeka Hivyo Damu Inashuti Na Ikikuta Sehemu Dhaifu Inapasua. Hasa Kichwani. Tahadhari Ni Kutumia Vyoo Vya Kukaa Hasa Kwa Watu Wa Makamo. Pili Ni Maji Ya Baridi Wakati Wa Kuoga. Hayo Maji Hufanya Mishipa Ya Damu Kusinyaa Hivyo Kuongeza Presha Ya Damu Hivyo Inapasuka. Tahadhari Ni Kuogea Maji Ya Vuguvugu Hasa Kwa Watu Wa Makamo
 
Back
Top Bottom