Na ndiyo sababu inashauriwa zoezi la kuoga maji baridi liende taratibu na kwa awamu, usianze kwa ghafla tu,ni vyema ukaanza miguuni,ukawa unapanda juu taratibu na kichwani iwe ni sehemu ya mwisho, pia unapotoka kwenye jambo linaloweza kuwa limesababisha mabadiliko ya msukumo wa damu mwilini (mfano mazoezi ya mwili, au mechi za kitandani ni vyema kuruhusu mwili kupoa kwanza kabla ya kwenda kuoga, pia ni vyema kuhakikisha unaepuka kupata choo kigumu kitakachopelekea kujikamua sana wakati wa kukata gogo jambo ambalo hufanya BP kupanda (na hii ni muhimu zaidi kwa watu wenye hypertension),kama pressure tayari ilikuwa juu ukijumlisha na ile inayopanda kwa kujikamua kuna uwezekano wa stroke,Pia unapoamka usiku mkubwa kwenda kujisaidia usiamke kwa ghafla ili kuweza kuruhusu ubongo kupata damu ya kutosha tena,anza kwa kukaa kitanda kwa dk chache,shusha miguu chini halafu subiri kidogo halafu nenda kajisaidie-zoezi hili unaweza kulifanya kama ndani ya dk tatu hivi zinatosha,ukikurupuka na kuwahi chooni tu unaweza kwenda kuangukia chooni kutokana na physiological changes hizo (ukajikuta unaishia kkuamini kuwa usiku mkubwa kuna majini chooni), kunaweza pia kukatokea ajali za kawaida kama kuteleza na kupiga kichwa chini so kujitahidi kuepuka visababishi vya utelezi chooni na bafuni.
Inawezekana na sababu za kiimani zipo lakini hizo hapo juu pia zina mchango kwa asilimia kubwa.