MtoMsimbazi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2009
- 1,800
- 3,091
Bibie.Diana Fares Majin na Mashetani yapo na yametajwa pia katika Biblia hebu soma hapa
Majini na Shetani, ni nini tofauti yake?
Math. 16: 22-23.
MASKANI ZA MAJINI. (WANAMOISHI)
Ndugu yangu msomaji umuhimu wa elimu hii ni kubwa sana, kwani Mwenyezi mungu ametupa tahadhari sana kuhusiana na Shetani kiumbe wake. Kwani yeye Mwenyezi mungu ndiye alie muumba na yeye mwenyezi Mungu ndiye alietupa habari kujikinga naye huyo Shetani. hivyo basi ni vyema kutambua baadhi ya sehemu ambazo anakaa au anaishi shetani. Sehemu hizo nazitaja kama ifuatavyo:
MAJANGWANI- Ni sehemu ambayo hupenda sana kukaa Shetani au Jini, hivyo ni vyema kupita sehemu hiyo kwa dua (dhikri) maalum.
NYUMBA ZA BINADAMU- Pia hukaliwa na majini wa kishetani pia ni vizuri tukalifahamu hilo na kuishi maisha ambayo mwenyezi mungu anayaridhia.
MASHIMO YA TAKA TAKA- Ni moja katika sehemu za Shetani kukaa au kuishi, kwa hiyo ni muhimu sana kuchukua tahadhari.
MAPANGONI- Pia ni sehemu ya tahadhari kwani jini anaamini kwamba ni sehemu tulivu.
CHOONI- Ni sehemu ilio faragha pia ni sehemu ya hatari sana mara nyingi mtu akianguka chooni hupata madhara makubwa sana. hivyo ni vyema kuingia sehemu hii na dua maalum.
MITI MIKUBWA- Pia hupendelea kuishi au kukaa majini, miti hiyo ni kama vile mbuyu, msufi. N.K.
VISIMA- Hii ni sehemu ya muhimu sana kwa majini kukaa au kuishi katika maisha yao, pia ni muhimu sana kwa maisha ya binadam. Hivyo ni muhimu sana twende visimani tukiomba dua za ulinzi.
MITO- Pia ni sehemu muhimu sana kwa wanadamu alafu pia ni sehemu ambayo hupenda kuishi au kukaa majini. Hivyo ni muhimu kukumbuka dua wakati tupitapo au twendapo mtoni kwa shida ya muhimu.
MABWAWA- Ni sehemu ambayo hupenda sana kuishi au kukaa majini, tena na watoto wengi hupenda kuoga katika mabwawa. Kwa hiyo ni lazima tuyafahamu hayo.
BAHARINI AU MAZIWANI- Nayo ni sehemu ambayo wanaishi majini au mashetani. pia si sehemu ya kudharau, ni vizuri kulitambua hilo na kujikinga nalo kwa dua au maombi kutoka kwa Mwenyezi mungu.
MILIMANI- Ni sehemu muhimu kwa majini na hupenda sana kuishi au kukaa. Pia ni lazima kufata sheria zote ambazo kwa waislamu Mtume amefundisha pia kwa wakristo wanamaombi yao yakiwa kama kinga.
KATIKA MWILI WA BINADAMU- Shetani anaweza kuishi au kukaa katika mwili wa binadamu pasipo binadamu kugundua. Hii inatokea kama shetani huyo katumwa aje kwako na mtu fulani au kapenda mwenyewe kuingia katika mwili wako.
Ndugu yangu msomaji baada ya kutambua, kujua, kufahamu na kuelewa sehemu ambazo waishizo majini au mashetani basi ni lazima kuwa makini na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushie matatizo mbalimbali. Kila chenye kuumbwa huumbwa kwa makusudio ya mwenye kuumba na kila chenye kutengenezwa hutengenezwa kwa makusudio ya mwenye kutengeneza.
Mkuu Mwanahip Nipo tu vipi wewe hali ya maisha huko uliko?
mimi ninaswali MziziMkavu kutokana na hii ujumbe wako nilio quote.....je kwa wale wanakua na nyumba ambazo ni self yaani choo na sehemu ya kulala almost vipo karibu hapa unashauri nini maana shetani nae anapenda kukaa chooni sasa nyumba yako ni self hii sasa si nihatari sn kwakua utakua umewaleta kabisa karibu yako...nini cha kufanya kwa mazingira kama hayo.

