Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

ni kwelikabisaaa... Ndo maana sisi waislamu tunaambiwa tutangulize mguu wa kushoto wakati wakuingia chooni ili ukiteleza uangukie nje( fanya majaribio utakubali hii kitu...) na kuomba dua ya kujikinga na mashetani wa chooni na kutoka tutangulize wa kulia( ili ikitokea bahati mbaya umeteleza uangukie nje pia..) na kuomba dua ya kumshuluru mungu kwa kutuondolea maudhi ya haja zetu zilizotupeleka huko.... Ila pia mtume s.a.w. Aliwahi kusema kuwa binadamu angepewa uwezo wa kuona mashetani wa chooni basi angekjisaidia vichakani maisha yake yote. Asante!!
Aiseee...kwahiyo ukiwa kwenge chumba cha choo kabisa. Utangulize mguu upi?? Haya ni maji ya kumezeshwa illogical.
 
Lakini medula iyoiyo ukianguka nje ya choo unaweza usife unaona iyo
Sasa kuangukia mchanga unafananisha kwenye masink... hata wagonjwa wa kwanza wa kipindupindu na ukimwi... walikuwa wakifikir ni uchawi. Ndii akili zetu zinapofanyia kazi....
 
Ni mambo ya kimwili zaidi na wala sio ushirikina
Basi kama ndio ushirikina tungekufa wengi,
Hamna jini wala mchawi
Ni mambo ya kimwili.
Either kuna kitu kwenye mwili wa mwanadamu umefeli ghafla au magonjwa hivyo kufa,
Ila hili ni suala la kimwili mtafute dokta mtaalamu wa masuala ya damu, mishipa, na mwili mzima kwa ujumla,
 
uko sahihi sana mkuu pamoja sio medical personel umejitahidi kuelezea kisayansi fulani. Ukisoma forensic medicine wanaeleza hivyo sasa kwa nyongeza ni kuwa ni kwamba % ya watu wanaoanguka chooni huanguka kinyume nyume na kuangukia kisogo kinachotokea pale ni kuwa kutokana na uzito wa mwili akianguka fuvu hupasuka na unajua likipasuka fuvu nini kitatokea. Wale wanaopalalyse inategemea ameangukaje na force aliyotumia kuanguka nayo. Kwa hiyo chooni hakuna kitu ila ni utelezi unaosababisha kuanguka. Medically tunashauri vyoo visakafiwe non slipperly floor. Na ukiangalia waliowengi wanaoanguka ni wazee na watu wa makamu /wagonjwa hii inaelezwa pia mtu as anaprogress kwa age balance inapungua. Nitajitahidi ni waletee shule nzuri kuhusu hili i promise. Tuachane na fikra za kishirikina. Hasa vyoo vile vya kukaa ndo vibaya zaidi coz lile sink linaact kama panga au kompressor tofauti na vyoo vya shimo au vile vya kuchuchumaa. Nawakilisha.
naunga mkono hoja.pia wengi hawasafishi vyoo kwa kusugua vema hata kama si vya tails ukiteleza tu imekula kwako
 
kama ni kweli basi mm ningekua nimeshakufa maana kuna ck nilianguka bafuni kwangu nikapigiza kichwa nilihc kuzimia ila nikaamka nikaendela kuoga
Wee utakuwa ulikipapasa
 
Nadhan iko shida ambayo lazima watu tufanye tafit ya kina maana mi nana ushahid wa watu 2 walioanguka hayo maeneo.Wa kwanza ni marehem mama yangu yeye aliwai kuanguka akaumia goti na ilo goti pamoja nakulitibu kwadawa mbalimbali halikupona lilimsumbua karbu miaka 3 badae akapata stroke upande huo huo wa goti ambayo ilidumu kwa muda badae ikampiga pande zote akaaga dunia.Mwingine ni shemej yangu ambaye nae alianguka tena kwenye bafu la kienyej akapooza mguu mmoja ambao ameutibu namazoezi sasa hiv anatembea ila kwa gongo nakuuburuza huo mguu na nikaribu miaka 2 sasa yuko na iyo hali.Kabadilisha hospital ila bado vipimo vinaonyesha hakuna tatizo.Kwaiyo nadhan iko shida ukianguka ayo maeneo japo sio lazima wote wanaoanguka lazima wapate shida au wafarik.Ninachojiuliza ni ichi kua kwanin weng wanaoanguka nakupata shida huwa wanachelewa kupona na weng lazima wapooze.
 
Mkuu kwa wapiga puri inakuwaje? au hao viumbe wanakuchukuliaje wakiona unapiga puri? sijawahi sikia mpiga puri kaanguka chooni, au ukianza kupiga puri hao majini wanaondoka?
Hahahahahahahahahaha
 
Mi ninachojuwa kuwa vyoo vyetu ni vyembamba na vidogo Kwa hiyo mtu akianguka choon tunategemea hata kosa balance ya kutanguliza mikono Chini badala yake kichwa ndo kitakuwa cha kwanza kugusa ukutu wa pembeni. Jaribu kufikiria wewe ukianguka sehem ya wazi tunatarajia mikono yako kufanya kazi za ziada.
 
Pia tambua kwa nn mtu pia anakufa ukianguka segemu yenye utelezi kama wa sabuni speed ya kwenda chini kasi ya hali ya juu

kwa kuwa kuna kuwa na sabuni hata mikono haiwezi kushika chini

Kutokana na utelezi lazima kichwa kiwe ndio mhanga

Na ndio maana ni rahisi kufa
 
Habarini wapendwa poleni na uchovu. Kuna baadhi ya vitu huwa vinatokea kwenye jamii tunapaswa kujua ni kwanini vinatokea katika mda nilioishi hua nasikia na kushuhudia matukio ya watu kuanguka chooni lkn ikitotea lazima atakufa au kupalalaizi kiungu hii ni kwanini ebu tupeane uzoefu hapa kidogo
 
Wapendewa ngoja tueleweshane lakini natumia maneno.ya imani flani ok ndani ya choo siku zote wanakaa majini yaani wadudu wachafu ...humo wanakaa wa aina zote wanawake na wanaume ..na wanaendelea kuzaliana kwa za hadithi za mtume mohammad (s a w) ametusisitiza jinsi ya kujikinga na kuwaepuka majini hawa kwa kusoma dua ...na hawa wataondoka na kukaa mbali na wew kumbuka hawa wanatembea kama mama sisi wanaona kama sisi sasa mara nyingi huwa milangoni na pindi unakutana nao hao hapo malangoni au ndani ndio mwanadamu huweza kujitambua au kupungwa kikumbo au lolote hufanya .... Kwanin wanaoanguka wanapata madhara makubwa hadii kupoteza maisha mtume ametoa utaratibu wa kuingia chooni soma dua la kujikinga kisha tanguliza mguuu wa kushoto kisha fuata wa kulia ...hii kwa sababu viungo vingi vizito katika mwili wa mwanadamu ini pafu bandama kongosho..nk vipo upande wa kulia unapotanguliza mguu wa kushoto ndani akitokea baati mbaya ukaanguka hutoangukia ndani maana upande mzito wa mkono wa kulia upo.nje na upande wa kushoto.wenye moyo na pafu upo.ndani ....na ukiangukia nje hao jamaa hawapo .....hii haitokuwa na madhara kwako ....na muda wakutoka chooni omba dua kisha tanguliza mguu wa kulia maana umetoka kwenye uchafu unaingia eneo safi na hapo ukianguka utaangukia nje kwenye mguu wa kulia ulio mzito .....na nje majini hayapendi kukaa ...na majini chakula chao kinyesi hasa kikavu.......SORRY KWA WENYE IMANI YA DINI YA KIISLAMU LAKINI.
 
Kwa jinsi ninavyojua mimi kidogo,kuanguka chooni au bafuni kunasababishwa vitatu, shinikizo la damu ambalo mgonjwa anakuwa nalo pasipo kujitambua,yaweza kuwa la juu au la chini,vitendo vya kuinama au kuchuchumaa na kuamuka,au kujimwagia maji baridi mwili hushutuka,ubongo huhusika zaidi na kuufanya mwili upoteze uwiano,kumbuka masikio pia huwa na kimiminika ambacho huuweka mwili sawa nayo hutikisika na kuutarifu ubongo na mara nyingi mtu huvutika kulalia nyuma na kwa vile kisogo huwa kimechongoka mkandamizo na kishindo cha mwanguko huwa mkubwa na madhara kwenye ubongo huwa makubwa ndo maana wengi hufariki au kupooza,ukitaka kujaribu tumia bomba la mvua mtu alifungue pasipo wewe kujua,au inama na kuamka ghafla dalili utaziona,ushauri tumia maji vuguvugu,kama unaumwa epuka kuinama na kuamka ghafla,pima shinikizo la damu mara kwa mara.
 
Chooni tunawela slippery tiles..

Chooni hatushafishi..

Chooni unatumia ndala zenye smooth surface..

Chooni umemwaga povu la Omo hujasafisha..




Sasa kwanini usianguke?
 
Back
Top Bottom