Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

kuna siku niliingia bafu lenye tiles... wakati naoga nikakumbuka kitu Fulani ikabidi nianze piga nyeto.... balaa ilikuwa pale wazungu walipotaka kutoka... nilijikuta naishiwa nguvu halafu nikateleza, ebana nilijibamiza sakafuni asikwambie mtu.... lakini nipo mpka leo

Mjomba acha puchu!!!!
 
Nimewahi kusikia kuna mmoja alianguka lakini hakufa alfajiri ilkuwa na wakati wanampeleka hospitali alikuwa akilalamika kukutana na mtu mkubwa sana ambaye alimbana na kumuumiza sana alikuwa akiirudia hiyo kauli mara nyingi alikata kauli njiani na alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini source; mama wa rafiki yangu ambaye ni ndugu wa marehemu
Kama naijua hii story!!
Mjomba wangu pia alianguka chooni akafariki,ila madaktari walisema presha. Na wapo pia wanaoanguka na hawafi wala kuugua.
 
mambo mawili yote yanawezekana kuhusu kuanguka chooni na kuugua na hatimae kufa. (1) inawezekana inatokana na pressure kwa sababu ndani ya choo hasa vyoo vya mashimo vinakua na mkandamizo wa hewa wa hali ya juu, ambao hupelekea hadi pressure ya mtu kutokana na msukumo wa damu wakati wa kujisaidia ukazidi kupanda na kuleta shida (kwa hiyo tujaribuni kula matunda na vitu vya mataka ili kulainisha choo). (2) chooni kama walivyochangia akina MziziMkavu kuna majini mabaya, ambayo humshambulia mtu anapokua uchi, pia ikumbukwe kwamba ukiingia chooni wale malaika wanaotulinda wao hawaingii humo kwa hiyo tunakua hatuna ulinzi, kinachosaidia ni dua "Ewe Mola wangu najilinda kwako kutokana na majini wakorofi wakike na wakiume" dua hii inawadhoofisha, kutanguliza mguu wa kushoto ni sunna, ukifanya hivyo majini wanakupuuza wanahisi na wewe ni wale wale tu.. siunajua hao hawajuani ni kama FBI na CIA..!!!!!!
 
kila kitu kitokeacho mkuu kinamaana yake na sababu yake mkuu.
vijana wa kleo kuna mambo mengi sana tunayapuuza na kuyazarau na huwa hatufuatilii kumbe ni ya msingi sana.
tunaangamia mkuu kwa kukosa maarifa.

ila sishangai koz wazee wanaishia chalinze
nilikuwa namsubiri mtu mwenye hoja kama hii.kuanguka chooni kuna uhusiano wa moja kwa moja na uchawi.ukianguka unakufa pona yako ni kupooza.kwa wenye kufaham elimu ya viumbe huwa ni jini anayetegwa chooni au bafuni kwa minajili maalum.yote kwa yote ni uchawi.
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Ni juzi tu nilikuwa najiuliza hili swali....OMG we really need your protection!
 
Hakuna mashetani wala Majini. Hio mi naona inakuwa ni Pressure kali inayoendana na paralysis. hata mtu akipatwa na kiharusi midomo hupinda na either mkono au mguu au vyote hupooza.
 
Bibie.Diana Fares Majin na Mashetani yapo na yametajwa pia katika Biblia hebu soma hapa

Majini na Shetani, ni nini tofauti yake?

Math. 16: 22-23.

MASKANI ZA MAJINI. (WANAMOISHI)

Ndugu yangu msomaji umuhimu wa elimu hii ni kubwa sana, kwani Mwenyezi mungu ametupa tahadhari sana kuhusiana na Shetani kiumbe wake. Kwani yeye Mwenyezi mungu ndiye alie muumba na yeye mwenyezi Mungu ndiye alietupa habari kujikinga naye huyo Shetani. hivyo basi ni vyema kutambua baadhi ya sehemu ambazo anakaa au anaishi shetani. Sehemu hizo nazitaja kama ifuatavyo:
MAJANGWANI- Ni sehemu ambayo hupenda sana kukaa Shetani au Jini, hivyo ni vyema kupita sehemu hiyo kwa dua (dhikri) maalum.
NYUMBA ZA BINADAMU- Pia hukaliwa na majini wa kishetani pia ni vizuri tukalifahamu hilo na kuishi maisha ambayo mwenyezi mungu anayaridhia.
MASHIMO YA TAKA TAKA- Ni moja katika sehemu za Shetani kukaa au kuishi, kwa hiyo ni muhimu sana kuchukua tahadhari.
MAPANGONI- Pia ni sehemu ya tahadhari kwani jini anaamini kwamba ni sehemu tulivu.
CHOONI- Ni sehemu ilio faragha pia ni sehemu ya hatari sana mara nyingi mtu akianguka chooni hupata madhara makubwa sana. hivyo ni vyema kuingia sehemu hii na dua maalum.
MITI MIKUBWA- Pia hupendelea kuishi au kukaa majini, miti hiyo ni kama vile mbuyu, msufi. N.K.
VISIMA- Hii ni sehemu ya muhimu sana kwa majini kukaa au kuishi katika maisha yao, pia ni muhimu sana kwa maisha ya binadam. Hivyo ni muhimu sana twende visimani tukiomba dua za ulinzi.
MITO- Pia ni sehemu muhimu sana kwa wanadamu alafu pia ni sehemu ambayo hupenda kuishi au kukaa majini. Hivyo ni muhimu kukumbuka dua wakati tupitapo au twendapo mtoni kwa shida ya muhimu.
MABWAWA- Ni sehemu ambayo hupenda sana kuishi au kukaa majini, tena na watoto wengi hupenda kuoga katika mabwawa. Kwa hiyo ni lazima tuyafahamu hayo.
BAHARINI AU MAZIWANI- Nayo ni sehemu ambayo wanaishi majini au mashetani. pia si sehemu ya kudharau, ni vizuri kulitambua hilo na kujikinga nalo kwa dua au maombi kutoka kwa Mwenyezi mungu.
MILIMANI- Ni sehemu muhimu kwa majini na hupenda sana kuishi au kukaa. Pia ni lazima kufata sheria zote ambazo kwa waislamu Mtume amefundisha pia kwa wakristo wanamaombi yao yakiwa kama kinga.
KATIKA MWILI WA BINADAMU- Shetani anaweza kuishi au kukaa katika mwili wa binadamu pasipo binadamu kugundua. Hii inatokea kama shetani huyo katumwa aje kwako na mtu fulani au kapenda mwenyewe kuingia katika mwili wako.
Ndugu yangu msomaji baada ya kutambua, kujua, kufahamu na kuelewa sehemu ambazo waishizo majini au mashetani basi ni lazima kuwa makini na kumuomba Mwenyezi Mungu atuepushie matatizo mbalimbali. Kila chenye kuumbwa huumbwa kwa makusudio ya mwenye kuumba na kila chenye kutengenezwa hutengenezwa kwa makusudio ya mwenye kutengeneza.

Mkuu Mwanahip Nipo tu vipi wewe hali ya maisha huko uliko?

Mkuu acha mawazo ya kishirikina. Nani aliyechora hizo picha? Mbona walioanguka hawajawahi simulia kuziona au kuona hayo mafudu?

Mimi mwenyewe nilipokua form 5 niliumwaga sana kwa mda mrefu, nilipoenda chooni, sikumbuki kilitokea nini, nilijikuta nipo sakafuni na ni mda mrefu ulipita, ila sikumbuki kuona hayo makitu.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: 1gb
'huku maisha ALHAMDULILLAH twashkuru kaka tuwazima mkuu wape DAA'WA wape DAA'WA wagalatia hao bora niseme wagalatia kuliko nikiwaita MAKAFIRI wanachukia kama nini aisee,wape DAA'WA kiongozi wangu...'
 
'huku maisha ALHAMDULILLAH twashkuru kaka tuwazima mkuu wape DAA'WA wape DAA'WA wagalatia hao bora niseme wagalatia kuliko nikiwaita MAKAFIRI wanachukia kama nini aisee,wape DAA'WA kiongozi wangu wafungue macho kuna mengi hawayajui hao jamaa aisee wafungue macho KA MKUBWA sisi tuko nyuma hapa tunaku-back up na kukupa ma-back vocal mkuu NO FEAR thats how we sapoz to be mkuu...'
 
Bibie charminglady Kuanguka kwa

chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka

chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao

wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza

upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea

umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya

unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi

(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa

kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi

(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi

wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

images

Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu.

thanks Dr
 
Je unamjua huyu ni JINI yupi na kama akikutokea utafanya nini???????????Mkuu.@LiverpoolFC

Hizi picha ni za kudanganyia watoto wasali kabla na baada ya kutoka chooni. Pia kuwasisitiza kutanguliza miguu.
Ni sawa ni ile ishu ya kuwafanya watoto waiheshimu qurani kwa kuwadanganya kuwa atakayeikojolea atageuka nyoka.
Ni sawa na kumwambia mtoto "tema mate nimpige".
 
duh kweli JF noma,mi sina cha kuchangia nakula pindi tu.Ila hizo kesi za watu kufa baada ya kuanguka bafuni/chooni hata mimi nazisikia sana,miaka mi3 iliyopita nilipokuwa nasoma UDOM kuna mwanachuo alifariki baada ya kuanguka bafuni

mkuu ni wawili pale udom, kama nnakumbuka ni kati ya 2009 na 10, na wote walikufa
 
Bibie charminglady Kuanguka kwa

chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka

chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao

wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza

upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea

umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya

unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi

(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa

kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi

(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi

wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.

images

Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu.

Jombaa ni jini au shetani,au hakuna tofauti?
 
Pia tunatakiwa..tukisha maliza haja ufanye utoke ..pia mambo ya kuimba chooni ni mabaya kabisa..kuna viumbe humo ndo makaazi yao..so unapomaliza toka..

mimi napenda haka kamchezo ka kuimba chooni haswa nikioga.
 
ukiona mtu kaanguka bafuni au chooni wahi umchane eneo lolote na wembe damu itoke kidogo, baada ya hapo mtoe kwa huduma ya kwanza.
 
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.

very easy uyo alipata stroke(kiharusi) kupinda kwa mdoma ni dalili mojawapo ya stroke.
matatizo yanayoongoza kusababisha stroke( kiharusi) ni shinikizo la damu(high blood pressure) na kisukari

kumbuka unaweza kuwa na shinikizo la damu au kisukari ata kwa zaidi ya miaka 10 bila kujijuia

stroke kwa kifupi ni damu kushindwa kusafiri vizuri kwenda kwenye eneo fulani(portion) la ubongo,hivyo basi eneo husika la ubongo kushindwa kufanya kazi

kuna stroke za aina mbili,1 inayosababisha damu kuvuja kwenye ubongo( hii ni hatari zaidi) 2 na isiyosababisha damu kuvuja kwenye ubongo
 
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.

1gb hii kitu hutokea sana kwa wagonjwa wenye matatizo ya shinikizo la damu (hypertension, watu husema Bp) na hata kisukari ambayo haikuwa ikijulikana. Dalili zao zaweza kuwa kupoteza fahamu, mdomo kupinda, na udhaifu wa upande mmoja wa mwili. Hii huitwa Kiharusi au Stroke, na mara nyingi ni aina ile ya kupasuka kwa mshipa wa damu kwenye ubongo.
Ni vizuri watu kuchunguza afya zao mara kwa mara, wasidhani ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari lazima uwe na dalili. Utashangaa mtu yuko safi kabisa, lakini ukimpima pressure iko zaidi ya 200/110mmHg, au sukari yake masaa nane baafa ya kula imezidi 7.0mmmol/l. Hizo values ni kubwa sana.
Kufia bafuni chanzo si mapepo, bali ni magonjwa sugu ambayo hayakugundulika na kupata tiba.
 
Last edited by a moderator:
mi nimeshaanguka mara nyingi sana lakini ...........
 
Ndugu yangu Mzizi Mkavu nafuatilia Vzur sana lecture yako na nakuelewa vzur saana.., ila nna swali kdogo; Je hzo picture ulzo ambatansha n Kweli n za Mashetan? If yes, zmepgwa kutoka wap ikiwa Mashetan hayaonekan dhahir kwa macho au techologia gan ime2mika ndugu?
 
Back
Top Bottom