Kuanzia IGP Harun Mahundi aondoke Polisi imekuwa mafia

Kuanzia IGP Harun Mahundi aondoke Polisi imekuwa mafia

Polisi wetu mishahara ni midogo...
Wana maisha magumu...

Kuna mtu pale Moshi miaka kama minne nyuma aliona usiku jirani na kwake fuso inashusha mzigo wa mafuta ya kula na wines nyingi kutoka nje ya nchi..
Akajidai kutoa taarifa polisi kwamba anawasiwasi na mali za wizi..

Polisi wakaja.. kumbe ni magendo.. Mhusika akachukuliwa... Kumbe ni mtu wa kuforce rushwa... polisi walimwachia akaendelea na biashara zake...

Baada ya wiki yule alietoa taarifa alifuatwa na Mhusika akaambiwa atamfanyia mpango apasuliwe paji la uso na shaba... Mtoa taarifa aliomba msamaha na kulia kama mtoto...
Akaambiwa nimepoteza kama million 4 kwa upuuuzi wako... Sasa ikabidi jamaa awe anamlipa kidogo kidogo kwa miezi mitano..

Sasa angalia mtoa taarifa akageukwa kwa sababu ya rushwa... Polisi wana shida sana na rushwa kwa kuwa mishahara midogo...
 
HasbunAllah wa niima l'wakil.

AlhamduliLlah Gozi linadunda kama kawa. Allah ampe unri mrefu

Mahasidi mshindwe.
Sasa siubadilishe ladha. Wewe unajisikia tu vizuri wote wanne kushare kitu cha gozi. Halafu wewe ndo bi mkubwa unaipata kwa nadra.
 
Mimi ni mtoto wa Polisi na mzee wangu alikuwa mkubwa sana kwa miaka mingi kwenye jeshi hili. Kuanzia IGP harun mahundi aondoke 1996 Polisi imegeuzwa genge la wahuni na mafia.

IGP Mahita ndiye aliye anzisha genge la umafia Polisi na viongozi wa serikali wamekuwa wakifumbia macho makusudi kwasababu genge hili limekuwa likitumia kuwasaidia kisiasa na kuwazuia wapinzani na kuiba kura.

1. Kwanza walianzisha mifuko ambayo haipo kisheria ambayo inakata makato kwa kila polisi mfano kuna mfuko wa kufa na kuzikana ambao Polisi wa chini hawaruhusiwi kuhoji pesa inatumikaje na wala hawapati chcochote! hata wakifiwa

2. Kikosi cha ulinzi maalamu kama wa banks na sehemu nyeti kampuni zinalipa Polisi lakini sio serikali wala Polisi wengine wanajua pesa inaenda wapi.

3. Rushwa barabarani kila RPC anapata chake kutoka kwa mkuu wa traffic wa mkoa na kati ya hizo kuna fungu linaenda kwa wakubwa makao makuu na hakuna mtu wa kuhoji

4. Kuna pesa inategemea kuletwa ya rushwa kutoka kwa RPC wa mikoa ya mpakani. Hii ruhswa na kuingiza na kutoa magendo bila kodi. RPC asipo tuma pesa anahamishwa haraka sana. Mikoa kama Kagera, Mwanza, Mara, Tanga, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha wanahusika na hili. Yaani ilifika wakati RPC akipandishwa cheo na kupekwa makao makuu Dar anachukia kama kapata msiba kwasababu hakuna rushwa makao makuu kama mikoani.

IGP mwema alijaribu kusafisha lakini hajafanikiwa kwasababu mitandao ilikuwa imeota mizizi sana na utamaduni wa rushwa umekuwa mkubwa sana kwa muda mrefu. Bado kuna wizi mkubwa kwa Polisi wa railways, vitengo vya magari na spair parts.

Polisi ni lazima ivunjwe na kuundwa upya na Polisi wa chini wawe na uhusu wa kusema maovu bila kuogopa mabosi wao. Lakini kuwe na uangalizi maalumu kama Bodi ambayo iwe na wanasheria na ofisi ya mkaguzi mkuu na iruhusiwe nkohoji Polisi wa kawaidia bila vipingamizi kwa wakati wowote.

Yaani Sirro nyumba yake ya Musoma ilikuwa inasimamiwa na maafisa wa Polisi kwenye ujenzi wakati ni nyumba binafsi. Lakini imejegwa na wadhamini. Tbaigana alijengewa mpaka Hoteli na wadhamini waziwazi. Hawa wadhamini ni watoa rushwa na wenye magendo

Hakuna kitengo wafanyakazi wanafanya kazi kwa shida kama Polisi wa chini. Lakini hakuna kitengo wakubwa wanaishi vizuri kama Polisi Mahita alikuwa na helikopta yake kabisa ya kumpeleka Morogoro kwao weekend

Naomba niongezee kitu kingine: kuna magari yanashikwa na Polisi ya wizi au wauza madawa yanataifishwa. Je umewahi kusikia mnada wa magari ya Polisi. Nakumbuka wakati mzee wangu akiwa RPC zamani tulishangaa tumeletewa Toyota 4 runner tukaambiwa ni magari ya wizi ya mnada na mzee kalipa laki moja tu kwa gari mpya .
Halafu RCO naye alipewa gari zuri yaani ulikuwa ni utamaduni na hakuna wa kuuliza wala kuhoji


Hakuna kiongozi amesaidia Polisi huko nyuma kama Mahundi ambaye alikuwa nasifika kwa kuwa na akili sana

Kikwete+mahundi.jpg
View attachment 2575252

Mwanzilishi wa mafia ya polisi

View attachment 2575253
1.JPG
Kamundu heshima kubwa kwako kwa hili na barikiwa sana lakini ili reform ya kweli iweze kufanyika inabidi CCM itoke madarakani
Kwasasa polisi iliyopo na CCM ni sawa chupi na kalio
 
Hukumsikia Mama Samia juzi? Alisema sakata la over invoicing ya ndege limeanzia hapo hapo.

Polisi kuna ufisadi zaidi ya rushwa ni organised crime.

Ukishtaki utatakiwa uhonge, ukishtakiwa utatakiwa uhonge. Ni "damned if you do damned if you don't".


Ooh hiyo hatari sana kama hata hapo Ikulu nako kuna mambo hayo na tutakuja kujuta kama wasipochukua hatua
 
Ni vituko hii nchi eti kamanda wa TAKUKURU wa mkoa ana mshahara wa Milioni 3.8 halafu, meneja wa TRA wa mkoa ana mshahara wa zaidi ya 9M halafu huyu wa TAKUKURU ndio aende kumkamata meneja wa TRA.

Mshahara wa mkuu wa takukuru wa mkoa ni mshahara wa kufikia kwa maafisa wa chini kabisa wa TRA, TANESCO na mashirika mengine makubwa ambayo tunalalamikia yamejaa rushwa halafu anaesimamia rushwa ana mshahara mdogo, hiyo rushwa ataisimamiaje huku ana njaa.

Takukuru iko kama geresha tu, hatuko serious kwenye kupambana na rushwa ndio maana kesi nyingi za takukuru ni za watendaji wa vijiji, hakimu wa mahakama za mwanzo, nk.

Takukuru waelekeze nguvu zao kwenye rushwa kubwakubwa kama embezzlement waachane na matrafiki ufisadi ndio unafanya tusiendelee sio hizo elfu mbilimbili za matrafiki
 
Ni kweli kabisa! Moja ya maeneo nyeti ukitaka kuvuruga taasisi yeyote ni kwenye recruitment process!

JWTZ kwa miongo mingi wako very serious kwenye recruitment na mafunzo. Anatoka askari aliyenyooka. Kozi za maafisa zimeshiba sio afisa anapelekeshwa na wanasiasa kama vile hajui mipaka yake.



Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app

..hata jeshini nako Magufuli alichafua.

..umesahau alipochanganya matukio ya kutoa kamisheni kwa maofisa kadet wa Jwtz na vituko vya wapinzani kuunga mkono juhudi?

..pia alivyokuwa akifanya mbwembwe zake za kisiasa huku amevalia combat za jeshi la wananchi?

..au maafisa wa Jwtz walioteuliwa ukuu wa mkoa au wilaya lakini wakawa wanatekeleza majukumu ya kiserikali na ya Ccm wakiwa ktk uniform na vyeo vyao vya kijeshi?

..pia kuna Jwtz aliyeteuliwa ktk Ccm ambaye alikuwa anatamba kwamba alipokuwa Mkuu wa Kikosi alitumia nafasi yake kutoa mafuta kwa magari ya kampeni za Ccm!!

..Kwa kifupi tuna matatizo makubwa sana nchi hii.
 
Nasikia Mahita alikua German steel yani chuma cha pua roho mbov ubaya ubaya tu
Umenikumbusha jamaa mmoja wa kuitwa Lu fruit....
Moja ya binadamu Wasio na huruma kuwai kutokea....
Ila jamaa Kwa mkewe ndipo utaona meno na very humble Kwa mkewe....

Kuna binadamu wana roho ngumu husamehewi huonewi huruma....
 
Nadhani ushauri wa msingi ndio uwe unatolewa kama hivi.Hata Wakubwa wakisoma wanajifunza kitu.
Polisi mliopo humu naimani mnaona yanayojadiliwa.Fanyeni kazi Kwa weledi na Mungu atawabariki,Haki ndio iwe msingi wenu....Sasa kama nyie Polisi mnakuwa sio kimbilio letu sie wananchi tutakimbilia wapi🤭
 
Hii ni mbaya sana, polisi ndio wanatakiwa kuwa watu wa kutazamwa kama mfano katika jamii.
Ndugu yangu mmoja amekuwa mtu wa mwisho kwenye ukoo wetu kutumikia TanPol baada ya "kuokoka" kwa kupata nafasi ya kusoma MBA na kuchomoka kabisa upolisi .

Anasema kama unamjua Mungu kweli na kulishika neno na mafundisho yake,huwezi kufanya kazi TanPol.
 
Wewe ni mtoto wa Mahundi?

Ila ni kweli Jeshi la polisi limeoza Sana
Hapana mimi sio mtoto wa mahundi lakini nafahamiana na mtoto wake John. Mimi pia nimenufaika kama mtoto wa kigogo kwenye hili huo ndiyo ukweli. Nakumbuka nilivyokuwa mdogo dereva wetu aliumwa kwenda kwake masikini alikuwa anakaa kwenye kibanda kama hema cha bati!. wakati sisi tulikuwa na magari matatu ya serikali ya kutumia na tunakaa uzunguni!. Nasema kwa manufaa ya umma na nchi.
 
Back
Top Bottom