Kuanzia IGP Harun Mahundi aondoke Polisi imekuwa mafia

Polisi wetu mishahara ni midogo...
Wana maisha magumu...

Kuna mtu pale Moshi miaka kama minne nyuma aliona usiku jirani na kwake fuso inashusha mzigo wa mafuta ya kula na wines nyingi kutoka nje ya nchi..
Akajidai kutoa taarifa polisi kwamba anawasiwasi na mali za wizi..

Polisi wakaja.. kumbe ni magendo.. Mhusika akachukuliwa... Kumbe ni mtu wa kuforce rushwa... polisi walimwachia akaendelea na biashara zake...

Baada ya wiki yule alietoa taarifa alifuatwa na Mhusika akaambiwa atamfanyia mpango apasuliwe paji la uso na shaba... Mtoa taarifa aliomba msamaha na kulia kama mtoto...
Akaambiwa nimepoteza kama million 4 kwa upuuuzi wako... Sasa ikabidi jamaa awe anamlipa kidogo kidogo kwa miezi mitano..

Sasa angalia mtoa taarifa akageukwa kwa sababu ya rushwa... Polisi wana shida sana na rushwa kwa kuwa mishahara midogo...
 
HasbunAllah wa niima l'wakil.

AlhamduliLlah Gozi linadunda kama kawa. Allah ampe unri mrefu

Mahasidi mshindwe.
Sasa siubadilishe ladha. Wewe unajisikia tu vizuri wote wanne kushare kitu cha gozi. Halafu wewe ndo bi mkubwa unaipata kwa nadra.
 
Kamundu heshima kubwa kwako kwa hili na barikiwa sana lakini ili reform ya kweli iweze kufanyika inabidi CCM itoke madarakani
Kwasasa polisi iliyopo na CCM ni sawa chupi na kalio
 
Hukumsikia Mama Samia juzi? Alisema sakata la over invoicing ya ndege limeanzia hapo hapo.

Polisi kuna ufisadi zaidi ya rushwa ni organised crime.

Ukishtaki utatakiwa uhonge, ukishtakiwa utatakiwa uhonge. Ni "damned if you do damned if you don't".


Ooh hiyo hatari sana kama hata hapo Ikulu nako kuna mambo hayo na tutakuja kujuta kama wasipochukua hatua
 

Takukuru waelekeze nguvu zao kwenye rushwa kubwakubwa kama embezzlement waachane na matrafiki ufisadi ndio unafanya tusiendelee sio hizo elfu mbilimbili za matrafiki
 

..hata jeshini nako Magufuli alichafua.

..umesahau alipochanganya matukio ya kutoa kamisheni kwa maofisa kadet wa Jwtz na vituko vya wapinzani kuunga mkono juhudi?

..pia alivyokuwa akifanya mbwembwe zake za kisiasa huku amevalia combat za jeshi la wananchi?

..au maafisa wa Jwtz walioteuliwa ukuu wa mkoa au wilaya lakini wakawa wanatekeleza majukumu ya kiserikali na ya Ccm wakiwa ktk uniform na vyeo vyao vya kijeshi?

..pia kuna Jwtz aliyeteuliwa ktk Ccm ambaye alikuwa anatamba kwamba alipokuwa Mkuu wa Kikosi alitumia nafasi yake kutoa mafuta kwa magari ya kampeni za Ccm!!

..Kwa kifupi tuna matatizo makubwa sana nchi hii.
 
Nasikia Mahita alikua German steel yani chuma cha pua roho mbov ubaya ubaya tu
Umenikumbusha jamaa mmoja wa kuitwa Lu fruit....
Moja ya binadamu Wasio na huruma kuwai kutokea....
Ila jamaa Kwa mkewe ndipo utaona meno na very humble Kwa mkewe....

Kuna binadamu wana roho ngumu husamehewi huonewi huruma....
 
Nadhani ushauri wa msingi ndio uwe unatolewa kama hivi.Hata Wakubwa wakisoma wanajifunza kitu.
Polisi mliopo humu naimani mnaona yanayojadiliwa.Fanyeni kazi Kwa weledi na Mungu atawabariki,Haki ndio iwe msingi wenu....Sasa kama nyie Polisi mnakuwa sio kimbilio letu sie wananchi tutakimbilia wapi🤭
 
Hii ni mbaya sana, polisi ndio wanatakiwa kuwa watu wa kutazamwa kama mfano katika jamii.
 
Wewe ni mtoto wa Mahundi?

Ila ni kweli Jeshi la polisi limeoza Sana
Hapana mimi sio mtoto wa mahundi lakini nafahamiana na mtoto wake John. Mimi pia nimenufaika kama mtoto wa kigogo kwenye hili huo ndiyo ukweli. Nakumbuka nilivyokuwa mdogo dereva wetu aliumwa kwenda kwake masikini alikuwa anakaa kwenye kibanda kama hema cha bati!. wakati sisi tulikuwa na magari matatu ya serikali ya kutumia na tunakaa uzunguni!. Nasema kwa manufaa ya umma na nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…