Kuanzia Julai 1, 2021 rasmi CHADEMA wanarejea kwenye ukorofi

Jikite kwenye hoja kamanda
Hadi hapa usalama upo kwa wengi,ikiwa ni kwa hata fisi wakijani, achilia mbali kitoweo cha fisi, au nyumbu hakuna kutekana, hakuna kubambikiana kesi, hakunawasiojulikana na vile vile mnanuna kwa mageuzi kabambe yanayofanywa, na bado mengi yaja.
 
Tupo hapa JF kuweka kumbukumbu
Mbona chadema inakuwasha Sana? Chadema bungeni hawapo lkn bado akina ndugai na kibajaj hawalali usingizi...wenzako ambao walijaribu kuisumbua chadema wameishia kuanguka kisiasa
 
Reactions: nao
Kamanda acha udikteta
 
Mama anacheka na Nyani Wakati ana shamba la Mahindi. Nikikumbuka siasa za 2012-2015, naisikitikia nchi yangu, nawasikitikia zaidi boda boda kwa sababu, kwenye maandamano yoyote wao ndio hutangulizwa mbele. Anyway, kazi iendelee# This is the era of survival for the fittest.
 
Big up
 
Hivi Polepole na Bashiru wameenda Kigoma? Siku zinakimbia sana.
Waende kufanya nini wakati wazandiki waliwaengua kwa mbwembwe za kusuka upya kikosi cha siasa uchwara?

Kwanini CDM hamjashiriki uchaguzi Buhigwe na Muhambwe?
 

Ungemalizia kwa kusema "asema nabii Tito" ungeeleweka vizuri zaidi.

Ila wewe kama si nabii huyo si mbaya ukiyajua haya bayana:

Hadi sasa mama kama binadamu anakwenda vizuri. Akiendelea hivyo ataendelea kuungwa mkono zaidi na zaidi.

Tusitegemee mama kuzinguliwa na waungwana unaowalenga kama ataendelea kusimamia haki, uhuru na zaidi sana asiposahau kutoa mrejesho na kuchukua hatua stahiki kwenye:

1. Ripoti za CAG zikiwamo za TPA na BOT Mar 2021.
2. Ripoti ya tume ya wataalamu kuhusiana na Corona.
3. Lile kundi dhwalimu lililotaka kumzimia yeye urais.

Akitufikisha kwenye hatima ya mzizi wote wa fitina yaani kupatikana kwa katiba muafaka mbona mama atastahili mitano tena baada ya 2025 ya heshima na taadhima.

Eeh mola wetu hebu ukamjalie hekima na busara rais wetu aendelee kuyaumbua manyang'au haya yasiyomtakia mema.
 
Malengo makubwa ya viongozi wa kile chama ni ruzuku tu, hawana mpango wa kuingia ikulu. Ila bahati mbaya wanachama na wapenzi wa kile chama wanahadaiwa.. hawajui walifanyalo. wanashangilia makonda akifukuzwa, Sabaya akishughulikiwa nk

Wanapenda kuona matatizo tu, ukijenga reli unatukanwa, ukijenga hospitali unatukanwa, ukijenga barabara utapondwa. Wanapenda kusikia mambo ya chuki, kufa, kufukuzwa kazi nk. Ni watu wa ajabu sana...
Kutwa wanajadili ya jirani wao hawana ofisi hata moja waliyoijenga, hawana mradi wowote wa maendeleo, pesa za ruzuku na makato ya wabunge ni mwenyekiti na mtu wa fedha ndio wanajua. Wapo kama nyumbu.. mmoja akianza wote wanafuata. Kwa mtindo huu CCM itatawala milele.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Duh tusubiri
 
Kamanda umejiunga lini Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…