Nchi HAIENDI bila ya makusanyo ya KODI/TOZO.....
Tubadilishe "mentalities" kwa KUJIFUNZA HULKA MPYA ya KULIJENGA taifa letu kwa gharama ya jasho letu......
Hizo TOZO zinakwenda katika mfuko MAALUM.....CAG atakuwa anaukagua na TAARIFA TUTAPEWA.....
#KaziIendelee
#NchiKwanza
Hauko siriasi mkuu, mfuko maalum? CAG? Ndio nini akikagua? Itatokea nini? Miaka 60 kodi zinalipwa na hakuna kinachotokea, ndo ije kuwa tozo za miamala? Kama kweli mnajali na mna huo uzalendo, ya nini kulibebesha taifa gharama za kijinga kwa fahari ya wasio fanya kazi?
Kipi kimewahi kuboreshwa/kuzuiwa na bungwe kisitokee kwa maslahi mapana ya nchi? Kama hakuna, nini tija ya kuwa na wabunge wengi wenye kulipwa mamilioni yasiyokatwa kodi, na viinua mgongo vya kufuru kila miaka 5 plus magari mazito mazito kila baada ya miaka 5?
Kwanini tusitumie gari za cc ndogo tu, mathalani 2000cc kwa mawizara na taasisi zote za umma kupunguza initial, operation na maintenance cost, nchi imefunguliwa kwa lami tayari, sehemu korofi tumia cruiser mkonge, ONDOA depreciation factor ya miaka 5, nenda na gari hata miaka 15, si tunanunua zero km na kulitunza? Nimeona gari la shirika flani likianza na km 9 mpaka 600,000 na bado liko barabarani.
Ondoa posho zisizo na maana serikalini zisizokatwa kodi, fanya consolidation ya mishahara, piga PAYE kama wanavyofanyiwa private sector, sio unamlipa mshahara sh 445,000 ambayo inakuwa taxed halafu unampa posho za sh 1,500,000 tax free. Mpe mshahara wa sh 1,945,000 kisha piga tax yote.
Ongeza uzalishaji, sio kunyang'anya masikini ili ukawarundikie wakina Ndugai!
Achana na ruzuku za vyama, wapambanie gharama za kujiendesha wenyewe ili watumie akili kuzalisha kisha waongee yaliyo kweli, sio tuandamane kisha wao wako London na familia zao.