Kuanzia Jumatatu, menu za simBanking zitaanza kutozwa

Kuanzia Jumatatu, menu za simBanking zitaanza kutozwa

leo nimeamka na hii
Ndugu Mteja, kuanzia 26 Julai 2021 kila uingiapo kwenye menyu yoyote ya Bank utatozwa Tsh100 kwenye salio lako la muda wa maongezi. Kwa taarifa zaidi piga 100

kazi iendeleeee
Hela zenyewe mnazo ndogo ndogo namna hiyo mnahangaika na ma benki ya nini, waachieni wenye mapesa mengi, weka pesa zako sehem ukihitaji ndogo ndogo unachukua bila makato na bila ya kukatwa ukitaka kujua zimebaki sh ngap hukatwi hata senti. mnafanya maisha kuwa magumu sana halaf mnabaki kuilamu serikali mnacho kifanya ni kuwanufaisha wana siasa kuziiba na kuzila tu. kilipwa benki chomoa zote watakazo kuwa wamezikata kwenye kuchomoa zote zinawatosha baada ya hapo kimya.
 
Mambo ni Faya!!!! SGR,STEGOLAZ zinahitaji kukamilika......Kuna huduma nyingine kuna option ya kuzipiga chini.
Na contact yeyeto ukiipiga chini ni lazima uwalipe hapo ndipo mtihani ulipo pesa Hakuna, hatukopesheki,tuliyokopa riba juu, wananchi awazalishi sababu hawana mazingira ya kuweza kubadili fursa tele kuwa pesa.Miradi mingi ilianzishwa kwa sifa ya kuwakonga watangulizi wake ikiwa sio lazima au ya haraka Sana
 
Hutaweza ku-acesss huduma
Hauta-access huduma kivipi, wakati ukiuliza tu hata kama hauna salio lazima ujibiwe!

Usichoelewa ni kwamba, jibu lolote unalopewa pindi uulizapo, hulipiwa, bila kujali una salio ama hauna.

Kama hauna chochote kwenye account, uingiapo muamala wowote mpya, wao hufyeka gharama ya huduma huduma hiyo waliyokupatia.

Jaribu kuchunguza utaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hauta-access huduma kivipi, wakati ukiuliza tu hata kama hauna salio lazima ujibiwe!

Usichoelewa ni kwamba, jibu lolote unalopewa pindi uulizapo, hulipiwa, bila kujali una salio ama hauna.

Kama hauna chochote kwenye account, uingiapo muamala wowote mpya, wao hufyeka gharama ya huduma huduma hiyo waliyokupatia.

Jaribu kuchunguza utaona.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo sawa ,hapo sawa wamefanya vyema ,kama hauna salio wanakupa huduma ,ukiingiza wanailamba hapo sio mbaya.
 
Mbona kama hayo makato yalishaanza muda? CRDB BankingSimu wanakata kama sikosei kwa Tigo ni 400/-
 
Nimeliona hilo leo. Hatuna budi kurudi kwenye foleni za benki. Nilihamisha fedha Tsh 200,000 toka benki kwenda Mtandao nilikatwa sh. 7,000. Toka mtandao kwenda kwa Wakala na tena kutoa ilighalimu sh 8,000. Makato jumla 15,000.
 
Mbaya zaidi hii kodi ya makato ya uzalendo kikifika kipindi cha uchaguzi haohao ccm wanatumia ndio sera yao kuwa wamejenga iyo miladi na barabara utadhani ni hela yao kumbe kodi zetu ambazo wapinzani nao wamechangia kukatwa kwao
 
Viongozi wako sahihi kabisa wala sio wapumbavu wako sahihi asilimia mia
WAPUMBAVU NI WANANCHI WENYEWE
 
No country can escape from poverty by excessive taxation.
Sasa hapa kwetu
Wizara ya fedha...Madelu
Wizara ya afya...Dada Doro
Wizara ya elimu...Dada Joy
Wizara ya nishati....Kalemani
Wizara ya Sheria...Kalamaganda
Hao wote eti Wana PhD Kama Mwakyembe ispokua doro
I rest my case
 
Wewe upo voda? Kwa maana ya kufanya kazi? Mimi nina number zaidi ya moja miaka 20 sasa nilihama voda kwenda airtel ikiwa ni hiyo sababu na hadi sasa nina voda hata iwe na 400 bal..ance ambayo haiko kwenye bundle haikubali kupiga code ya crdb sim banking
Jamaa ameongea ukweli, hicho kiwango cha 500 ni uongo.
 
leo nimeamka na hii

Ndugu Mteja, kuanzia 26 Julai 2021 kila uingiapo kwenye menyu yoyote ya Bank utatozwa Tsh100 kwenye salio lako la muda wa maongezi. Kwa taarifa zaidi piga 100

kazi iendeleeee
jamani naomba meejesho menu zenu vp
 
Back
Top Bottom