Kuanzia leo naacha pombe na namrudia Mungu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Hello Jamiiforums

Kichwa cha habari kinajitosheleza, wadau na wanywaji wa pombe wote najua tumekuwa tukikutana sehemu tofauti tofauti ili kupoza mioyo (kumwagilia moyo) huku tukiipa miili yetu pole kwa kujipongeza kama ushindi kwenye mishe zetu.

Kinywaji hiki maarufu Duniani chenye shepu na ladha tofautitofauti huku kikiwa na ushawishi wa kipekee, natangaza kuacha rasmi na kuianza ibada.

Kwasababu kwa takiribani miaka 24 nakunywa pombe na sijaona faida zake. Kwa wale wote niliowakosea pindi natumia pombe nawaomba mnisamehe.

Natangaza msimamo huu Leo 27/7/2024 huku nikimuomba Mungu aniongoze katika njia sahihi.

Salaam Jamiiforums
 
Vipi na jina utabadilisha au..?
 
Bado umelewa subiria pombe iishe kichwani , leo ni tarehe 27 sio 28, Hongera Kwa kumkumbuka MUNGU MUUMBA MBINGU NA NCHI.
 
Unaacha pombe au unaacha ulevi
 
Jana ilikuwa anniversary ya ndoa yangu. Nimetimiza miezi nane . Sikujua hata kama ni hiyo siku ila niliamka na furaha sana . Nikaenda mahali kukaa tu asubuhi saa moja . Vitu vilishuka paka saa 11 kuelekea jioni. Mfukoni nilikuwa na laki 3. Nimerudi home jioni nampa wife 100k. Nilienjoy na wadau , nilitoa mawazo. Nimeapa sana naiacha ila kuna sehemu nayo pombe ina refresh na pia napata connection nyingi sana kupitia ULABU. Pia nawaomba msamaha wale wote nimewakosea. CCM OYEEEEEE MAMA SAMIA MITANO TENA
 
Kila kitu ukiamua kuacha inawezkana.

Hongera mkuu kwa kuamua kuachana na pombe. Lakini pia,ili uwe salama zaidi,achana na kampani za washikaji wanaopiga mtungi.

"Every thing you do,be it god or bad,there is price you must pay".. Kuna marafiki utawapoteza katika safari ya kutafuta uhuru mpya.
 
Hata mimi naacha sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…