Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ifikapo tarehe 1/11/2021 bodaboda na bajaji zote marufuku kuingia mjini na wale waliokua mjini watoke wote isipokua bajaji za walemavu.

Agizo hilo limetolewa na Abdi Issango, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dms.

#PbOnSaturday
 
... another great move! Tunaomba watoe tafsiri ya "mjini" ili kuondoa utata. Kwa mfano, kuna vibajaj vinapiga routes za Mbezi hadi Manzese hizi zinakuwa zimeingia mjini?

Badala ya "mjini" wangeainisha ni barabara zipi ambazo bajaji na bodaboda hazitakiwi kabisa kuonekana. Kwa mfano, Nyerere Rd. moja ya barabara muhimu nchini ndio inayoongoza kwa bodaboda; zinakera sana!
 
Safi sanaaaaaaaa! Nimeipenda hii move. Na Sasa hivi vibanda vya ajabu kando ya barabara hakuna tena.

Ngoja 2025 ifike tuone kama hawajabadili maamuzi.
 
Hahahahaha nasema hivi hatutoki n'goo hata wafanye nn watapga wataua kudadekiiii
Kusema tuu hamtoki haisaidii, onyesheni kwamba hamtoki kwa kufungua kesi mahakamani kwa sababu kwa ninavyojua nchi hii hakuna sheria ya kuzuia mtanzania asitembelee mjini akiwa na pikipiki au bajaj. Hiki kinachodanyika ni uonevu tuu unaofanywa kupitia matamko ya hovyo hovyo.
 
Sio kila wakati kutaka kuonyesha ubabe wa bila kutumia akili

Huwezi kufukuza tu wakati wanajua fika hao wanahitajika sana kwa mishe mishe za haraka
Wapo mpaka wanaobeba parcels au documents za muhimu

Bora kuwa na mpaka wa marufuku kuingia na anaeingia nakazia yaani chombo chochote cha moto kilipe hela kama congestion charge na Camera zifungwe na kurekodi kila anaeingia na analipa kwa muda maalumu

Anakuwa analipia kwa masaa 24 kiasi fulani hapo wengi wataondoka wenyewe au hata watalipia serikali itakusanya fedha za kuendeleza miradi ya jiji

Duniani nchi zilizoendelea wanapambana na uchafuzi wa hewa kwa hiyo wamejiongeza na nyie mjiongeze sio kuwafukuza

Kwa sasa mataifa makubwa wanajuandaa kuyaondoa magari ya mafuta yote na wameweka malengo na ili watu wanunue magari ya kisasa zaidi

Watu hawafukuzwi bali gharama zimekuwa nyingi na bei ya mafuta imepanda zaidi, kuingia mjini gharama mara mbili
Ila ndio hivyo

Ubunifu unatakiwa sio kufukuza tu
 
Hizi Sheria huwa zinapitishwa na taasisi/vikao gani?
Hakuna sheria kama hiyo, maana ingekuwepo ungesikia zamani kabisa hizo marufuku, haya ni matangazo tuu kama lile tangazo la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom