Kuanzisha biashara ni jambo gumu sana kuliko kutafuta ajira

Unaleta usomi mwingi na analysis kibao nenda kusini kanunue nazi na mihogo tafuta nafasi sokoni katika hiyo hela tumia chinni ya 5M huwezi kuona matokeo bila kuchukua hatua jinsi unavyousoma mchezo ndivyo unavyoamua kuongeza mtaji au kubaki na huohuo ukiendelea kuitafakari, usianze biashara kwa kuweka mtaji wote kwenye biashara moja.
 
njoo dm nikupe mchongo utanishukuru
 
Watu kama nyie nawaona wengi sana huku mtaan kwa mfano ananunua gari canter au fuso mwisho wa siku anafirisika sasa huwa najiuliza hizo mpaka ananunua gari alizipataje kwanin asiendeleze izo mishe zilizompatia izo ela na ndo kiwe chazo kikubwa cha kipato chake? Kwa mfano kama wewe hizo 40M umezipata kwa njia gani? Hii inamaanisha kwamba unachokifanya kinalipa bas kitanue ichoicho ? Au umeiba izo ela?
 
njoo na 20m nikuingize kwenye biashara ya magari used within 4 month's usipokuwa na 40m niite mbwa
 
Hahahah mtu kapiga mshindo wake akiwa ofisini. Katimuliwa kazi hajui cha kufanya na hio hela aliopigaga.
 
Madeni yanaua sana hii biashara, ila ukiwa na mtaji mkubwa/frem yako unaweza usiwe unakopesha kwa wateja wasioaminika ama lah unakua na standards zako za kumpa mtu bidhaa kwa mkopo.
Wanakopa mno mno ukiwaendekeza unafunga hata miezi 3 humalizi.
 
Naomba utufafanulie hapo kwenye kufanya kinyume na unachokijua
 
Amekuibia. Mahindi mwaka jana na mwaka huu yapo juu sana. Sasa hivi Sumbawanga gunia kwa mkulima ni 75k. December itakuwa 120-150k. Nenda mwenyewe huko Sumbawanga. Chukua nyumba weka store magunia yako. Kisha Rudi kutoa mrejesho December.
 
Business idea and plan inaanza kabla hujapata pesa ya mtaji.
That's right, fursa inakuja yenyewe automatically kichwani ikiwa associated na courageous toka moyoni na rohoni uwe na pesa au usiwe nazo, mtaji uwe mkubwa au mdogo,kwani ndizo zitakazokupa nguvu ya kutokukata tamaa pamoja na uvumilivu mnaita fighting spirit, kwasababu kutokukata tamaa pamoja na uvumilivu ndio msingi wa mfanyabiashara yoyote, kwani biashara zina ups and downs, ni courageous pekee ndio itamvusha.

Ukiona mtu anababaika au ana wasiwasi ipi ni biashara sahihi afanye ili atoke haraka,bora umwambie asifanye biashara tu kwasababu hatakuwa na maono ya hiyo biashara mbeleni, biashara itakufa kirahisi pindi akipata changamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…