Kubainishwa misimamo ya Iran kuhusu Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kubainishwa misimamo ya Iran kuhusu Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

jollyman91

Member
Joined
Sep 21, 2021
Posts
69
Reaction score
29
Katika miaka ya hivi karibuni Syria imekuwa ikikabiliwa na vita na harakati kubwa za makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani na sehemu ya ardhi ya nchi hiyo ikadhibitiwa na kukaliwa kwa mabavu na magaidi.
Hadi sasa vita hivyo vimesababisha maafa na mauaji ya makumi ya maelfu ya wananchi wa Syria na mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi hiyo. Utawala haramu wa Israel umeshadidisha mgogoro wa Syria kutokana na hatua zake za kufanya hujuma na mashambulio dhidi ya mamlaka ya kujitawala Syria. Wakati huo huo, kigugumizi cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria nacho kimekuwa na mchango katika kushadidi mgogoro huo na kuchukua muda muda mrefu.
Majid Takht Ravanchi, balozi na mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa sambamba na kubainisha misimamo ya Iran kuhusu Syria katika kikao cha Baraza la Usalama kuhusu matukio ya kisiasa na kiusalama ya nchi hiyo ya Kiarabu, amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo kuilazimisha Israel ili isitishe mara moja uvamizi na chokochoko zake dhidi ya mamlaka na umoja wa ardhi nzima ya Syria.
Ravanchi amesisitiza kuwa chokochoko za Israel dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ya umoja wa ardhi nzima ya Syria zinakiuka sheria za kimataifa na kwamba hatua za kiuhasama za utawala wa Kizayuni zinatishia amani na usalama wa eneo na uga wa kimataifa. Katika kikao hicho, mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ametilia mkazo pia ulazima wa kuendelea mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi huko Syria na kueleza kuwa vita dhidi ya makundi ya kigaidi havipasi kusitishwa kwa sababu hatua za uharibifu za makundi hayo ni tishio kwa usalama na umoja wa ardhi nzima ya Syria na pia kwa amani na usalama wa eneo hili.
4bvc974bb13b511pyhz_800C450.jpg
Rais Bashar al-Assad wa Syria

Hassan Beiki, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anasema: Hatua za upande mmoja za Magharibi katika eneo la Asia Magharibi limeufanya mgogoro wa Syria uzidi kuwa mkubwa na kuibadilisha nchi hiyo ya Kiarabu kuwa moja ya maeneo hatari ya harakati za makundi ya kigaidi.
Hatua ya kindumakuwili ya Marekani ya kulipatia misaada ya silaha kundi la kigaidi la Daesh na makundi mengine yanayopigania kujitenga na wakati huo huo kuunda muungano haramu nje ya maazimio ya Umoja wa Mataifa kimsingi hatua hizo za Washington zimeunga mkono mpango mchafu wa kuitumbukiza Syria katika lindi la vurugu, machafuko na vita. Himaya, misaada na uungaji mkono huo wa Marekani kwa makundi ya kigaidi lengo lake ni kudhoofisha mrengo wa muqawama. Utawala haramu wa Kizayuni nao umeendelea kufanya hujuma na mashambulio dhidi ya Syria kwa uratibu na mipango maalumu kwa ajili ya kuikalia kwa mabavu sehemu ya ardhi ya Syria. Hatua hizo kwa hakika zinatajwa na weledi wa mambo kuwa zimeufanya mgogoro wa kupandikizwa wa Syria uchukue wigo mpana zaidi. Moja ya malengo ya kimkakati katika kuendelea hujuma na mashambulio hayo na kuurefusha mgogoro wa Syria ni kubadilisha mazingira ya kisiasa, kisheria na kijiografia ya miinuko ya Golan ya Syria ambayo inakaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Majid Takht Ravanchi, balozi na mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amezitaja hujuma hizo kwamba, ni harakati za kupigania kujitenga nchini Syria na kusisitiza ulazimika wa kuhitimishwa chokochoko hizo.
4bsf10f1af0aa91dsnv_800C450.jpg
Miinuko ya Golan ya Syria

Sera za kimkakati za Iran katika mazingira haya ni kuunga mkono amani, uthabiti, umoja wa ardhi ya Syria na mamlaka ya kujitawala nchi hiyo. Filihali Syria inahitajia mno ukarabati na kuandaliwa mazingira ya kurejea wakimbizi nchini humo. Usama Danurah, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na mjumbe wa zamani wa timu ya Syria katika mazungumzo ya Geneva Uswisi anasema kuwa, Iran ikiwa moja ya wadau wakuu watatu wa mchakato wa mazungumzo ya Astana, ina nafasi na mchango muhimu katika masuala haya hususan katika vita dhidi ya ugaidi nchini Syria. Aidha Iran mbali na kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya ugaidi ikiwa na ushirikiano wa kimkakati na Russia, inaweza kuwa na nafasi muhimu pia ya mpatanishi ambayo inakubaliwa na pande zote.
Hivi sasa kufuatia juhudi za kieneo na kimataifa na kufuatiliwa makubaliano ya mwenendo wa mazungumao wa Astana, nchi ya Syria imevuka kile kipindi cha vita vigumu na mapigano makali na magaidi na hivi sasa imeingia katika hatua ya anga ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo kwa njia ya kisiasa, na kuandaa uwanja wa kurejea wakimbizi nchini humo. Pamoja na hayo, panahitajika himaya ya kweli ya Umoja wa Mataifa na ya mataifa yanayoitakia kheri Syria na yanayotaka amani na usalama virejee tena katika nchi hiyo ya Kiarabu. Hotuba ya Majid Takht Ravanchi, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa katika kikao cha Baraza la Usalama inatilia mkazo mtazamo huu.
 
Back
Top Bottom