Inaendelea..
Kubenea kupitia MWANAHALISI akawa mwiba mchungu kwa wanasiasa wengine.. Lakini siasa za Tanzania ni MTAFUTANO.. kuelekea mwishoni mwa 2007 EL akaundiwa kashfa ya RICHMOND na kufika February 2008 ikabidi ajiuzulu uwazirj mkuu... Alizidiwa kwenye mapambano
Kilichofuatia kinajulikana wazi.. Visasi na kutafutana.. EL alikuwa kajiuzulu lakini bado alikuwa na nguvu na connection pia.. MWANAHALISI lilizidi kuwa mwiba... Kilichofuatia 2008 kinajulikana wazi.. Kubenea alinusurika kifo na hata kuwa kipofu baada ya kuvamiwa ofisini kwake Mwananyamala na kujeruhiwa na kumwagiwa tindikali machoni
Sababu zilizokuja kutolewa baadae zinachekesha sana.. Nitaweka makala yake hapa
SK alipona na kuendelea na maisha..
EL hakukata tamaa bado alipania kuwa the next president... EL si mpinzani na hakuwahi kuwa mpinzani.. EL alikuwa na hasira na kisasi pande zote mbili UPINZANI NA kwenye chama chake CCM.. EL ni Mmasai asiyeamini kwenye kushindwa.. Aliipenda CCM lakini ikamtenda.. Hakuupenda UPINZANI kwanza ulishamsimanga kwenye list of shame.. Lakini sasa hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima chombo cha kutimiza ndoto zake..
Nguvu ya Dr Slaa CHADEMA ilichagizwa kwa kiasi kikubwa na EL na MWANAHALISI.. SK ni mkosoaji si mwanasiasa.. Connection za EL zilizidi kukatwa na hatimaye akaangukia CHADEMA na SK naye kumfuata huko.. SK baada tu ya kuingia kwenye siasa MWANAHALISI lilipoteza mvuto na umaarufu.. Mwishoni likafungiwa..
Yaliyotokea ni mengi baada ya hapo
Dr Slaa aliyemkaribisha EL CHADEMA alimkimbia.. Wanajuana vema wasingewezana hata kama CHADEMA ingeshinda
Ya Mwakyembe yalipita humohumo..
Kubenea kupitia CHADEMA akaingia rasmi kwenye siasa na kuwa mbungo kupitia jimbo jipya la Ubungo.. Huko kwenye siasa kapwaya.. Huyu si mwanasiasa ni mkosoaji tena wa kuletewa habari.. Hakuna vyanzo tena vya kumpa habari na mfadhili mkuu kaomba poo... Uandishi hauwezi kumlipa tena... Nyakati si rafiki sana.. Familia inahitaji kuishi bado na ni lazima maisha yaendelee
Je Kubenea yuko tayari kufumba macho na kula matapishi yake?
Je Kubenea yuko tayari kusamehe na kusahau ili akae na watesi wake waliomkosakosa kumdhulumu haki yake ya kuishi?
Je abaki CHADEMA iliyombeba na kumsitiri kipindi chote cha miaka mine au avae uso wa mbuzi na kuamua kuunga juhudi?
Wazaramo wanasema KUMKOMA NYANI JILADI... je Kubenea ataweza kufanya hivyo? Ni wazi yuko njiapanda kwakuwa pia ana hofu ya kuwekwa ghalani ama kupelekwa kwa jirani kwakuwa ni kama bohari kuu imejaa kama pishi la mchele... Imejaa WAUNGA JUHUDI BANDIA
View attachment 1407054View attachment 1407055
Jr[emoji769]