Kubenea awaonya wanaopiga ramli kuhusu hatima yake CHADEMA, azungumzia Virusi vya Corona

Kubenea awaonya wanaopiga ramli kuhusu hatima yake CHADEMA, azungumzia Virusi vya Corona

MHARIRI Mtendaji wa Gazeti la Mwana Halisi na Mseto, Said Kubenea, amevamiwa ofisini kwake na watu wenye silaha na kumwagiwa tindikali usoni na kusababisha apoteze uwezo wa kuona.


Na Muhibu Said


MHARIRI Mtendaji wa Gazeti la Mwana Halisi na Mseto, Said Kubenea, amevamiwa ofisini kwake na watu wenye silaha na kumwagiwa tindikali usoni na kusababisha apoteze uwezo wa kuona.


Katika tukio hilo, vile vile mshauri na Mhariri wa Habari wa magazeti hayo, Ndimara Tegambwage, alijeruhiwa na kushonwa nyuzi 15 kichwani baada ya watu hao kumkatakata kwa mapanga.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jamal Rwambow, ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza kwenda kumjulia hali Kubenea hospitalini juzi usiku, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Hadi jana mchana, Kubenea (37) ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa na kitu kizito karibu na jicho la kulia, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), huku taratibu za kumpeleka nchini India kwa matibabu zaidi zikiendelea kufanywa kutokana na hali yake kuwa mbaya.


Tukio hilo limetokea baada ya watu wasiojulikana kuchoma moto gari lake na kisha kumpigia simu na kumtumia ujumbe wa maandishi wa simu (sms) wakitishia kumuua.


Akisimulia mkasa wa kushambuliwa na kumwagiwa tindikali hospitalini hapo jana, Kubenea ambaye anaongea kwa tabu kutokana kuelemewa na maumivu, alisema wakiwa ofisini kwenye saa 3:00 za usiku wa kuamkia jana pamoja na Ndimara ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia masuala ya Kijamii la IDEA na vijana wake watatu, watu watatu walifika na gari na kugonga mlango.


Kubenea alisema baada ya mlango kugongwa, alikwenda na kuufungua ili kuwatambua wageni waliokuwa wakibisha hodi.


Alisema baada ya kufungua mlango, watu wale walimwambia kuwa ‘Tunakutaka wewe’ na baada ya kuwambia hivyo, wakamwamuru kukaa chini na kuanza kutoa mapanga, visu na nondo.


“Nilipotaka kufunga mlango, wakawahi kuingia ndani. Ndimara ambaye alikuwa anasafiri leo (jana) kwenda Darfur, Sudan, akawauliza kuna nini? Kuuliza hivyo, wakamvamia Ndimara na kuanza kumshambulia kwa mapanga,” alisema Kubenea.


Alisema hali hiyo ilizua mapambano makali ofisini kati yao na watu hao yaliyodumu kwa dakika kadhaa kabla ya watu hao kuzidiwa nguvu na kukimbia.


Kubenea alisema tukio la kumwagiwa tindikali lilikuja baada ya mmoja wa watu hao kuangusha chini panga alilokuwa akilitumia na yeye (Kubenea) kuliokota na kutaka kulitumia katika mapambano hayo.


“Baada ya mapambano kuchukua kama dakika mbili hivi, panga la mmoja wao likaanguka chini. Nikaliokota, nilipotaka kulitumia, ndio wakanimwagia tindikali,” alisema Kubenea.


Hata hivyo, alisema hakukata tamaa, badala yake, alijitahidi na kuingia kwenye moja ya vyumba vya ofisi hiyo kutafuta silaha kwa ajili ya kukabiliana na watu hao na kufanikiwa kupata chupa lakini aliporudi kwa ajili ya kuendelea na mapambano, alikuta watu hao wametoka nje ambako waliendelea kupambana na Ndimara.


Alisema baada ya kudhibitiwa na Ndimara huko nje, watu hao walijaribu kummwagia tindikali usoni, lakini haikumuathiri kwa vile alivaa miwani.


“Ndimara alinisaidia sana. Kwani kama ningekuwa peke yangu, wangeniua au kuniteka,” alisema Kubenea.


Kubenea alisema baada ya hali kutulia, walikodi teksi na kukimbizwa katika hospitali binafsi ya Dk Mvungi iliyoko Kinondoni ambako walipatiwa huduma ya kwanza kabla ya usiku huo kuhamishiwa Muhimbili.


Alisema madaktari wanaomtibu wameshauri akatibiwe haraka nchini India kutokana na kutojua aina ya tindikali iliyotumika kumdhuru.


“Madaktari wanasema ingekuwa ni tindikali ya kawaida, ingekuwa rahisi kwao kunitibu, lakini hii inaweza kuendelea kutafuna kwa muda mrefu na kuathiri macho kabisa. Hivyo, wameshauri kama upo uwezekano ni vizuri nikaenda India haraka, ikiwezekana kesho (leo),” alisema Kubenea ambaye anaona kwa tabu.


Alisema anaamini watu waliotekeleza tukio hilo, wametumwa kumshughulikia kutokana na waliowatuma kuchukizwa na msimamo wake wa kuweka hadharani maovu ya baadhi ya vigogo serikalini kupitia magazeti yake.


Kubenea alisema dhana hiyo inapewa nguvu kutokana na kuwa tangu Juni 13, mwaka jana, amekuwa akitumiwa sms za vitisho ambapo miezi miwili badaye watu wasiojulikana walichoma moto gari lake na kutamba kupitia sms kuwa wametimiza jambo hilo na kwamba kilichobaki ni kuuondoa uhai wake.


Alisema baada gari lake kuchomwa moto, aliendelea kupokea sms zinazomweleza kuwa:


“Kiburi chako kitakuponza, jiandae kwa shughuli nzito itakayokupata”, “Kifo chako kitakuwa cha aina yake, mzoga wako hautaonekana”, “Dawa ya kushughulikia maiti kama wewe imepatikana, jiandae”, “Maandalizi ya mauti yako yameiva, watangazie mabwana zako wanaokutuma. Unanuka uvundo wa kufa”, “Vuta pumzi zako za mwisho, hatuko mbali, yamebaki masaa machache kabla hatujakupeleka panapostahili”.


Alisema awali, alidhani watu wanaomtumia sms hizo ni waandishi wenzake wanamtania. Lakini kadri matukio ya kutisha yalivyozidi kutokea, akaamini kuwa watu hao ni maadui zake.


Mamia ya watu wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Halima Mdee, waliokwenda kumjulia hali Kubenea, jana asubuhi walifurika katika Wodi ya Sewahaji chumba namba 19 alikolazwa mwandishi huyo kabla ya kuhamishiwa katika chumba maalum hospitalini hapo.


Akizungumza hospitalini hapo jana, Duni alisema Kubenea amekuwa mhanga wa kusimamia ukweli na kuwashutumu waliomtishia kumuua kwa sms.


Kamanda Rwambow, alisema polisi wanaendelea na upelelezi na kwamba leo watatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukio hilo.
 
Inaendelea..
Kubenea kupitia MWANAHALISI akawa mwiba mchungu kwa wanasiasa wengine.. Lakini siasa za Tanzania ni MTAFUTANO.. kuelekea mwishoni mwa 2007 EL akaundiwa kashfa ya RICHMOND na kufika February 2008 ikabidi ajiuzulu uwazirj mkuu... Alizidiwa kwenye mapambano

Kilichofuatia kinajulikana wazi.. Visasi na kutafutana.. EL alikuwa kajiuzulu lakini bado alikuwa na nguvu na connection pia.. MWANAHALISI lilizidi kuwa mwiba... Kilichofuatia 2008 kinajulikana wazi.. Kubenea alinusurika kifo na hata kuwa kipofu baada ya kuvamiwa ofisini kwake Mwananyamala na kujeruhiwa na kumwagiwa tindikali machoni
Sababu zilizokuja kutolewa baadae zinachekesha sana.. Nitaweka makala yake hapa

SK alipona na kuendelea na maisha..
EL hakukata tamaa bado alipania kuwa the next president... EL si mpinzani na hakuwahi kuwa mpinzani.. EL alikuwa na hasira na kisasi pande zote mbili UPINZANI NA kwenye chama chake CCM.. EL ni Mmasai asiyeamini kwenye kushindwa.. Aliipenda CCM lakini ikamtenda.. Hakuupenda UPINZANI kwanza ulishamsimanga kwenye list of shame.. Lakini sasa hakuwa na jinsi ilikuwa ni lazima chombo cha kutimiza ndoto zake..

Nguvu ya Dr Slaa CHADEMA ilichagizwa kwa kiasi kikubwa na EL na MWANAHALISI.. SK ni mkosoaji si mwanasiasa.. Connection za EL zilizidi kukatwa na hatimaye akaangukia CHADEMA na SK naye kumfuata huko.. SK baada tu ya kuingia kwenye siasa MWANAHALISI lilipoteza mvuto na umaarufu.. Mwishoni likafungiwa..
Yaliyotokea ni mengi baada ya hapo
Dr Slaa aliyemkaribisha EL CHADEMA alimkimbia.. Wanajuana vema wasingewezana hata kama CHADEMA ingeshinda
Ya Mwakyembe yalipita humohumo..
Kubenea kupitia CHADEMA akaingia rasmi kwenye siasa na kuwa mbungo kupitia jimbo jipya la Ubungo.. Huko kwenye siasa kapwaya.. Huyu si mwanasiasa ni mkosoaji tena wa kuletewa habari.. Hakuna vyanzo tena vya kumpa habari na mfadhili mkuu kaomba poo... Uandishi hauwezi kumlipa tena... Nyakati si rafiki sana.. Familia inahitaji kuishi bado na ni lazima maisha yaendelee

Je Kubenea yuko tayari kufumba macho na kula matapishi yake?
Je Kubenea yuko tayari kusamehe na kusahau ili akae na watesi wake waliomkosakosa kumdhulumu haki yake ya kuishi?
Je abaki CHADEMA iliyombeba na kumsitiri kipindi chote cha miaka mine au avae uso wa mbuzi na kuamua kuunga juhudi?
Wazaramo wanasema KUMKOMA NYANI JILADI... je Kubenea ataweza kufanya hivyo? Ni wazi yuko njiapanda kwakuwa pia ana hofu ya kuwekwa ghalani ama kupelekwa kwa jirani kwakuwa ni kama bohari kuu imejaa kama pishi la mchele... Imejaa WAUNGA JUHUDI BANDIAView attachment 1407054View attachment 1407055

Jr[emoji769]
Naelewa sasa, Sihitaji tena kushabikia siasa kwa namna hii....Bora nikae nyumbani na mke wangu tugegedane tu. OVER
 
Chadema bana wanachekesha bandiko hili limekuja zilivyo zagaa tetesi kuwa ana hama chadema kabla ya hapo halikuja akihama ndio kila mwana ufipa atamtaja Kama rafiki yake na ndugu yake na kumponda Sana yajayo yanafurahisha
 
MHARIRI wa gazeti la MwanaHalisi na Mseto Bw. Saed Kubenea amelihusisha tukio la kuvamiwa na kumwagiwa tindikili kuwa linatokana na kazi zake pamoja na msimamo wa gazeti.

Bw. Kubenea aliyasema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati akitoa ushahidi wake kuhusiana na tukio lililofanyika ofisini kwake la kuvamiwa na kumwagiwa tindikali pamoja na kujeruhiwa kwa sime.

Alidai kuwa alikuwa akipata barua za vitisho kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na mawakili wanaowatetea viongozi wanaodaiwa kuwa ni mafisadi lakini yeye amekuwa akijibu kupitia gazeti lake.

“Tukio hili ninalihusisha moja kwa moja na kazi zangu kwani ndani ya miaka miwili nimeweza kufichukua maovu mengi ndani ya jamii hasa ya viongozi hivyo hata tukio hili nadhani limetokana na hayo,” alidai Bw. Kubenea.

Mbali na barua hizo za vitisho pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa akipokea ujumbe mfupi wa simu za mkononi ambao hakuweza kuusoma lakini mahakama iliutaka upande wa mashitaka kwenda katika kampuni ya simu na kuchapisha ujumbe huo ili uweze kusomwa mahakamani hapo Mei 19 mwaka huu.

Alisema kuwa Januari 5 mwaka huu akiwa ofisini kwake saa 2.00 usiku ghafla alisikia mlango ukisukumwa kwa nguvu na alipokwenda kufungua alikutana na mtu aliyemwamuru kukaa chini lakini alikaidi amri hiyo.

“Baada ya kuniambia nikae chini na amenifuata mimi nilirudisha mlango haraka na kuingia ndani lakini walifanikiwa kufungua mlango huo na kuingia vijana watatu ambao walianza mashambulizi hadi kunimwagia maji maji ambayo yanilifanya nipoteze uwezo wa kuona kutokana na macho kuingiwa na maji hayo,” alisema Bw. Kubenea.

Alisema kuwa katika purukushani hizo, Mhariri mwenzake, Bw. Ndimara Tegabwage alifanikiwa kuwazidi nguvu waliokuwa wamevamia na kutoka nao nje ya ofisi ambapo walikimbia.

Baada ya kukimbia kwa wavamizi hao, walikwenda hospitali iliyopo Kinondoni na walifanikiwa kutoa taarifa hizo katika Kituo cha Polisi Oysterbay na askari walifika hospitalini hapo na kuwashauri kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Alidai kuwa kutokana na madhara ambayo aliyapata kwa kumwagia kemikali alilazimika kwenda India kwa matibabu zaidi.

Kesi hiyo ina jumla ya washitakiwa sita ambao baadhi yao wako rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamama.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni, Bw. Alex Anyemike, Bw. Hashimu Mdoe, Bw. Augustino Kimario, Bw. Hamisi Almasi, Bw. Alfred Benard na Bw. Frednand Msekwa ambao wanadaiwa Januari 5 mwaka huu, Kinondoni katika ofisi za Gazeti la MwanaHalisi na Mseto waliwajeruhi, Bw. Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage.

Inadaiwa Bw. Kubenea alijeruhiwa kwa sime katika shavu na kumwagiwa kemikali na Bw. Tegambwage alikatwa kwa sime kichwani

Jr[emoji769]
 
mr chopa mimi sio CHADEMA soma kwa makini andiko langu
Chadema bana wanachekesha bandiko hili limekuja zilivyo zagaa tetesi kuwa ana hama chadema kabla ya hapo halikuja akihama ndio kila mwana ufipa atamtaja Kama rafiki yake na ndugu yake na kumponda Sana yajayo yanafurahisha

Jr[emoji769]
 
Bro natafuta kazi kama yako siwezi kupata hapo Lumumba?. maana maisha yanabana kweli kitaa afu nyie wenzetu mnashaini tu na elfu saba kwa siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda ufipa ukageuzwe msukule Kama wenzako hutakuwa na akili Tena ya kuwaza maisha utakuwa tarumbeta tu humu la kupiga kelele kila kitu
 
Baada ya uhuru bado tuliendelea kuwa na mahusiano mena na waingereza.. Walitusaidia kwa mengi ili tuweze kusimama tena kama taifa huru (japo in return walitegemea fadhila fulani toka kwetu)

Mojawapo ya mikataba tuliyofunga nao ni kutumia magari yanayotengenezwa kwao kama magari rasmi ya serikali ya Tanzania.. Popote ulimwenguni hakuna dili kubwa kama hili kwakuwa akitumiacho serikali ndio mwananchi atakitumia hichohicho

Kwahiyo usafiri rasmi wa serikali ukawa ni Land rover 109 by then... Just imagine ni tenda kubwa kiasi gani kwa serikali yote nchi nzima... Lakini hapo hapo wananchi nao wakawa wanaona fahari kununua magari kama ya serikalini (ona ma vx leo hii)

Sijui ninini kilitokea kwa hakika.. Lakini Mjep akatia fitina na kufanikiwa kupora tenda husika toka uingereza.. Mfanikisha dili akiwa Mzee Malecela by then na msaidizi wake akiwa EL.. EL akamchezea rough Mzee na kuchukua hongo yote... Nitasimulia zaidi

Back kwa Mchonga.. Waingereza walilia na Mwalimu kwa kusitisha mkataba.. Walimuona kama msaliti baada ya kumsaidia kwenye mengi... Tukaingia kwenye migogoro ya kidiplomasia lakini ikamalizwa kimyakimya..

Hata hivyo tangu wakati huo hatukuwa vizuri tena na hawa jamaa na ndio maana waliokuwa wanafahamu undani wa hili jambo hawakutaka kabisa Mwalimu akatibiwe uingereza

Dah, ulipogusia Hapo kwa mchonga na Landcruiser natamani nielewe kidogo.. Ishu ni nini?

Jr[emoji769]
 
Naona leo mmelipwa vizuri mkarudi kwa kasi mtandaoni....
Haya ni matumizi mabaya ya fedha za misaada. Watu wa Mungu wamejitoa kusaidia mapambano dhidi ya Corona matokeo yake vifaa walivyotoa bure vinauzwa fedha anapewa Polepole kulipa madeni ya Lumumba Bk7!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fainali uzeeni. Kama hujajipanga imekula kwako na ikiongezewa na athari za kiuchumi kutokana na CORONA, itakuwa balaa kwa ujasiriamali wa kisiasa.
 
Kwenye list of shame Lowassa alitajwa kama chambo tu na kufunika ukweli ila kiuhalisia habari za siri za serikali yeye ndio alikuwa mvujishaji
Mshana Jr

Asante sana. Ni kwa kiasi gani nguvu ya Dr. Slaa CHADEMA ilichagizwa na EL?

Jr[emoji769]
 
Hitimisho langu [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Kasema hatoondoka chadema , amezungumzia corona pia
Je Kubenea yuko tayari kufumba macho na kula matapishi yake?
Je Kubenea yuko tayari kusamehe na kusahau ili akae na watesi wake waliomkosakosa kumdhulumu haki yake ya kuishi?
Je abaki CHADEMA iliyombeba na kumsitiri kipindi chote cha miaka mine au avae uso wa mbuzi na kuamua kuunga juhudi?
Wazaramo wanasema KUMKOMA NYANI JILADI... je Kubenea ataweza kufanya hivyo? Ni wazi yuko njiapanda kwakuwa pia ana hofu ya kuwekwa ghalani ama kupelekwa kwa jirani kwakuwa ni kama bohari kuu imejaa kama pishi la mchele... Imejaa WAUNGA JUHUDI BANDIA


Saed Kubenea: Sina mpango wa kuondoka CHADEMA - JamiiForums


Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom