Mkuu, nimesoma MwanaHalisi ya leo na kuirudia mara nne, napata wasiwasi kuwa Kubenea tumempoteza. Habari kuu ya leo ni Sitta, Mwakyembe na Nape. Akina Rostam, Chenge na Lowassa wanatajwa kisaniisanii tu, wamechomekezwa tu. Halafu, Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya ambaye mshahara wake hauzidi shilingi laki mbili kwa mwezi (na ambaye MwanaHalisi ilishawahi kumwita kibaraka wa Lowassa alipojitoa kugombea ubunge Monduli) "ananunua" ukurasa mzima wa MwanaHalisi kusimulia jinsi CCJ ilivyoungwa mkono lakini bila kuanzishwa rasmi!
Haiingii akilini kwa mwandishi makini kama Kubenea, mpambanaji shupavu kama Kubenea, mpigania haki na mchambuzi wa habari makini kama Kubenea, leo anataka kutuambia kwamba anayefikiria kuanzisha chama cha siasa au kukiunga mkono chama fulani ambacho hata hivyo hakikuweza kuanzishwa, ana makosa sawasawa na maharamia waliobaka rasilimali za nchi yetu toka uhuru na kutufanya tubaki masikini wa kutupwa wakati Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa na kila aina ya utajiri. HAPA SIKUBALIANI KABISA NA KUBENEA COME SUN COME RAIN! Nikikubaliana naye kwa hili, basi itabidi nikubaliane naye aendeleze kampeni ya kumsulubu hata mzee wetu MUSTAFA SABODO kwa kuichangia CHADEMA wakati yeye ni mwana CCM!
Anaowachochea wasulubiwe leo ni victims wa protracted hate campaign ya Rostam na Edward kuanzia mwaka 2007 na ambao, tutake tusitake, walichangia kuliweka suala la ufisadi kwenye agenda za nchi na mpaka leo wanaangaliwa kwa jicho la uhasama na mafisadi wote ndani ya Chama Tawala kuwa chanzo cha kusulubiwa kwao. CCJ, pamoja na kuwa Chama hewa, kiliitingisha CCM kisawasawa na kuishikisha adabu. Yeyote aliyekuwa nyuma ya uanzishwaji wa Chama hicho nampongeza, hastahili kusutwa na wanademokrasia wote na wapenda usawa na haki. Kubenea anapopoteza karatasi na muda mwingi kuwashambulia akina Sitta, Nape, Mwakyembe kwa ajili ya kitu ambacho si jinai, bali ni sehemu ya demokrasia, ananipa wasiwasi kuhusu uelewa wake wa mambo. Ningemtegemea zaidi mtu kama Tambwe Hiza, Makamba n.k. wenye maslahi finyu ndani ya CCM na wenye hasira (zinazochelewa sana kupanda) kwamba CCJ iliwatingisha, kuwa na msimamo huo, lakini si mwanaharakati kama Kubenea! Pamoja na hilo, huwezi kumhukumu mtu kwa hearsay (maneno ya kusimuliwa na akina Mpendazoe) na vilevile kwa chama ambacho hakikupata fursa kuingia ulingoni.
Kadiri tunavyosonga mbele, maswali mengi yanajitokeza: Hivi hawa akina Mpendazoe, Slaa and company, kwa nini walishindwa kutumia hoja hii kuwapunguzia kura akina Mwakyembe na Sitta kwenye majimbo yao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu? Kwa nini "makada" wa CCM kama akina Daniel Ole Porokwa wanajitutumua leo kwa gharama kubwa ya kuruka na ndege toka Arusha hadi Dar na kuandaa Press Conference kwenye majengo ya kifahari, wasifanye hivyo kwenye vikao vya NEC mikoa na Taifa vya mchujo wa wagombea ubunge? Hivi wote, makada wa CHADEMA na CCM walikuwa wanasubiri tu mchakato wa kuvuana magamba ndipo waingize suala la CCJ? Naamini tumeanza kumpoteza Kubenea polepole, lakini ni wajibu wetu sote kumrejesha kwenye mstari wa mapambano halisi. It is not too late. Inatia wasiwasi sana kuona kuwa kwa mara ya kwanza katika miaka mingi ambayo nimeanza kusoma MwanaHalisi, ni kipindi hiki nashuhudia magazeti ya mafisadi (MTANZANIA, TAZAMA, RAI) yakiongea lugha moja na gazeti letu kipenzi la MwanaHalisi. It is not healthy at all. Kubenea unatuulia gazeti.