Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Homeboy

Jamaa anauza story hakuna kitu kama hicho! Ni vita wanapigana Magamba hao wanajaribu kumtumia Kubenea kama AK47. Kubenea is not that much cheap. Wanajua Magazeti yao ya Uhuru, Mzalendo, Habari leo hayauziki.

Reverend nakubaliana na wewe! Said angekuwa mtu wa hivyo, angekuwa amechukua hela nyingi wakati ule kabla ya kufichua uozo wote aliokwisha ufufua! Said ana mipango ya kupata mitambo yake na si ajabu kesha pata, sasa mifisadi inataka kumpakazia!
 
majungu tu hana lolte huyu mtoa mada, yaani mwenzetu mpaka toleo lijalo ameshajuwa litaandika nini, kama si wehu huu tuuwitaje?

Hizo ni habari za ndani kwahiyo mleta thread asipuuzwe kuna jambo analifahamu.
 
hakuna haja ya kumshambulia source kwa mada yake kilichobaki kwa sasa ni kufanyia uchunguzi tukianzia ijumaa. Mwisho wa siku ikmbukwe kuwa we all struggle for profit!
 
MwanaHALISI la leo ni "Sitta, Mwakyembe, Lowassa watoswe". Imeandikwa na Kubenea mwenyewe kwa kuchanganya mada. Nadhani alipita JF jana. Kamtumia Dr Hassy Kitine.
 
Kubenea hajanunuliwa. Kwanza, gazeti la MwanaHALISI linakwenda mtamboni Jumatatu jioni kwa hiyo stori hii haiwezi kuwa imeandikwa baada ya KUbenea kutembelea JF kama mnavyotaka kuaminisha umma. Hayo ni mambo ya kufikirika tu.

Pili, Alichokifanya leo ni kuonyesha kazi ya uandishi wa habari inavyotekelezwa. Amewachukuwa wahaini wote na kuwaweka kikapu kimoja. Kazi kwako Kikwete- Hongera Kubenea. HONGERA MWANAHALISI kila mmoja umempa hukumu yake.
 
Kubenea endelea kuanika ukweli. Mungu yupo pamoja nawe. Ulipoanza kumchambua Lowassa walisema umetumwa na Mengi na unatumiwa na kina Sitta. Leo unaandika juu ya kina Mwakyembe na Sitta wameanza kukusakama kuwa umenunuliwa na kina Lowassa. Je, hawa hawamjui mtu anayenunuliwa. Soma MwanaHALISI utaona hoja za Kubenea katika makala ya GUMZO. MTU ALIYENUNULIWA ANAWEZA KUANDIKA YALE? ACheni kumchafua kipenzi cha wananchi.
 
Kujidhalilisha sio mpaka uvue nguo hadharani, hata mawazo na hoja unazotoa kama ni utumbo kama huu ni kujidhalillisha.Suala la Kubnea eti apewe mil 20 ili aharibu biashara yake haliingii akilini, labda mwendawazimu tu ndio anaweza kukubali.Habari ya Parokwa kuandikwa kwa kina kwenye Mwanahalisi tunalitegemea kwa sababu huwa linafanya hivyo kwa kila matukio ambayo huitaji ufafanuzi zaidi.Hata RAI mwema litaandika cause haya ndio magazeti yanayotupa habari kwa kina zaidi kuliko mengine yote.Acha kudhalilisha watu kama umetumwa na wenye Magamba umegonga mwamba,kachukue posho yako, kazi umeshafanya ingawa bikla mafanikio.
 
Hatukatazwi Kupenda mtu/kitu lakini ni vizuri sana kuruhusu Bongo zetu kuwaza 'Kinyume cha Mambo' (Mohamed Said Abdullah akimtumia Bwana Msa).

Nimeisoma thread hii na kugundua kuwa Watanzania wengi hawako tayari kufikiri kinyume na kile wanachopenda kufikiri.
Nimegundua kuwa watanzania wengi wanapenda kupata mtu wa kuwapigania vita vyao lakini wao wenyewe wanabaki kuwa Wapambanaji wa kwenye Keyboard tu.

Nimegundua kuwa Watanzania wengi hawataki kusikia mawazo mbadala (nasisitiza, mawazo mbadala) kumhusu yule waliyemteua kuwa mpiganaji vita wao.

Watanzania wengi hawaamini katika msemo wa 'Everyone has his/her Price'.. Kila Mtu ana Bei Yake.
Kuna member ametoa uchambuzi mzuri sana kuhusiana na mabadiliko ya Vichwa vya Habari vya Mwanahalisi. Ni wachache sana wamechangia kuhusu hili.

Imetolewa hoja kuwa tusubiri Mwanahalisi tuone Kichwa cha habari. Nimelinunua na kichwa kikuu cha habari kinasema 'Sitta, Mwakyembe, Lowassa Watoswe'

Inawezekana kikawa kichwa cha habari cha kawaida na kinachoweza kutumika kushinda hoja ya mwanzilishi wa thread, lakini unaposoma habari yenyewe na kukuta aslimia kubwa ya content ya habari yenyewe (karibuni 90%) inahusu zaidi tuhuma za Sitta na Mwakyembe za kuwa waanzilishi wa CCJ na uwezekano wao wa kufukuzwa kwenye Chama na habari/majina ya Lowassa/Rostam/Chenge yametajwa kwenye paragraph MOJA tu kati ya karibuni Paragraph 40 za habari hiyo huku majina ya Sitta na Mwakyembe yakitajwa almost kila baada ta Pragraph moja ni lazima tuzipe nafasi akili zetu ya kuanza kujiuliza...!
 
Nimeisoma thread hii na kugundua kuwa Watanzania wengi hawako tayari kufikiri kinyume na kile wanachopenda kufikiri..

BABA DESI, FUNGUKA..WAKINA RACHEL WALISHAVULIWA NGUO KWA KIASI CHA KUTOSHA NA WATANZANIA WALA HATUNA MASHAKA KUWA HAWAFAI KUWA CCM,KUBENEA SASA ANAJARIBU KUONESHA UPANDE MWINGINE WA COIN..HAKUNA MANTIK YA KUTUMIA MUDA MWINGI KUWAELEZEA AKINA RACHEL ILI ETI USIONEKANE UMENUNULIWA..KILICHOPO MEZANI NI UNAFIKI WA 6&CO..BIG UP KUBENEA
 
HIVI KUBENEA AMESOMA MPAKA WAPI? Hebu wana JF nimwagieni CV yake hapa ili nimuassess vizuri kama mtu solid au boya.:mod:
 
HIVI KUBENEA AMESOMA MPAKA WAPI? Hebu wana JF nimwagieni CV yake hapa ili nimuassess vizuri kama mtu solid au boya.:mod:

Mijitu mizuzu utaijuwa tu kwa matendo yao, hivi haujuwi kwamba Kikwete ana degree ya uchumi? na haujui kama Balali alikuwa ni Phd Holder?
 
Tuombe Mungu huyu isiwe kweli. maana tunampoteza mtu ambaye amekuwa silaha kwetu kufukua yaliyooza. Mungu tunusuru.
 
Kijembe ambacho mmoja wa mapacha watatu wa ufisadi, Rostam Aziz Abdulrasul, alikirusha kwa Saed Kubenea kuwa anaweza kumnunulia mtambo wa kuchapishia gazeti lake la MwanaHalisi mapema mwaka huu, kimegeuka kuwa "azma iliyotimia" baada ya mwandishi huyo machachari aliyejizolea sifa kemkem kwa ujasiri kutiwa mfukoni na sasa ni sehemu ya majeshi ya Rostam ya kumlinda na kuwasambaratisha wabaya wake!

Kubenea ambaye mwaka juzi alishambuliwa na watu "wasiojulikana" na kumwagiwa tindikali machoni karibu apofuke, kasahau yote hayo na sasa ni silaha ya kuaminika ya Rostam katika kujihami dhidi ya kampeni kali ya CCM inayoongozwa na Katibu Mwenezi Taifa Nape Nnauye ili mkuu wake mpya Rostam abakie na gamba lake.

Taarifa za ndani kwenye duru za mwanahabari huyo zinasema kijembe kile cha kumnunulia Kubenea mtambo wa kuchapishia magazeti kimefanyiwa kazi na Kubenea yuko mbioni kupata mtambo mpya wa kisasa lakini kwa sharti la kuachana na habari hasi za Rostam na Lowassa kwenye gazeti lake na kuendesha kampeni kali dhidi ya msururu wa watu aliopewa katika miaka mitatu ijayo. Baadhi ya watu hao ni JK na familia yake, "Mtoto wa Mkulima", Magufuli, Chilligati, Nape, Sitta, Anne Kilango, Ole Sendeka, Lembeli, Mwandosya, Membe, Kinana, Mwakyembe, Mkuchika, Chatanda na Kigoda. Kubenea kakubali dili hilo ambalo tayari limemwingizia zaidi ya sh. milioni 20.

Gazeti la MwanaHalisi ambalo limekuwa kwa muda mrefu msumari wa moto kwa mapacha watatu wa ufisadi kutokana na Kubenea kuamini kwamba wawili kati ya mapacha hao watatu walihusika na mpango wa kumtoa roho au kumpa kilema cha maisha, halitabeba taarifa tena za Lowassa wala Rostam ila za wabaya wao hao.

Mathalan, toleo la kesho kutwa la MwanaHalisi tayari lina taarifa ndefu ya Daniel Porokwa akiwamwagia sumu "maadui" wa RA na EL bila kujali kuwa gazeti lake lilimwandika Porokwa mwaka jana kuwa kibaraka wa Lowassa baada ya kujitoa kugombea Ubunge jimbo la Monduli. Porokwa "alizawadiwa" kazi ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya, gari mpya aina ya NOAH, shilingi milioni 2, na ng'ombe kadhaa baada ya kujisalimisha na kukubali Lowassa amkanyage kichwani kwa mila eti ya Kimasai kama siyo ya kishirikina.

Hongera mtoa taarifa hizi (Kamaudoulton) nyeti ambazo zina harufu ya ukweli sina sintokuwa na mashaka na taarifa hizi kwani kuna taarifa mashirika ya pensheni za hivi karibuni haswa ppf juu madudu yake lakini Kubenea hakuweza kuandika kabisa nondo za wana jf mpaka magazeti mengi mfano mwananchi, habari leo na mengine mengi walito taarifa kwa mwananchi juu madudu ya shirika hilo lakini mwanaHalisi likakaa kimya ndipo nikajua kweli kubenea amekuwa siyo tunaye mfahamu. Tayari ameshaanza kupokea mirungula.
 
Tuombe Mungu huyu isiwe kweli. maana tunampoteza mtu ambaye amekuwa silaha kwetu kufukua yaliyooza. Mungu tunusuru.

Mkuu, nimesoma MwanaHalisi ya leo na kuirudia mara nne, napata wasiwasi kuwa Kubenea tumempoteza. Habari kuu ya leo ni Sitta, Mwakyembe na Nape. Akina Rostam, Chenge na Lowassa wanatajwa kisaniisanii tu, wamechomekezwa tu. Halafu, Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya ambaye mshahara wake hauzidi shilingi laki mbili kwa mwezi (na ambaye MwanaHalisi ilishawahi kumwita kibaraka wa Lowassa alipojitoa kugombea ubunge Monduli) "ananunua" ukurasa mzima wa MwanaHalisi kusimulia jinsi CCJ ilivyoungwa mkono lakini bila kuanzishwa rasmi!

Haiingii akilini kwa mwandishi makini kama Kubenea, mpambanaji shupavu kama Kubenea, mpigania haki na mchambuzi wa habari makini kama Kubenea, leo anataka kutuambia kwamba anayefikiria kuanzisha chama cha siasa au kukiunga mkono chama fulani ambacho hata hivyo hakikuweza kuanzishwa, ana makosa sawasawa na maharamia waliobaka rasilimali za nchi yetu toka uhuru na kutufanya tubaki masikini wa kutupwa wakati Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa na kila aina ya utajiri. HAPA SIKUBALIANI KABISA NA KUBENEA COME SUN COME RAIN! Nikikubaliana naye kwa hili, basi itabidi nikubaliane naye aendeleze kampeni ya kumsulubu hata mzee wetu MUSTAFA SABODO kwa kuichangia CHADEMA wakati yeye ni mwana CCM!

Anaowachochea wasulubiwe leo ni victims wa protracted hate campaign ya Rostam na Edward kuanzia mwaka 2007 na ambao, tutake tusitake, walichangia kuliweka suala la ufisadi kwenye agenda za nchi na mpaka leo wanaangaliwa kwa jicho la uhasama na mafisadi wote ndani ya Chama Tawala kuwa chanzo cha kusulubiwa kwao. CCJ, pamoja na kuwa Chama hewa, kiliitingisha CCM kisawasawa na kuishikisha adabu. Yeyote aliyekuwa nyuma ya uanzishwaji wa Chama hicho nampongeza, hastahili kusutwa na wanademokrasia wote na wapenda usawa na haki. Kubenea anapopoteza karatasi na muda mwingi kuwashambulia akina Sitta, Nape, Mwakyembe kwa ajili ya kitu ambacho si jinai, bali ni sehemu ya demokrasia, ananipa wasiwasi kuhusu uelewa wake wa mambo. Ningemtegemea zaidi mtu kama Tambwe Hiza, Makamba n.k. wenye maslahi finyu ndani ya CCM na wenye hasira (zinazochelewa sana kupanda) kwamba CCJ iliwatingisha, kuwa na msimamo huo, lakini si mwanaharakati kama Kubenea! Pamoja na hilo, huwezi kumhukumu mtu kwa hearsay (maneno ya kusimuliwa na akina Mpendazoe) na vilevile kwa chama ambacho hakikupata fursa kuingia ulingoni.

Kadiri tunavyosonga mbele, maswali mengi yanajitokeza: Hivi hawa akina Mpendazoe, Slaa and company, kwa nini walishindwa kutumia hoja hii kuwapunguzia kura akina Mwakyembe na Sitta kwenye majimbo yao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu? Kwa nini "makada" wa CCM kama akina Daniel Ole Porokwa wanajitutumua leo kwa gharama kubwa ya kuruka na ndege toka Arusha hadi Dar na kuandaa Press Conference kwenye majengo ya kifahari, wasifanye hivyo kwenye vikao vya NEC mikoa na Taifa vya mchujo wa wagombea ubunge? Hivi wote, makada wa CHADEMA na CCM walikuwa wanasubiri tu mchakato wa kuvuana magamba ndipo waingize suala la CCJ? Naamini tumeanza kumpoteza Kubenea polepole, lakini ni wajibu wetu sote kumrejesha kwenye mstari wa mapambano halisi. It is not too late. Inatia wasiwasi sana kuona kuwa kwa mara ya kwanza katika miaka mingi ambayo nimeanza kusoma MwanaHalisi, ni kipindi hiki nashuhudia magazeti ya mafisadi (MTANZANIA, TAZAMA, RAI) yakiongea lugha moja na gazeti letu kipenzi la MwanaHalisi. It is not healthy at all. Kubenea unatuulia gazeti.
 
Ahsante Mkuu kwa kunielewa. Nilipoanzisha hoja hii baadhi ya wanaJF waliishia kunitupia madongo tu bila kutafakari. Sikufanya hivyo kwa kumchukia Kubenea ila kwa sababu mimi ni shabiki wake wa miaka mingi. Sasa nasadiki yote waliyonieleza maana yamejitokeza kwa asilimia 100 kwenye toleo la sasa la MwanaHalisi. Mkono wa Rostam, Lowassa na watu wasio na itikadi ndani na nje ya CCM unaonekana bayana!
 
Back
Top Bottom