Kubeza maendeleo yaliyoletwa na CCM ndani ya miaka 60 ni kukosa busara. Tulipata uhuru tukiwa nyuma sana kimaendeleo

Kubeza maendeleo yaliyoletwa na CCM ndani ya miaka 60 ni kukosa busara. Tulipata uhuru tukiwa nyuma sana kimaendeleo

Hivi wakati tunapata uhuru hali yetu ya uchumi (pato la taifa + deni la taifa) ilikuwaje na sasa ikoje?
 
Bora kukosa busara kuliko kukosa akili kwa kufikiria maendeleo yameletwa na CCM badala ya WATANZANIA WENYEWE. Mshajiona wenye nchi kiasi kwamba CCM ni muhimu kuliko Tanzania? 😡
Ndio maana katiba mpya hawaitaki maana itawapotezea sifa za kijinga wanazopeana
 
Inashangaza sana kusikia mtu anakebehi kuwa Ccm imelifanyia nini taifa hili ndani ya miaka sitini.

Pamoja na kuwa tulikuwa chini ya uangalizi wa UN mpaka tutapopata uhuru lakini mwangalizi wetu yaani Mwingireza hakufanya maendeleo ya maana kama katika makoloni yake ya kudumu kama Kenya na Zimbabwe. Hivyo mpaka anatupatia uhuru aliacha taifa letu lipo na hali mbaya ya kiuchumi na maendeleo.

Mw Nyerere alipopata uhuru aliandaa misingi mizuri ili kila mtu aweze kufaidi keki ya taifa hasa kwa kuanzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Na ilikuwa na nia nzuri tu ila husuda za Mapebari wakamuangusha.

Tuachane na setbacks na mafanikio katika awamu zote tano mpaka hii ya mama Samia
Ukweli ni kuwa kwa taifa lililokuwa halina kitu kimaendeleo, leo hii tunamiundombinu iliyosimama ya barabara, afya,elimu hadi viwanda. Si busara kuibeza Ccm ambayo iliachiwa nchi ikiwa masikini kabisa kwa kila namna. Na leo hii tupo hii stage.

Kwani mnaobeza mlitaka tuwe kama Usa ambao wanamiaka zaidi ya mia mbili tangu wapate uhuru?
Tache kujifariji kama njia ya kutokutaka kuwajibika kikamilifu au njia ya kutetea mapungufu yetu.
 
Swali zuri sana hilo bwashee. Chadema ina miaka zaidi ya 25 ya uhai, lakini mpaka sasa haina hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu! Hitimisho: chadema ni kama huyo mtoto 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
CCM warudishe mali zote walizochuma kwa Watanzania halafu tuone kama hawajabaki uchi.
 
Argument yako ni illogical, una maana chadema hawana hata kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu kwa sababu ccm walichuma mali?
CHADEMA mnaowasema hawana makao makuu, kutwa mnafanya figisu kutaka kuwadhoofisha na kuwaua; yaani mnateseka na chama ambacho hakina hata "kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu"
 
CHADEMA mnaowasema hawana makao makuu, kutwa mnafanya figisu kutaka kuwadhoofisha na kuwaua; yaani mnateseka na chama ambacho hakina hata "kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu"
Bwashee ebu niambie kilipo kiwanja cha kujenga ofisi ya makao makuu ya chadema. Nasubiria kwa hamu unijuze!
 
Nini maana ya kuchagua chama kiunde serikali?
Hao waliouwa viwanda, killimo na elimu na kutugawa watanzania ndio unawazungumzia? Hamna kitu wametufukarisha sana hao na mawazo yao ya kimaskini, eti nataka matajiri waishi kama mashetani, pumbav.

Acha Ujinga.
 
Back
Top Bottom