mashuleni kuna adhabu za bakora zaidi ya hizo na sioni watu wakipost kabisa.
Hata kitabu cha biblia kinasema kuwa upumbavu umefichwa katika moyo wa mtoto hivyo fimbo ndio hutumika kuuondoa. Ikaenda mbele ikasema kuwa mzazi asiyemchapa fimbo mwanawe ,hampendi.
“Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na kuzimu” (Methali 23:13-14)
Mithali 22:15
"Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,
bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye."
methali 20:30
"Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,
nayo michapo hutakasa utu wa ndani"
methali 13:24
"Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema."
ndugu yangu, mimi nilishadeclare interest humu kuwa ni mwanasheria na nimeshawakilisha kesi nyingi sana za mauaji, hicho kipigo cha mithali kwenye Biblia, ndio kipigo kikubwa kama kile? ndio kupiga mtoto kama unauwa nyoka, mahakamani huko kuna kesi nyingi tu za mzazi kuua mtoto, anafikiri anaadhibu, wengine wanapiga mateke, wengine ngumi, wengine anampiga mtoto kofi nzito, anadondoka, anasubiri wee kwamba ataamka, mtoto ndio amekufa hivyo. kesi nyingi sana zipo huko mahakamani wazazi kuua watoto na wanaishia masononeko maisha yao yote.
zaidi ya yote, mtoto anayepigwa kama hao kwenye madrasa anaingiziwa roho ya hofu na ukatili kana kwamba hata akifanyiwa kitendo kibaya akatishiwa kwamba asiseme akisema atashughulikiwa, hata ufanyeje ataificha hiyo siri. siri hizo za kubakwa na kulawitiwa n.k, ambazo mtakuja kuzijua akiwa mtu mzima ameshaharibika yupo upande mwingine wa shilingi.
sisi sote watoto huwa tunawaadhibu, ila unamkalisha, mnajadili na kumweleza kosa alilofanya na unamwadhibu kistaarabu sio kumkomoa ila kumrekebisha. unampa na mtoto nafasi ya kujieleza kwa nini amekosea, mara nyingi watu wanapiga watoto kwa sababu wamejipakulia mboga hasa nyama, kumbe mtoto alikuwa anaona njaa, ungemuuliza angesema mama nimekula nyama hiyo kwa sababu nilikuwa na hamu au niliona njaa, na kwa sababu umezoea kumpigapiga hata ukirudi hatakwambia "mama nimekula nyama" kwa sababu anajua utampiga, ila kama wewe ni rafiki, ukirudi tu atakwambia unajua nini maza nimeona njaa nikala nyama.
watoto hao wa shule wengine wanapitia mateso makubwa kwa wazazi wao, wengine wakirudi nyumbani wanajitafutia vyakula, wazazi wapo ulevini huko au wapo kutafuta maisha wanarudi usiku, watoto wanaosha vyombo, wanafanya kazi zote mama akifika pawe panaeleweka, wanachoka, na bado shuleni wanahcapwa viboko, nyumbani wanachapwa, madrasa wanachapwa sasa wakimbilie wapi? ndio wanabaki na mioyo ya sugu na ukatili unazaliwa. mi nilifikiri huko madrasa ndio lingekuwa kimbilio kwa watoto kwa sababu wanaenda kufundishwa mambo ya Mungu, sasa huko nako wanaumizwa wakimbilie wapi sasa? si ndio maana wanakimbilia mtaani?