Kuchapwa watoto kiasi hiki ni sawa?

Kuchapwa watoto kiasi hiki ni sawa?

Aise tulivyokuwa wadogo muda wa madras sisi wakristo tulijaribu kwenda siku moja kuwasindikiza wenzetu ili wakimaliza elimu yao tuendelee kucheza na mpira wetu wa matambara.
Aisee kipondo walichokuwa wanakipata pale hatukuenda tena!
Kwanza tukashangaa mbona mafundisho yetu ya komunio na kipaimara hatushushiwi kipigo vile?! Eti kisa wenzetu wamekosea kukariri alfu be te....
Maustadhi wanakosea sana. Ni kama ma stress yao wanayaleta pale au labda ni wakatili tu!
Hahahha hadi mkajuta kuwasindikiza
 
Mkuu, Unayaita maisha waliokulia na kulelewa wazazi wako ni ya kishamba na kibushiparty? Yan walikuwa na maisha hayo halafu wakaweza kukuzaa, kukulea hadi leo umekuwa mtu mzima mwenye akili timamu then unadiriki kuinua kalamu na kuandika kwamba eti hayo yalikuwa ni maisha ya kishamba na kibushiparty? Kweli?
Mimi nadhani kilichokuwa sahihi ni kuyaangalia maisha hayo na kuchota yale yaliyokuwa mambo mazuri, yenye kuboresha na kuheshimisha kizazi cha sasa. Hizo ni Tunu za maisha. Yale unayoona sio sawa uyaache- chukua yale mema na uyaendeleze.
Mtoto, hata mtu mzima hustahili kuadabishwa (ndio haki yake au malipizi yake). Tukumbuke adhabu sio zawadi na lengo la adhabu ni kumfanya mhusika aone, achukie na kutubia kosa lake; tena ajitahidi kwa bidii zote kutokurudia tena kosa alilotenda. Kutokutoa adhabu kwa mkosaji ni kosa kubwa sana kwani mkosaji huyo ataona ni kawaida tuu atazembea na atarudia-rudia kosa hilo na hatimaye atajenga tabia. Je, hiyo ni sawa?
Kwa mfano mtoto wako wa kike (darasa la 5) anaanza mazoea ya kukutana na wavulana wanampa vizawadi e.g. pipi au fedha faraghani na anawaruhusu wamshike-shike makalio au chuchu(kama zipo) halafu ww mzazi siku moja unabahatika kumkuta live. Ukimhoji ulikuwa unafanya nn anakujibu "sio kitu". Unarudia swali tena kwa ukali lakini bado anakujibu anakuangali macho makavu "miye sijafanya kitu"
Mara paap! Anatokea mamaake na akiwa bado yu mbali kidogo anakuambia: "mwache huyo mtoto mbona alikuwa anacheza tuu? .....
Dah! hapo ujue siku yako imeshaharibika. Utaendeleaje? Kucheka? Kununa? au kutafuta mwarobaini?
Mwisho: Inakuwaje "wazazi mashabiki" tukio la kawaida kabisa mashuleni linapigwa vid.clip na linasambazwa mitandaoni kwa maneno mazito eti ni ukatili uliopitiliza ili kuamsha hisia ndani ya Jamii na tena kuamsha hisia za chuki baina ya familia ya mtoto na mwl. aliyetoa adhabu hiyo? Hilo ni kwa lengo Ovu. Kwani kulikuwa na shida au ugumu gani kuripoti tatizo hilo kwenye uongozi wa shule ili kuwezesha kulipatia ufumbuzi at local level na under field conditions? Tunakuza jambo dogo kiasi hicho utadhani mtoto amechunwa ngozi hadi kwa Mufti, Polisi na kwa waziri Mh. Dr. D. Gwajima.
Je, mtoto aliyechapwa aliumia/alidhurika kiasi hadi akalazwa Hospitali? Hakuna watoto wengine waliochapwa siku hiyo? Je, madrasa hiyo haina uongozi au msimamizi (ukimwacha huyo mwl)? Kooote huko "wazazi mashabiki" mmeona hakufai ila ni kumlipua mwl.
Sijui unataka kutuambia nini, nimechoka kusoma
 
Hivi bado mnachapana mboko? Mtoto anaishi yale anayoyashuhudia. Yaani ana adopt. Wa kuchapwa ni mzazi anayeshindwa kumtengenezea mazingira salama mtoto
 
Wewe bado upo kijijini au haujasoma, sikucheki ila nakuonea huruma, Mungu akusaiide. maisha wazazi wangu waliyokulia yalikuwa mabaya sana na hawakutaka mimi nikulie hayo, na hata mimi niliyokulia yalikuwa sio perfect na sitaki watoto wangu wapitie hell niliyopitia. kama haujaelewa sina kingine cha kukusaidia.
 
mashuleni kuna adhabu za bakora zaidi ya hizo na sioni watu wakipost kabisa.

Hata kitabu cha biblia kinasema kuwa upumbavu umefichwa katika moyo wa mtoto hivyo fimbo ndio hutumika kuuondoa. Ikaenda mbele ikasema kuwa mzazi asiyemchapa fimbo mwanawe ,hampendi.

“Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na kuzimu” (Methali 23:13-14)
Mithali 22:15
"Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,

bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye."

methali 20:30
"Mapigo na majeraha huusafisha ubaya,

nayo michapo hutakasa utu wa ndani"

methali 13:24
"Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema."
Duuuh hii kalii.
 
Labda kwasababu hapo ni madrasa sidhani kama viboko vinahitajika. Halafu pia hivyo vitoto bado vidogo.

Ila mbona sie tukiwa primary na sekondari tumechapwa sana, hapo ni cha mtoto.
Mnataka kuniambia kwamba siku hizi hakuna shule inayochapa viboko?
 
Zipo. Ila viboko vya madras si mchezo! Shuleni at least kale kaptula ka khaki na wavulana sababu ya utundu na kujiandaa tulikuwa tuna vaa 2!
Madras si mchezo aisee!
 
Wewe bado upo kijijini au haujasoma, sikucheki ila nakuonea huruma, Mungu akusaiide. maisha wazazi wangu waliyokulia yalikuwa mabaya sana na hawakutaka mimi nikulie hayo, na hata mimi niliyokulia yalikuwa sio perfect na sitaki watoto wangu wapitie hell niliyopitia. kama haujaelewa sina kingine cha kukusaidia.
Hii imekaavizuri sana. Kumbe unaelewa kukumbuka Ulipotoka, Ulipo kwa sasa, Unaelekea wapi na Utafikaje huko. Hiyo ni busara na inakutaka utumie uzoefu wa yale uliyojifunza au uliyopitia (history yako) halafu uache yale yasiyofaa, uyachukue yale mazuri kisha uyaboreshe na kuyaendeleza.
Kuwepo kijijini au kutokusoma sio kosa la ajabu saana japokuwa haipendezi lakini maisha ni popote - inategemea ww unajichukuliaje na unamtizamo gani kwa wale ambao hawapo hapo ulipo ww. Usiwadharau na wala usijivune na kwaona wao ni watu duni au wamepoteza mwelekeo.
Nyie wa mjini mbona ndo tunasikia vituko kila uchao ilhali mpo mjini na mmesoma? Mbona bado hamjastaarabika?. Huku vijijini mavituko yenu hayo ya huko mjini, huku hayapo au ni nadra sana kuyasikia.
 
Any corporal punishment to humans is evil, sio kwa mtoto wala kwa mtu mzima na haifundishi wala kuinfluence any change of behavior
 
Vitabu vya dini vinasema, mtumwa anapaswa kumheshimu na kumtii mmliki wake, hata kama anamtesa na kumlawiti..; unajua hilo?
Duh! Nilikuwa silijui hilo aisee. Hebu tuwekee hizo aya hapa mkuu tujisomee wenyewe.
 
Any corporal punishment to humans is evil, sio kwa mtoto wala kwa mtu mzima na haifundishi wala kuinfluence any change of behavior
Please, show the references or the appropriate quotations/citations. Ni hayo tu.
 
Zipo. Ila viboko vya madras si mchezo! Shuleni at least kale kaptula ka khaki na wavulana sababu ya utundu na kujiandaa tulikuwa tuna vaa 2!
Madras si mchezo aisee!
Yep. Kazi ya kumwandaa mtoto si mchezo. Usipokuwa makini hapo utajikuta unazalisha na kulea maduwanzi, watu wazima wakorofi wa kila aina.
 
Nadhani pia hako katoto bado kadogo sana ostqz angetafuta namna nyingine
 
Hivi bado mnachapana mboko? Mtoto anaishi yale anayoyashuhudia. Yaani ana adopt. Wa kuchapwa ni mzazi anayeshindwa kumtengenezea mazingira salama mtoto
Kwa mlolongo huo wa logic yako hapa, tutajikuta tunarudi hadi kuyachapa makaburi ya babu zako. Inafaa tuseme hivi: Tubadilike na Tujisahihishe; na mabadiliko hayo yanaanzia na wewe. Kuwa stable na ngangari kwenye suala la malezi ya watoto wako ili kuepuka ule msemo wa "mitoto ya siku hizi ni balaa tupu" haisikii wala haifundishiki.
 
Back
Top Bottom