usipende maisha ya kishamba na kibushiparty uliyokuzwa wewe na watoto wako wakuzwe hivyo. kama haujui, mtoto anayechapwa chapwa huwa anapoteza kwanza uwezo wa kujieleza, na uwezo wa kujiamini. hao ndio wamejaa hata makazini ukimwambia simama hapo mbele jieleze hawezi, na hajiamini, kwa sababu alikuzwa kwa hofu na woga mtupu. na inawezekana wewe ndio mtu wa aina hiyo. don't pass that to your kids please! baki nazo wewe peke yako.
Mkuu, Unayaita maisha waliokulia na kulelewa wazazi wako ni ya kishamba na kibushiparty? Yan walikuwa na maisha hayo halafu wakaweza kukuzaa, kukulea hadi leo umekuwa mtu mzima mwenye akili timamu then unadiriki kuinua kalamu na kuandika kwamba eti hayo yalikuwa ni maisha ya kishamba na kibushiparty? Kweli?
Mimi nadhani kilichokuwa sahihi ni kuyaangalia maisha hayo na kuchota yale yaliyokuwa mambo mazuri, yenye kuboresha na kuheshimisha kizazi cha sasa. Hizo ni Tunu za maisha. Yale unayoona sio sawa uyaache- chukua yale mema na uyaendeleze.
Mtoto, hata mtu mzima hustahili kuadabishwa (ndio haki yake au malipizi yake). Tukumbuke adhabu sio zawadi na lengo la adhabu ni kumfanya mhusika aone, achukie na kutubia kosa lake; tena ajitahidi kwa bidii zote kutokurudia tena kosa alilotenda.
Kutokutoa adhabu kwa mkosaji ni kosa kubwa sana kwani mkosaji huyo ataona ni kawaida tuu atazembea na atarudia-rudia kosa hilo na hatimaye atajenga tabia. Je, hiyo ni sawa?
Kwa mfano mtoto wako wa kike (darasa la 5) anaanza mazoea ya kukutana na wavulana wanampa vizawadi e.g. pipi au fedha faraghani na anawaruhusu wamshike-shike makalio au chuchu(
kama zipo) halafu ww mzazi siku moja unabahatika kumkuta live. Ukimhoji ulikuwa unafanya nn anakujibu "sio kitu". Unarudia swali tena kwa ukali lakini bado anakujibu anakuangali macho makavu "miye sijafanya kitu"
Mara paap! Anatokea mamaake na akiwa bado yu mbali kidogo anakuambia: "mwache huyo mtoto mbona alikuwa anacheza tuu? .....
Dah! hapo ujue siku yako imeshaharibika. Utaendeleaje? Kucheka? Kununa? au kutafuta mwarobaini?
Mwisho: Inakuwaje "wazazi mashabiki" tukio la kawaida kabisa mashuleni linapigwa
vid.clip na linasambazwa mitandaoni kwa maneno mazito eti ni ukatili uliopitiliza ili kuamsha hisia ndani ya Jamii na tena kuamsha hisia za chuki baina ya familia ya mtoto na mwl. aliyetoa adhabu hiyo? Hilo ni kwa lengo Ovu. Kwani kulikuwa na shida au ugumu gani kuripoti tatizo hilo kwenye uongozi wa shule ili kuwezesha kulipatia ufumbuzi at
local level na
under field conditions? Tunakuza jambo dogo kiasi hicho utadhani mtoto amechunwa ngozi hadi kwa Mufti, Polisi na kwa waziri Mh. Dr. D. Gwajima.
Je, mtoto aliyechapwa aliumia/alidhurika kiasi hadi akalazwa Hospitali? Hakuna watoto wengine waliochapwa siku hiyo? Je, madrasa hiyo haina uongozi au msimamizi (
ukimwacha huyo mwl)? Kooote huko "wazazi mashabiki" mmeona hakufai ila ni kumlipua mwl.