Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

IMG_20230410_64360.jpg


ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
 
Ustaarabu (Civilizations) utaanguka lakini haimaanishi mwanadamu ataanguka. Madola mengi ya kale yamepitia hiki ambacho leo hii tunakipitia, hivyo hakuna jipya chini ya jua.

Dola la Rumi hadi lilishawahi kuwa na wafalme mashoga kama saba hivi, likaanguka na maisha bado yanaendelea leo hii. Hivyo kutokea kwa haya mambo, ni hatari wa CIVILIZATION na siyo HUMANITY.
 
Wakumbushe jamii hata wakikengeuka ukweli wawe nao.

Na baadhi ya ndugu wapo pamoja na shetani kuvunja ndoa za ndg/watoto wao. Jamii inaona sawa tu.

Shetani anajifanya kama haoni ila anageuka pembeni na kucheka kwa furaha.
 
Ndo maana wanakuita mzee, akati kijana mdogo.
Ndo km hivi kuwaza kizee zee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hayo mawazo hayachagui rika, sote tutakuwa na familia na ni muhimu kukumbushana
 
Wakumbushe jamii hata wakikengeuka ukweli wawe nao.

Na baadhi ya ndugu wapo pamoja na shetani kuvunja ndoa za ndg/watoto wao. Jamii inaona sawa tu.

Shetani anajifanya kama haoni ila anageuka pembeni na kucheka kwa furaha.
Wengine ukitaka kuwa na ndoa wanakuambia inapoteza muda ni heri ukae pekeyako, hao ni mawakala wa shetani
 
Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho, anguko lake litakuwa kubwa kuliko yale ya wakati uliopita
Nyakati hizi ni za hatari sana, lakini zilikuwepo huko nyuma. Yote uyaonayo ya Homosexuality, Abortions, Transgenderism, Violence and War yalikuwepo katika vipindi vyote vya wanadamu (All the ages of men), na ndiyo vimekuwa vyanzo vikubwa vya madola ya kale kuanguka.

Dola lolote lile huanza kuanguka kutokana na uozo wa ndani (Internal Decadence), manifested in the form of extreme corruption, sexual perversion, hatred towards GOD & The Divine and Lawlessness. Hivyo jamii yetu pia inaelekea kwenye anguko kubwa kama jamii za kale:

  • The Antedeluvian Age ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Post Deluvian Age ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Bronze Age ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Iron Age ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Medieveal Age ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Middle Ages ilianguka kisa uozo wa hivi.​
  • The Capitalist na Information age itaenda kuanguka soon.​


Hivyo dunia haiwezi kuisha, lakini OUR AGE IS AT THE PRECIPICE, na kama maandika yanavyosema. Matthew 24:37 "As it was in the days of Noah, so it will be at the coming of the Son of Man". Haya yote ya sijui USHOGA, KUTOA MIMBA, RUSHWA yalifanywa hata na mataifa ya kale ya ISRAEL NA YUDA, ukisoma kwenye YEREMIA, MAMBO YA NYAKATI na WAFALME. Na ndiyo chanzo kikubwa MUNGU kuwafukuza kikatili Waisraeli pale Middle-East.

Kuna kitabu kinaitwa THE GREAT LEVELER: VIOLENCE AND THE HISTORY OF INEQUALITY FROM THE STONE AGE TO TWENY FIRST CENTURY, kimeandikwa na Walter Scheidel, kinasema kwamba Ustaarabu (Civilizations) huwa zinafika juu na kujisahau hivyo zinaanguka vibaya na kuzaliwa nyingine ambazo zinakuwa hazina hatia na zenye usawa kwa watu wote.
 
Kuoana kimila ina maana kuna utaratibu ulifuatwa, sio kuokotana tu na kisha kuishi pamoja
Zamani watu walikuwa wanaoana makabila ya karibu, sasa hivi Muha wa Kigoma yuko Dar es Salaam amekutana na Mngoni wa Songea na wote na mafukara huo muda wa kufuata taratibu za kimila wanaupata wapi?
 
Nyakati hizi ni za hatari sana, lakini zilikuwepo huko nyuma. Yote uyaonayo ya Homosexuality, Abortions, Transgenderism, Violence and War yalikuwepo katika vipindi vyote vya wanadamu (All the ages of men), na ndiyo vimekuwa vyanzo vikubwa vya madola ya kale kuanguka.
Dola lolote lile huanza kuanguka kutokana na uozo wa ndani (Internal Decadence), manifested in the form of extreme corruption, sexual perversion, hatred towards GOD & The Divine and Lawlessness. Hivyo jamii yetu pia inaelekea kwenye anguko kubwa kama jamii za kale:
  • The Antedeluvian Age ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Post Deluvian Age ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Bronze Age ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Iron Age ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Medieveal Age ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Middle Ages ilianguka kisa uozo wa hivi.
  • The Capitalist na Information age itaenda kuanguka soon.


Hivyo dunia haiwezi kuisha, lakini OUR AGE IS AT THE PRECIPICE, na kama maandika yanavyosema. Matthew 24:37 "As it was in the days of Noah, so it will be at the coming of the Son of Man". Haya yote ya sijui USHOGA, KUTOA MIMBA, RUSHWA yalifanywa hata na mataifa ya kale ya ISRAL NA YUDA, ukisoma kwenye Yeremia, NYAKATI n WAFALME. Na ndiyo chanzo kikubwa MUNGU kuwafukuza Waisraeli pale Middle-East.
Pia kumbuka kwamba Mungu aliweka ahadi kwamba hatoleta gharika au kusambaratisha vizazi kwa maovu yao tena, bali atawasubiri mpaka siku ya hesabu ifike
 
Back
Top Bottom