Kudrive umbali mrefu

Kudrive umbali mrefu

Zarumenda

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2020
Posts
360
Reaction score
482
Kwamara ya kwanza mwisho wa mwez huu nimepanga ksafir umbali mrefu kwakutumia usafir binafsi Dar to Mwanza. Naomba muongozo kipi cha kuzingatia hasa ili kupunguza mazonge njiani hususani issue ya service ya chombo chenyew?
 
1. Hakikisha unafanya service ya engine.
2. Hakikisha unakua na spare tyre.
3. Hakikisha unakua na wheels spaner, Jeki, Pembe tatu, fire extinguisher.
4. Hakikisha gari ina bima na kadi ya ukaguzi.
5. Kutoka Dar to Morogoro jitahidi kua makini sana kwasababu kidogo lami imejisokota na kuna tochi nyingi pia kua makini na magari makubwa yanayo paki karibu na barabara hasa kuanzia Chalinze, Gairo na Dumila.
6. Ukisigea Pandambili to Kibaigwa pale tembea mwendo wa haja wala usiwe na shaka.
7. Kutoka Kibaigwa hadi Chamwino barabara ipo vizuri ila kua makini pale Mtanana karibu na Nako hua kuna Trafic wanaweka kizuizi cha kizushi nabhawaeleweki wale, lakini barabara ipo njema hadi unaingia Dodoma.
 
8. Dodoma kua makini sana maana zile barabara za kutoa Dar road zinaweza zikakuchanganya namna ya kuifikia Singida road.
Ukianza kutoka Dodoma kua makini kidogo maana pale panakuaga na tochi mitaa ya Nala, lakini utawakuta Trafic kabla ya mzani ama baada ya mzani, pale tembea kwa umakini jidogo.
9. Baada ya Nala we nyooka mazima hadi Bahi ingawa maeneno ya hapo kati ukitoka Barazani panakuaga na tochi za ghafla hasa pale ukisha ona alama ama kibao cha don't overtake, na ukisha wapita tu nyooka na 120 hadi Bahi ukiiona tu punguza mwendo uzingatie 50 pale wanakuepo wazee na tochi yao ingawa wanaweleka. Usisahau Bahi kuna bams iliyo changamka na jitahidi kua makini sana.
 
1. Hakikisha unafanya service ya engine.
2. Hakikisha unakua na spare tyre.
3. Hakikisha unakua na wheels spaner, Jeki, Pembe tatu, fire extinguisher.
4. Hakikisha gari ina bima na kadi ya ukaguzi.
5. Kutoka Dar to Morogoro jitahidi kua makini sana kwasababu kidogo lami imejisokota na kuna tochi nyingi pia kua makini na magari makubwa yanayo paki karibu na barabara hasa kuanzia Chalinze, Gairo na Dumila.
6. Ukisigea Pandambili to Kibaigwa pale tembea mwendo wa haja wala usiwe na shaka.
7. Kutoka Kibaigwa hadi Chamwino barabara ipo vizuri ila kua makini pale Mtanana karibu na Nako hua kuna Trafic wanaweka kizuizi cha kizushi nabhawaeleweki wale, lakini barabara ipo njema hadi unaingia Dodoma.

Balikiwa kwakunipa mwangaza
 
10. Kutoka Bahi barabara ni mbaya sana na kuna mashimo korofi kwenye lami, pia kua makini sana na magari makubwa yanapo kwepa mashimo yatakufata upande wako, na baada ya kumaliza hayo mashimo usidanganyike na uzuri wa barabara, endelea kwenye polepole maana mbele kuna blind Conner na bumps ya ghafla na kisha kuna reli na baada ya reli kuna wazee...🤨
11. Ukisha wapita wazee pale unaweza ongeza mwendo ulio changamka hadi utakapo ona kibao cha kuingia Manyoni, pale zingatia sana 50, maana wale wazee ni noma sana kwa amana. Pia Manyoni kuna bumps 2 za kipuuzi sana pale, baada ya kumaliza senta ya Manyoni utakuta na Reli pia kuna wazee pale.
 
Muhimu zaidi, endesha kwa kujilinda. Tii sheria za barabarani.

Upo kwenye safari yako mwenyewe. Usipende ligi za kipuuzi.

Fahami uwezo wa engine yako. Kisha tumia uwezo huo katika uendeshaji wa kiungwana.

Ukijihisi mchovu, simama. Pumzika kisha endelea na safari.
 
Mengi Yameelezwa Hapo Juu Ukifika Manyoni Pitia Itigi Barabara Ni Nzuri Mpaka Tabora. Uwe Makini Sana Sana Buses Zinaanza Safari Usiku Huwa Wana Haraka Hata Sehemu Hatarishi. Unaweza Kusema Aina Ya Gari Unayoitumia Uongezewe Ujuzi
 
Kama ni mara yako ya Kwanza kufanya safari ndefu jikaze kiume maana mziki wa kutoka DAR - MWANZA tunaweza wachache sanaaa..
Jitahidi uanze safari yako usiku kuanzia saa nne Hadi tano kama sio mzoefu wa usiku Toka DAR SAA 10 usiku uanze safari yako
Kama ndo mara ya kwanza namshauri aanze safari saa saba mchana ili angalau saa kumi na Moja kumi na mbili ashavuka moro.Kipande ya dar moro iko na majanga sana Bora kuimaliza mapema.
 
Dar to Mwanza, zaid kidogo ya km 1000.. kama ni mara yako ya kwanza naomba fanya yafuatayo.. ukiacha usalama wa chombo.

1. Pata usingizi wa kutosha kabla ya safari

2. Vunja safari katikati... ni vizuri ukalala Singida

3. Usikubali kwa namna yeyote kushawishiwa kuendesha gari usiku ukiwa umechoka

4. Usikubali ku overtake bila tahadahari ya kutosha.

5. Nenda taratibu, max 100km/hr..

6.Beba carton ya maji makubwa na uyanywe taratibu.

7. Macho kwenye sahani ... angalia taa zote za tahadhari, usikubal hata moja iwake, na ikiwaka paki pembeni kwenye usalama tafuta fundi.

8. Fuata alama za barabarani...

9. Usiendeshe kwa hofu ya maaskari barabarani, wapo kwa usalama wako

10.Mwisho na sio kwa umuhimu, Sali kabla ya safari, Mungu akutangulie.
 
Kama ndo mara ya kwanza namshauri aanze safari saa saba mchana ili angalau saa kumi na Moja kumi na mbili ashavuka moro.Kipande ya dar moro iko na majanga sana Bora kuimaliza mapema.
Ni kweli sio mbaya Kwa muda huo Ila asiwe na mawenge ya kutaka kutunisha msuli na madereva wendawazimu atajikuta anapigwa vyeti vya kutosha.
 
Dar to Mwanza, zaid kidogo ya km 1000.. kama ni mara yako ya kwanza naomba fanya yafuatayo.. ukiacha usalama wa chombo.

1. Pata usingizi wa kutosha kabla ya safari

2. Vunja safari katikati... ni vizuri ukalala Singida

3. Usikubali kwa namna yeyote kushawishiwa kuendesha gari usiku ukiwa umechoka

4. Usikubali ku overtake bila tahadahari ya kutosha.

5. Nenda taratibu, max 100km/hr..

6.Beba carton ya maji makubwa na uyanywe taratibu.

7. Macho kwenye sahani ... angalia taa zote za tahadhari, usikubal hata moja iwake, na ikiwaka paki pembeni kwenye usalama tafuta fundi.

8. Fuata alama za barabarani...

9. Usiendeshe kwa hofu ya maaskari barabarani, wapo kwa usalama wako

10.Mwisho na sio kwa umuhimu, Sali kabla ya safari, Mungu akutangulie.
Max 100 km/h kama atalala singida inatosha Ila kama anataka kutoboa bila Kulala hiyo speed ni ndogo Sana na inachosha..
Safari ndefu kama hiyo huwa nagonga 130 - 170
 
8. Dodoma kua makini sana maana zile barabara za kukutoa Dar road zinaweza zikakuchanganya namna ya kuifikia Singida road.
Ukianza kutoka Dodoma kua makini kidogo maana pale panakuaga na tochi mitaa ya Nala, lakini utawakuta Trafic kabla ya mzani ama baada ya mzani, pale tembea kwa umakini jidogo.
9. Baada ya Nala we nyooka mazima Kibaigwa ingawa maeneno ya hapo kati ukitoka Barazani panakuaga na tochi za ghafla hasa pale ukisha ona alama ama kibao cha don't overtake, na ukisha wapita tu nyooka na 120 hadi Bahi ukiiona tu punguza mwendo uzingatie 50 pale wanakuepo wazee na tochi yao ingawa wanaweleka. Usisahau Bahi kuna bams iliyo changamka na jitahidi kua makini sana.

Dah umetaja nala dodoma nikakumbuka almanusura yule mbwa atuulie kwenye harrier pale kwenye makutano ya barabara yenye traffic light maeneo ya uwanja wa jamhuri pale . Dah
 
Sema kupitia itigi
1. Kutoka Manyoni hadi itigi barabara ni nzuri sana, ingawa kuna bumps kama nne ambazo hazija changamka sana, lakina pia wazee hawapo barabarani hadi unaingia Itigi kabla ama baada ya roundabout.
2. Baada ya Itigi utapita mzani mbele kama 2mkts the unakutana na maliasili kisha roundabout inayo ikataa Njea ya kuekea Mbeya.
3. Kuanzia hapo road ni mkea na hakuna tochi wala mbambamba....... utakipia 120 kama ikikupendeza, then ukikaribia Kigwa kidogo pale hua lami imejisokota kidogo, lia kwa mwendo wa 100 hakuba ubaya hadi unaingia Kigwa.
4. Kuanzia Kigwa tembea kwa tahadhari kama 1kmt utakuta kituo cha wazee, ila hawana baya then tembea na 120 hadi utakapo uona ubao wa kuingia Taborajazz, pale kua makini kidogo maana kuna muembe mkubwa upande wa kulia wazee wanajificha pale, ingawa wanaeleweka hawana baya mkuu.
Kesho nikumbushe niendelee kuanzia Tabora to Mwanza..
 
Back
Top Bottom