Kudrive umbali mrefu

Kudrive umbali mrefu

Dah umetaja nala dodoma nikakumbuka almanusura yule mbwa atuulie kwenye harrier pale kwenye makutano ya barabara yenye traffic light maeneo ya uwanja wa jamhuri pale . Dah
Pole sana mkuu, huyo alikua mgeni wa niia.
Kiukweli pale panachanganya sana waendeshaji wengi
 
Lakini pia kutokea Misigiri hadi Igunga njia inavishimo chokozi sana, na kutoka Igunga hadi Nyandekwa to Ziba kwasasa hapafai kabisa ile barabara
Misigiri shangazi alikuwa anatoa msosi mmoja hatari.. apumzike salama huko alipo aise.. yani apumzike anapo stahili.. ilikuwa bufeee moja la hatari...😅😅 makuku masaki
 
Pole sana mkuu, huyo alikua mgeni wa niia.
Kiukweli pale panachanganya sana waendeshaji wengi
huyo mshenzi ni mwenyeji .Sema siku hiyo alikuwa maji dah. Nikikumbuka yaani. Tulikuwa tukusanywe kwa pamoja chini ya kichanja cha trailer iliyokuwa imebeba container
 
I
Nitaendelea kukupa udambwi udambwi kama utasema unataka kupitia Itigi, Tabora, Isikizya, Nzega to Mwanza..... ama utapitia Ikungi, Singida, Shelui, Ingunga, Nata, Nzega to Mwanza.umemaliza big bro🙏
 
Kwamara ya kwanza mwisho wa mwez huu nimepanga ksafir umbali mrefu kwakutumia usafir binafsi Dar to Mwanza. Naomba muongozo kipi cha kuzingatia hasa ili kupunguza mazonge njiani hususani issue ya service ya chombo chenyew?
Kata vipande ili upumnzike la sivyo tuanze kuandaa R.I.P mapemaaa
 
1. Kama ni mara ya kwanza kuendesha vunja safari hiyo sehemu mbili, kama walivyoshauri lala Singida
2. Overtaking ni chanzo kikubwa sana cha ajali hasa hizi za high way.. kuwa makini sana sana unapotaka kuovertake jiridhishe bila shaka kwamba utapita gari au magari yaliyo mbele yako bila kuleta madhara kwa gari nyingine yeyote. Overtake kwa haraka then rudi kushoto kwenye lane yako. Don't overtake kwa kufuata mkumbo kwamba wa mbele yaka katoka na ww unamfuata nyuma bila kujirishisha, usimake assumption kabisa
3. Kama huna uzoefu wa kuendesha usiku, acha kabisa usiku huwa kuna mambo mengi
4. Fanya service ya nguvu siyo kumwaga tu oil, hakikisha pia miguu ya gari iko vizuri kuanzia tairi, ball joint, cv joints, shock up, brake pads, bearings etc..
5. Mwisho kabisa chenji hela ndogondogo buku mbilimbili tatu tano za hukonga polisi njiani, huwezi fuata hizo 50 zote lazima utaboreka
 
Usikamie safari. Safari yangu ndefu ya kwanza na private ilikuwa Mwanza-Iringa. Nikaikamia. Nilichezea mikeka 6 njiani, overspeeding. Nakumbuka nilispend 120,000 kulipa faini. Achilia mbai zile za kumalizana na wazee kishikaji.
 
Kama ni mara yako ya Kwanza kufanya safari ndefu jikaze kiume maana mziki wa kutoka DAR - MWANZA tunaweza wachache sanaaa..
Jitahidi uanze safari yako usiku kuanzia saa nne Hadi tano kama sio mzoefu wa usiku Toka DAR SAA 10 usiku uanze safari yako

Nahis ntatembea wakati kuna mwanga tu japo kuwa traffic niwengi
 
Back
Top Bottom