Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

toa mfano unaoeleweka sasa alafu unajua Kuna kitu miye huwa nashangaa sana watu wote waodharau walimu ambao wapo secta tofauti na uwalimu wengi wao wazazi wao ni walimu

Yani huu ni utafiti ulio wazi hakuna secta ya utumishi wa umma au nje ya utumishi wa umma ambayo watumishi wake wanaojitahidi na kuhakikisha watoto wao watapata elimu bora kama walimu

Walimu ndio wanaongoza kuwa na watoto madaktari , injinia, wahasibu, mahakimu nk ila ajabu hawa watu wanadharau walimu sasa unajiuliza hivi hiyo kazi ingekuwa ina tatizo mzazi wako aliwezaje kukosomesha

Ukibisha wewe ingia tasisi yoyote sema jamani wale watumishi ambao wazazi wao ni walimu wandike majina hapa Kuna offers ya inakuja utaona asilimia tatu watakuwa watoto wa walimu

Tusidharau walimu jamani wapo vizuri sema wengi wao hawatambui hilo
Hatuwadharau walimu ila kusema idara zote mishahara ifanane kuna uwezekano baadhi ya kazi watu hawataamua kusoma.
Mishahara inakua mikubwa kwa baadhi ya sekta ili kuwapa motisha watu wajiunge zaidi na kada hizo.
Unafikiri ni kwann watu wanaosoma ualimu ni wengi kuliko udaktari?
 
Nadhani Idara zinazofanya kazi day and night (24/7), no weekend no sikukuu, ... wanatakiwa kupewa motisha zaidi. Kwa mfano Idara ya Afya na Majeshi should be given priority.
 
Unadhani inawezekana hivi changamoto za idara ya afya unaifananisha na idara ya elimu?

Ufananisho huu unatumia hoja ipi Mkuuu
Pia wingi wa walimu unawapoza
 
habari wanandugu!

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani Moja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya Wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi Wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu Wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu Wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu. yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti

by mkulima Wa nyanya
Sasa mtalingana vipi kama kuna mwingine ana shahada ila umemkuta kazini miaka kama 6 hivi??
 
Nyie endeleeni kubishania sijui huyu mshahara umefanya kile, sijui yule mshahara hauna lolote..... Kalaga bahooo.
HIVI NI NANI ALIYEWALOGA KUWA WANASIASA WA SASA WATALETA UFUMBUZI?
Mniyaa bahooo..... Mimi nafanya yangu baaasiii
 
Naona kuna watu muda wa kukaa darasanai imekuwa hoja ya kulipwa mishahara wanayolipwa, haaya basi.

Ila mkumbuke kuna watu wanakaa darasanai miezi sita mpaka mwaka mmoja tu na wanawazidi mishahara
 
Sidhani kama tumefikia huko kwenye kupanga mishahara upya!!!!Mishahara hupangwa baada ya kufanyika utafiti siyo uhakiki.Na ndiyo maana kwa kiwango kimoja cha taaluma watu watatofautiana!Mfano,mkufunzi msaidizi wa chuo kikuu ana digrii moja sawa pengine na mwalimu wa sekondari lakini mshahara wa mkufunzi uko juu sana ya ule wa mwalimu wa sekondari.
Ukisema hivyo,mimi niliyechukua digrii ya kufundisha elimu ya awali(Bachelor of Early Childhood Education) unamaanisha ntalipwa kidogo kwasababu nafundisha chekechea,you cant be serious.
 
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.
acha ujinga huyo MMED wa neurology amefundishwa na nani??
 
Kama mapadri nao wangekuwa wanalipwa kama watumishi wengne ndani ya Tanzagiza, kwa kufuata kigezo cha kusoma miaka mingi wangekuwa wanaongoza kwa mishahara
maana miaka 6 darasani sio jambo la sport sport
 
Every Tanzanian deserves a fair shot at a decent wage, and the ability to pursue the jobs they want.
Teachers deserve more than our gratitude, they deserve our full support.

"High-quality early education is one of the best Investment we can make.
 
jamani vitu vingine tuwe tuna uliza wenyeji mwalimu wa ngazi ipi Tanzania analipwa mshahara wa laki mbili mbona mnapenda kuona kama walimu ndio watumishi hohe hahe kwa kila kitu

Hivi mnajua Kuna walimu wanachukua mshahara milioni moja yani hiyo milioni ni yake hapo makato yote yamefanyika

Hivi mnajua katika watumishi wa umma ukiweza tatu bora mwalimu hawezi kukosa kuwa na mshahara mzuri ukitofautisha na idara nyingine

Tatizo walimu wamejaa uchoyo na unafiki ndio maaana wanaoneka hawana kipato wanaogopa kusema wapo vizuri kiuchumi kwakujua wataobwa au kukopwa




Umeharibu vibaya sana mwisho wa post yako inawezekana wewe ni zile sample walizozitumia TWAWEZA
 
Acha ushamba kwani hakuna walimu wenye div1? Usiropoke vitu usivokuwa na maarifa navyo nikweli mwalim halingan na dactar lkn div sio kigezo hii ni dalili ya ulimbukeni
mwalimu wa div 1? km yupo ni one in a million...hakuna asiyejua kwamba bongo mtu anaenda ualimu as a last resort usitake kusema otherwise! labda unazungumzia hiyo crush programe ya udom!
 
mwalimu wa div 1? km yupo ni one in a million...hakuna asiyejua kwamba bongo mtu anaenda ualimu as a last resort usitake kusema otherwise! labda unazungumzia hiyo crush programe ya udom!

Mimi ni one in a million unayosema. Na nimeenda kwa hiari yangu.
Je kuna tatizo ??
 
hakuna wafanyakazi wenye ushiirikiano kama walimu sasa. lakini idara ya afya uchoyoooooo umezidi
 
Back
Top Bottom