Kuelekea maadhimisho ya miaka miwili ya Rais Samia, Tutaje mafanikio ya ndani ya miaka miwili

Kuelekea maadhimisho ya miaka miwili ya Rais Samia, Tutaje mafanikio ya ndani ya miaka miwili

Uti wa Mgongo wa Taifa letu umeimarishwa vyema chini Daktari ni Rais Samia Suluhu aliyeamua kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo.

Wakulima mashambani wamejawa na tumaini baada kuona kilimo kimetengewa bajeti ya kihistoria ya shilingi bilioni 954. Hili ni ongezeko la asilimia 317 ukilinganisha na mwaka uliopita.

Wakulima walipolia na kupaza sauti kuhusu ongezeko la bei ya mbolea duniani, Rais Samia Suluhu Hassan aliwafuta machozi wa kuweka bilioni 150 kama ruzuku ya mbolea kwa wakulima na sasa wakulima wanatumia mbolea hiyo kuongeza uzalishaji wa chakula na kipato.

Wakulima hao waliopewa ruzuku, ndio hao hao wanaonufaika na shilingi bilioni 83 zilizowekwa kuongeza uzalishaji wa Mbegu huku pia taasisi ya Utafiti wa kilimo nchi yaani TARI ikiongezewa kufanya utafiti na uzalishaji wa mbegu bora.

Acha wakulima walime, sababu sasa masoko ya mazao yameimarika, Wafanyabiashara wa mazao ya Tanzania wananufaika.

Kupitia jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu kufungua nchi na kutafuta masoko, Parachichi toka Njombe Lidunda kwenye Supermarket za China, Ulaya na Afrika Kusini, soko la Korosho za Mtwara limeimarika Marekani na pande nyingine za dunia. Iko hivyo kwa mazao mengine pia.

Hesabu kali zinapigwa na kutengewa bajeti ili tupunguze utemezi hali ya hewa, Serikali inaongeza eneo la umwagiliaji malengo yakiwa kwamba nusu ya eneo linalolimwa nchini litumike kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji ifikapo 2030. Hii itaongeza uzalishaji, ajira zaidi ya milioni 3 zitatengenezwa kwa wanawake na vijana kwenye kilimo ifikapo 2025

Nyota njema imeonekana kwenye kilimo, mwanga unaonekana, watumishi ambao wameajiriwa katika sekta hii wamewezeshwa zaidi, mwaka huu maaafisa ugani kilimo zaidi ya 7,000 nchi nzima walikabidhiwa vifaa vitakavyowawezesha katika kuongeza ufanisi kwa faida ya kilimo.

Asante miaka miwili ya kilimo, Asante Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wakulima na kuwaongezea kipato huku usalama wa chakula nchini ukiimarika.

2-13-scaled.jpg
 
Wafanyabiashara wa eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam, wamekiri moja ya mambo yaliowafurahisha kwenye miaka miwili ya Rais Samia Suluhu ni jinsi alivyowapigania kuhakikisha wanabaki kwenye maeneo yao ya kufanya biashara.

Lakini pia Mama amefanya maendeleo mengi tu katika kuboresha miundombinu, elimu, afya, umeme, Maji nk;
Miaka miwili ya Mama ni Neema kwa watanzania

 
Na kweli ni neema km mchele tu kilo 3500 maharage 4000 kilo unga wa sembe kilo 2000 sasa ww huoni neema hiyo..wasiompenda wana wivu tu[emoji2962][emoji2962][emoji41]
 
Back
Top Bottom