Sio Simba hii. Nikikumbuka Galaxy walivyofanya, imani inanitoka kabisa.
Wachezaji wetu wa Simba wa sasa waliunajisi uwanja wa Mkapa kwa kuruhusu kufungwa bao tatu na kutupwa nje ya CCL
Kabda ya hapo Watanzania tulijua na wapinzani wetu kutoka nje ya nchi nao walijua kua Kwa Mkapa mbele ya Lunyasi SSC haponi mtu
Kocha wa Ahly Mosimane katika hafla ya kupanga draw ya CCL alisema anafarijika maana this time hawatakwenda kwa Tanzania(kucheza na Simba kwa Mkapa)
Hebu vijana wetu wauchukulie serious mchezo huu. Asec Mimosas hatujawahi kuwafunga ndani wala nje na kumbukumbu ya Sekou Bamba bado tunayo alivyotuua pale Shamba la Bibi. Ila siku zimebadikika na lolote linawezkana. Tukapambane