Kuelekea Mei Mosi 2022: Rais Samia, Waokoe Watumishi wako Dhidi ya Dhulma Kali ya Makato ya Lazima ya Mshahara kutoka kwa Vyama vya Wafanyakazi

MoseKing

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2017
Posts
4,928
Reaction score
8,976
Ni ukweli ulio wazi kwamba sisi kama Watumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunapitia kipindi kigumu hasa kiuchumi na Cha muda mrefu sasa.

Licha ya changamoto nyingi ambazo Watumishi wamekuwa wakipitia, hali iliyopelekea Watumishi kuamua kuwa pamoja katika vyama kwaajili ya kupambania maslahi yao, leo vyama hivi vimegeuka "Janga Jipya" la kuwumiza Watumishi kiuchumi. Inasikitisha sana!

Rais wetu Mpendwa, tunajua unatupenda Watumishi wako na unatufikiria kwa mema lakini huku kwetu, Kuna mzimu ambao hata kama ikitokea ukaongeza chochote siku ya Mei Mosi hakitasaidia sana, maana tayari Kuna Mzimu wa Vyama vya wafanyakazi Tanzania ambassador hukata 2% ya mshahara wa mfanyakazi kwa LAZIMA" kwa jina la Ada ya UWAKALA.

Hii Ada ya UWAKALA imekuwa Ni tatizo kubwa mnoo, kiasi kwamba sasa hivi Hakuna tofauti ya Mwanachama rasmi wa chama Cha wafanyakazi na asiye Mwanachama.

Mheshimiwa Rais, Watumishi wako unaowaamini hasa Wakurugenzi ( DEDs ) wamekuwa sehemu ya mchezo huu kwasababu wengi wao ni wanufaika wa mchezo huu.

Sasa hivi imegeuka trends kwa baadhi ya Watumishi kuanzia vyama vya wafanyakazi, na kuanza kukata mishahara ya Watumishi kwa jina la ADA YA UWAKALA hasa wale wasio wanachama. Ada hii hukatwa 2%.

Inaumiza sana kuona Watumishi wanaumizwa na watu ambao walitemea watakuwa msaada kwao.

Mheshimiwa Rais, kwa mfano ukitaka kunua shida za Watumishi unawasikiliza Hawa vyama vya wafanyakazi, Maumivu anayopewa huyu mtumishi na hivi vyama vya wafanyakazi utasikia wapi ?

Katika hili, Mheshimiwa Rais tunakuomba kuelekea Mei
uliangalie suala hili kwa jicho HURUMA.

1) Sheria ya ajira na mahusiano kazini (2004) ifanyiwe marekebisho na Ada ya UWAKALA ifutwe au iwe kiwango kimoja ( Flat rate ).

2) Vyama vya wafanyakazi visikate mishahara ya Watumishi kwa LAZIMA kwa namna yoyote wale ambao siyo wanachama wao.

Ni matumaini ya Watumishi kiwa utasikia kilio Hiki maana wewe Ni Rais Msikivu.

Nalisema hili kwasababu Mei Mosi huandaliwa na TUCTA ambao ndio wanufaika na Wakandamizaji wa Watumishi, hivyo inakuwa Ni ngumu Watumishi kusema wakasikika.

Asante.
 
Vyama vya wafanyakazi ni allies wa ccm... Itakuwa ngumu sana!

Wazo huru: Zungumzia vile vile mafao na PAYE!
Kama vyama vya upinzani vinatafuta haki zao kupitia mazungumzo na CCM.

Hata Watumishi wanastahili kupita njia hiyo, maana vyama vya wafanyakazi sasa hivi havimsaidii tena mtumishi.

Na kibaya zaidi, vimeteka USEMAJI kwahiyo Mtumishi Hana sehemu ya kusemea.

Na hata kama Rais akiongeza mishahara, haitasaidia sana maana hivi vyama vinakata Makato kwa njia ya Asilimia, maana yake mshahara wako ukiongezeka na wao wanaongeza Makato.
 
Ni vizuri hotuba ya mwaka huu ikawa fupi sana,yenye kutimiza ahadi aliyoitoa mwaka jana.Asitumie mda mwingi yeye,bali watumishi washerehekee.

Miaka saba bila nyongeza si mchezo!
Kumbuka vyama vya wafanyakazi hukata kwa asilimia.

Kwahiyo hata ukiongezwa mshahara, na vyama vya wafanyakazi na wao wanaongeza Makato.

Kwahiyo, utajikuta Hakuna Cha maana utakachopata.

Suala hili linapaswa kuwa HIARI.

1) Sheria ya ajira na mahusiano kazini ifanyiwe marekebisho, ili Ada ya UWAKALA ifutwe au iwekwe kiwango ambacho Ni FLAT RATE, isiwe Asilimia.

2) Watumishi wawe na hiari ya kujiunga na vyama wanavyivipenda na kuridhia Makato kwenye mishahara yao.
 
Reactions: F4B
Kuea mwanachama wa Vyama vya Wafanyakazi ni HIYARI sio lazima.

Kama ukiona havina nafasi katika ajira yako unaweza kujitoa na ukawa HURU.

Ukumbuke hivi vyama vimeingia kwenye siasa na kujiondoa kwenye falsafa ya kumtetea mfanyakazi na vimekuwa kama daraja la kuingia kwenye siasa.

Sioni kama kuna chama kinachoweza kujitanabahisha kwamba kimetetea maslahi ya mfanyakazi mnyonge, HAKUNA.

Unachangia kila mwezi na mwisho wa mwaka unaambulia Tshirt na kofia! Makato yenyewe ni makubwa na hayaakisi michango wanayokata!

Hawa wamekuwa ni wanyonyaji na wala sio watetezi wa wanyonge.
 
Kujiunga kwa mfanyakazi kwenye vyana vya wafanyakazi iwe ni ihari na si lazima.
Hilo siyo TATIZO.

Tatizo Ni kwamba uwe umejiunga au hukujiunga UTAKATWA 2% ya Mshahara wako, kwenda kwenye vyama vya wafanyakazi.

Hii 2% inaitwa Ada ya UWAKALA ( Agency fees) kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ( 2004).
 
Hilo siyo TATIZO.

Tatizo Ni kwamba uwe umejiunga au hukujiunga UTAKATWA 2% ya Mshahara wako, kwenda kwenye vyama vya wafanyakazi.

Hii 2% inaitwa Ada ya UWAKALA ( Agency fees) kwa mujibu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini ( 2004).

Na hapa nazungumzia zaidi kuhusu Makato na siyo kuwa Mwanachama au la.
 
Kama kweli ni hivyo hilo ni tatizo ila hiyo Agency Fee iachukuliwa na nani?
 
Hii sio ada ya uwakala, ni kodi! Haiwezekan uwakate unao wawakilisha kwa viwango tofauti kwa kazi ileile ya uwakala.. watumishi nchi hii tunaonekana mabwege
Of course, hili Ni tatizo kubwa mnoo.

Na litaendelea kuwa tatizo kubwa kama litabaki kuwa kama lilivyo sasa hivi.

Maana hata kama mishahara ikiongezwa, inaweza isisaidie maana na wao wanaongeza Makato.
 
Hataweza kuongeza mishahara kama alivyoahidi maana hazina inavuja atakuja na sababu zingine mtabaki macho wazi
 
MIAKA 7 hata huruma hawana. Hatuna tena CCM.
 
Umesahau makato ya chama cha walimu , CWT? Mnyonyaji mkubwa wa walimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…