MoseKing
JF-Expert Member
- Jul 5, 2017
- 4,928
- 8,976
Ni ukweli ulio wazi kwamba sisi kama Watumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunapitia kipindi kigumu hasa kiuchumi na Cha muda mrefu sasa.
Licha ya changamoto nyingi ambazo Watumishi wamekuwa wakipitia, hali iliyopelekea Watumishi kuamua kuwa pamoja katika vyama kwaajili ya kupambania maslahi yao, leo vyama hivi vimegeuka "Janga Jipya" la kuwumiza Watumishi kiuchumi. Inasikitisha sana!
Rais wetu Mpendwa, tunajua unatupenda Watumishi wako na unatufikiria kwa mema lakini huku kwetu, Kuna mzimu ambao hata kama ikitokea ukaongeza chochote siku ya Mei Mosi hakitasaidia sana, maana tayari Kuna Mzimu wa Vyama vya wafanyakazi Tanzania ambassador hukata 2% ya mshahara wa mfanyakazi kwa LAZIMA" kwa jina la Ada ya UWAKALA.
Hii Ada ya UWAKALA imekuwa Ni tatizo kubwa mnoo, kiasi kwamba sasa hivi Hakuna tofauti ya Mwanachama rasmi wa chama Cha wafanyakazi na asiye Mwanachama.
Mheshimiwa Rais, Watumishi wako unaowaamini hasa Wakurugenzi ( DEDs ) wamekuwa sehemu ya mchezo huu kwasababu wengi wao ni wanufaika wa mchezo huu.
Sasa hivi imegeuka trends kwa baadhi ya Watumishi kuanzia vyama vya wafanyakazi, na kuanza kukata mishahara ya Watumishi kwa jina la ADA YA UWAKALA hasa wale wasio wanachama. Ada hii hukatwa 2%.
Inaumiza sana kuona Watumishi wanaumizwa na watu ambao walitemea watakuwa msaada kwao.
Mheshimiwa Rais, kwa mfano ukitaka kunua shida za Watumishi unawasikiliza Hawa vyama vya wafanyakazi, Maumivu anayopewa huyu mtumishi na hivi vyama vya wafanyakazi utasikia wapi ?
Katika hili, Mheshimiwa Rais tunakuomba kuelekea Mei
uliangalie suala hili kwa jicho HURUMA.
1) Sheria ya ajira na mahusiano kazini (2004) ifanyiwe marekebisho na Ada ya UWAKALA ifutwe au iwe kiwango kimoja ( Flat rate ).
2) Vyama vya wafanyakazi visikate mishahara ya Watumishi kwa LAZIMA kwa namna yoyote wale ambao siyo wanachama wao.
Ni matumaini ya Watumishi kiwa utasikia kilio Hiki maana wewe Ni Rais Msikivu.
Nalisema hili kwasababu Mei Mosi huandaliwa na TUCTA ambao ndio wanufaika na Wakandamizaji wa Watumishi, hivyo inakuwa Ni ngumu Watumishi kusema wakasikika.
Asante.