Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Labda mm sijaelewa mtu anataka kuhamia kwenye chama mnongea naye nn maana kama mnafanya naye makubaliano maana yake nikama mnaingia naye mikataba na sio hiyari yake kuhamia ccm kunakitu anakitaka

mkataba ni hiyari sema at a price.
 
Kwa kasi hii ya Magufuli hamna haja ya kukaa kwa vipinzani uchwara.



Upinzani Leo ndio watetezi wakubwa Wa majizi na Mafisadi ,sasa unabaki huko kutafuta nini??
Nizamu yetu sisi wapinzani kutetea, mbona ninyi ccm mmetetesa wezi kwa miaka yote, kumbe mkuki kwa nguruwe,............
 
Imekaa vizuri. Hatuwezi kubaki na upinzani ambao siku zote unatetea mafisadi. Kwa mwenye akili timamu kabisa hawezi kubeza kazi nzuri anayoifanya mheshimiwa rais Magufuli kwa sasa.
 
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajia kufanyika tarehe 23th July 2016 mjini Dodoma, tayari zipo taarifa za kuaminika juu ya Viongozi wakubwa wa Vyama vya Upinzani kuazimia kujiunga na CCM katika siku hiyo.

Taarifa iliyotufikia inamtaja Mbunge mmoja maarufu wa CHADEMA ambae mpaka jana alikuwa anamaliza mazungumzo ya mwisho na viongozi waandamizi wa CCM juu ya utaratibu wa mapokezi yake na hatma yake kisiasa.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Pia yupo Mgombea Uenyekiti wa BAVICHA na mgombea Ubunge wa Moja ya Majimbo ya Kaskazini. Pamoja nao yupo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, pamoja na Makatibu kadhaa wa Mikoa wa Chama cha ACT.

Ukiachilia mbali Viongozi hao wa wapinzani ambao idadi yao kwa ujumla inakaribia 18, wapo waliokuwa wa CCM na wakahama na kumfuata LOWASSA upinzani, Viongozi hao nao wameendelea kubembeleza ili waweze kupokelewa tena ndani ya CCM. Watatu kati yao tayari wako Dodoma wakiongozwa na aliyekuwa "Mtoto na Msiri" wa Lowassa ambae pia alikuwa ni KATIBU wa CCM Wilaya ya Monduli.

Wakati Viongozi hao wakijiandaa kujiunga na CCM, maandalizi ya Mkutano Mkuu yameendelea kukamilika na kufikia hatua nzuri, ambapo jana Katibu Mkuu wa CCM alikagua hatua ya maandalizi na kujiridhisha kuwa Mkutano Mkuu utakuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo kwa sehemu kubwa.

Kungekuwa na ukweli naona ungebolda jina la huyo Mbunge.Mpe hongera zake.
 
Hii taarifa ni ya uzushi hakuna *upuuzi* kama huo kipi kiliwaondoa na kipi kinawarudisha
 
Labda mm sijaelewa mtu anataka kuhamia kwenye chama mnongea naye nn maana kama mnafanya naye makubaliano maana yake nikama mnaingia naye mikataba na sio hiyari yake kuhamia ccm kunakitu anakitaka


Kama mwanaCCM mwaminifu nitashangaa, "kuongea'' kuongea nae nini?
 
Wakati ccm wakitalajia kuwapokea hao 18 tarehe 23/7 ....tarehe 25 upinzani utapokea vigogo kutoka ccm 180 ...hii inaitwa kampa , kampa tena ...
Bado unaamini wale wenyeviti wa mikoa na Wilaya takriban 60 waliotangazwa na Mbowe wakati akimkaribisha EL bado wako njiani eeh?
 
Siku hizi kuhamia chama mpaka ufanye mazungumzo kama vile klabu za ulaya zinavyonunua wachezaji. Zamani kujiunga na chama ilikuwa lazima usome miezi 3 ndipo ukabidhiwe kadi
 
Bado unaamini wale wenyeviti wa mikoa na Wilaya takriban 60 waliotangazwa na Mbowe wakati akimkaribisha EL bado wako njiani eeh?
Mbona walisha kuja, au ww hauna taarifa ? sasa subiri hiyo tarehe 25 uone mafuriko ya watu wanavyovua gamba na kuvaa gwanda....teh teh teh teh ...nahv kunakosa kosa zinaendelea dhidi ya ninyi kwa ninyi ...ss yetu macho mkuu...lkn maandalizi kwetu yamekamilika tunasubiri tu muda
 
Kumbe ni biashara!
Haya ccm mkifika bei mtujuze mmewasajili kwa kiasi gani na kodi ni kiasi
 
Back
Top Bottom