Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Nisingependa kuona Upinzani unakufa kabisa TZ yetu hivyo ningependekeza CCM isimamishe, na isichukuwe tena wahamiaji wanaotoka Upinzani hasa chadema, kwani huku kutapelekea chadema &Co. kufa na hii siyo ishara nzuri kwani tunahitaji Upinzani Tanzania hata kama chadema ni wasanii lkn bado tunahitaji upinzania nawaelewa wanachadema ambao wanamkubali na Raisi Magufuli(PhD) na kwamba hawaoni matumaini chadema lkn pia naomba waelewe kwamba kuondoka kwao chadema kutakiua chadema na binafsi nisingependa hilo kutokea!!
 
Acha kutumia hisia kuandika
Jitahd kutumia fikra japo 0.5 ya akili zako
Usiwe mjinga kias hicho
 
Tandale One unaleta tetesi ! Wewe si ni chanzo cha kuaminika ? Mashaka matupu !.
 
Kwa kasi hii ya Magufuli hamna haja ya kukaa kwa vipinzani uchwara.

Upinzani Leo ndio watetezi wakubwa Wa majizi na Mafisadi ,sasa unabaki huko kutafuta nini??

Nadhani mahakama ungewapa ushahidi ungelisaidia zaidi taifa
 
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajia kufanyika tarehe 23th July 2016 mjini Dodoma, tayari zipo taarifa za kuaminika juu ya Viongozi wakubwa wa Vyama vya Upinzani kuazimia kujiunga na CCM katika siku hiyo.

Taarifa iliyotufikia inamtaja Mbunge mmoja maarufu wa CHADEMA ambae mpaka jana alikuwa anamaliza mazungumzo ya mwisho na viongozi waandamizi wa CCM juu ya utaratibu wa mapokezi yake na hatma yake kisiasa.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Pia yupo Mgombea Uenyekiti wa BAVICHA na mgombea Ubunge wa Moja ya Majimbo ya Kaskazini. Pamoja nao yupo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, pamoja na Makatibu kadhaa wa Mikoa wa Chama cha ACT.

Ukiachilia mbali Viongozi hao wa wapinzani ambao idadi yao kwa ujumla inakaribia 18, wapo waliokuwa wa CCM na wakahama na kumfuata LOWASSA upinzani, Viongozi hao nao wameendelea kubembeleza ili waweze kupokelewa tena ndani ya CCM. Watatu kati yao tayari wako Dodoma wakiongozwa na aliyekuwa "Mtoto na Msiri" wa Lowassa ambae pia alikuwa ni KATIBU wa CCM Wilaya ya Monduli.

Wakati Viongozi hao wakijiandaa kujiunga na CCM, maandalizi ya Mkutano Mkuu yameendelea kukamilika na kufikia hatua nzuri, ambapo jana Katibu Mkuu wa CCM alikagua hatua ya maandalizi na kujiridhisha kuwa Mkutano Mkuu utakuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo kwa sehemu kubwa.
Sasa mbunge akiondoka nani anakuwa kapata hasara? pia kumbuka wanaondoka watu sio chama, kwanza mbunge si kiongozi ni mwakilishi hata angekuwa kiongozi kufa kwa Imamu si mwisho wa ibada
 
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajia kufanyika tarehe 23th July 2016 mjini Dodoma, tayari zipo taarifa za kuaminika juu ya Viongozi wakubwa wa Vyama vya Upinzani kuazimia kujiunga na CCM katika siku hiyo.

Taarifa iliyotufikia inamtaja Mbunge mmoja maarufu wa CHADEMA ambae mpaka jana alikuwa anamaliza mazungumzo ya mwisho na viongozi waandamizi wa CCM juu ya utaratibu wa mapokezi yake na hatma yake kisiasa.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Pia yupo Mgombea Uenyekiti wa BAVICHA na mgombea Ubunge wa Moja ya Majimbo ya Kaskazini. Pamoja nao yupo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, pamoja na Makatibu kadhaa wa Mikoa wa Chama cha ACT.

Ukiachilia mbali Viongozi hao wa wapinzani ambao idadi yao kwa ujumla inakaribia 18, wapo waliokuwa wa CCM na wakahama na kumfuata LOWASSA upinzani, Viongozi hao nao wameendelea kubembeleza ili waweze kupokelewa tena ndani ya CCM. Watatu kati yao tayari wako Dodoma wakiongozwa na aliyekuwa "Mtoto na Msiri" wa Lowassa ambae pia alikuwa ni KATIBU wa CCM Wilaya ya Monduli.

Wakati Viongozi hao wakijiandaa kujiunga na CCM, maandalizi ya Mkutano Mkuu yameendelea kukamilika na kufikia hatua nzuri, ambapo jana Katibu Mkuu wa CCM alikagua hatua ya maandalizi na kujiridhisha kuwa Mkutano Mkuu utakuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo kwa sehemu kubwa.
Naona Rutha Makeke anarudi kwa JPM
 
Mnyikaaaa
Habari za hivi Punde zilizonifikia Dawati langu la taarifa kutokea Arusha zinasema Naibu katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) John Mnyika leo akisaidiwa na Mwanasheria wa CHADEMA John Malya wamefungua Kesi kwenye Mahakama ya Afrika Mashariki kuhusu Unyanyasaji wa Bunge la Tanzania kwa wapinzani na Kuzuia Mikutano ya Kisiasa kinyume na Katiba
 
Huu ni uongo una uzushi! Tetesi halafu uthibitisha mmana ake nini? Hivi unafikiri JJ Mnyika hata kama kuna mambo hayafurahii Chadema unafikiri anapelekwa na bongo za CCM?

Kamanda huu mchezo hauhitaji hasira. Kamanda Mnyika hajatajwa popote
 
Waende kwa dicteta uchwara waoga wakubwa.
Dicteta atawahonga ukurugenzi labda. Wengine watalipwa kwa ukuwadi kwa mirupo has a yule wa mjengoni aka the skimmer

Kamanda vipi? Kamanda unatakiwa upambane siyo kulalamika
 
Safi sana kampa kampa tena magamba yameshanganyikiwa huko dodoma bundi ameshatua
Tatizo kubwa ninaloliogopa kampa kampa kuna watakaofaidika nacwatakaopoteza. Watakaokimbia ccm watakua wezi na waliotegemea mteremko nitafurahi kuona hao 187 wa kwenda opposite side ni wasafi na siyo makapi
 
Huu ni uongo una uzushi! Tetesi halafu uthibitisha mmana ake nini? Hivi unafikiri JJ Mnyika hata kama kuna mambo hayafurahii Chadema unafikiri anapelekwa na bongo za CCM?
Hakuna sehemu ametajwa Mnyika, unaweza kututhibitishia Kuwa anayezungumzwa hapa ni Mnyika.?
 
loh! nilikuwa najiandaa kesho nichukue kadi ya sisihem sasa basi!! kwa hicho kilichoandikwa hapo juu, schukui kadi tena! kumbe inatakiwa uongee nao kwanza juu ya hatima yako!!! Mhesh. JPM anayo kazi!!! watu bado hawataki kuachana na mind set zileee!
nakaa pembeni nishuhudie m/ kiti mpya atakavyowatumbua!!!
 
Kwa hisani ya Ezekiel Kamwaga
image.jpeg

Ni nani huyu Mgana Izumbe Msindai?

Msindai ni mmoja wa wanasiasa waliohama CCM baada ya chama hicho kukata jina la Edward Lowassa kwenye kinyang'anyiro cha urais kupitia chama hicho mwaka jana.

Ni mmoja wa wanasiasa waandamizi hapa nchini, akiwa amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki na baadaye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.

Kuna wakati Msindai ndiye aliyekuwa mwanasiasa mwenye ushawishi zaidi mkoani kwake na haikuwa ajabu wakati Wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Tanzania walipomfanya kuwa Mwenyekiti wao baadaye.

Wakati akiwa mbunge; Msindai alipewa jina la utani la "CRDB Benki inayomjali Mteja" kutokana na tabia yake ya kutatua matatizo ya wananchi wa jimbo lake kwa kutumia fedha zake za mfukoni.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Msindai alikuwa miongoni mwa wana CCM waliojitambulisha hadharani kama wafuasi wa Lowassa.

Yeye, Hamisi Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na John Guninita; pengine ndiyo waliokuwa wana CCM ambao hawakuficha mapenzi yao kwa Lowassa; sirini na hadharani.

Kwa waliofahamu maisha yake ya kisiasa, ilikuwa vigumu kuamini angefiti vipi katika maisha ya upinzani.

Kuondoka kwake hakuwezi kuchukuliwa kama pigo kubwa kwa CHADEMA... Hakuwa na nafasi yoyote ya mamlaka ndani ya chama hicho.

================================== ===================================
KAULI YA OLE SENDEKA JUU YA KUHAMA KWA MSINDAI:

SENDEKA: Kuna mtikisiko utatokea

" Kwa sasa sikanushi wala kukubali kwamba Mgana Msindai anarejea CCM. Ila ninachoweza kukwambia kwa uhakika ni kwamba kuna watu watahamia CCM hivi karibuni.

" Kuna mtikisiko utatokea muda si mrefu kutoka leo".

Haya ni maelezo ya Christopher ole Sendeka, Msemaji wa CCM baada ya gazeti la Raia Mwema kuibua stori kuhusu Mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki, Mgana Izumbe Msindai kurejea CCM akitokea Chadema.

Juhudi za kumpata Mgana zinaendelea.
 
Wanasiasa kama hawa inabidi uwaonee huruma tu....

Ila CHADEMA walimbwela sana.... Sijui walipatwa na nini hawa jamaa
 
Back
Top Bottom