Kiukweli binafsi naamini ndiyo siku ambayo itakuwa ya kihistoria katika Taifa langu la Tanganyika.
Naamini pia mabadiliko makubwa yatatokea. Sasa Kuna inshu lazima kuwaonea hofu wananchi ambao watajitolea kupambania haki zetu kutoka kwa mafisadi wa nchi hii.
Kama tunavyoelewa asilimia kubwa ya watanzani ni waoga kwa kuendekeza ujinga kwa watawala. Tunaogopa kudai haki zetu hata kama tunayo haki ya kufanya hivyo.
Hii yote inatokana na hofu ya kesho juu kitumbua changu. Kwani ukiangalia uwezo wa kulipia mwanasheria ndiyo changamoto.
Lakini kama itatokea wanasheria watajitolea pindi mambo yakiwa tofauti, basi naamini watu watakao jitokeza nahisi hakuna watakaoweza kuwazui pia nahisi historian itaandikwa siku hiyo.
Tunahitaji wanasheria watuunge mkono aswa wakina Madereka, kibatara, mwambu..,na aswa zaidi mawakili wa kesi ya ugaidi ya mbowe na mawakili walio jitokeza kuwatetea wakina dr.slaa na kina mdude kule mbeya.
Hii itatufanya kuwa na Imani na hali ya ujasili kuweza kupambania haki yetu dhidi ya wanyang'anyi walioteyali kufanya lolote pale wanapoona mirija yao ya ufisadi inaenda kukatwa.
Tulio wengi humu wengine ni maasikari, watumishi waaminifu kwa serikali ya CCM tunasindwa kuwa upande wa raia moja kwa moja kutokana na kuhofia kupoteza haki yangu ya kuishi Mimi ama wanao nitegemea.
Yote kwa yote tunaunga mkono nguvu ya umma.