Mdau Mkulima,element ya Uislam unaionaje katika hii saga?Hicho chama cha Wachaga na wakwe zao. Zitto mtu wa bara huko hawawezi kumruhusu aongoze hicho chama.
Wangwe alijitahidi lakini akaishia kufa.
Pole sana Zitto; ndio siasa za TZ hizo.
Mdau Mkulima,element ya Uislam unaionaje katika hii saga?
Nashindwa kuilewa misimamo ya Zitto! Siku si nyingi alikuja hapa ukumbini akizungumzia kustaafu siasa ili aweze kutumikia profession aliyoisomea, mara anagombea uenyekiti wa Taifa Chadema, sasa amejitoa sijui atakuja na lipi?
Nimekupata Mkuu.Mimi ni Athiest na hayo mambo yenu ya dini ni mbalimbali kabisa. Tatizo hapa ni ukabila kuliko udini.
Angalia kule Kilimanjaro yaani viongozi wote wa CHADEMA ni kabila moja, kulikoni? Kuna makabila mengine mengi na wengi Wakristo lakini kupita kule itakuwa ni taabu.
Pia katika Wachaga kuna Waislam wengi sana na hawabaguani kwa dini ila ukiwa kule unagundua kabisa dharau ya Wachaga dhidi ya makabila mengine.
Mzee Mtei amejidhalilisha kuingia kwenye kulinda maslahi ya mkwewe.
Zitto ataweza?
Maswali Magumu
Ansbert Ngurumo
[source tanzania daima jumapili]
Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.
Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.
Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.
Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.
Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyang'anyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.
Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.
Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.
Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...
Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.
Katika hili, mmechemsha!

Kuna vijana kadhaa ndani ya CHADEMA walikuwa wamekomalia kuhakikisha Zitto haendi mbele, imenisikitisha sana. Na tuna nakala ya kila kilichoongeleka katika kikao cha jioni ya leo, baada ya kusikiliza mara kadhaa nimejikuta nakosa imani KABISA! Lakini, muda bado unaruhusu.... Mruhusuni Zitto agombee nafasi ya uenyekiti, acha unyanyasaji kwa kisingizio cha ujana!
Yawezekana kugombea kwake kama angeshindwa kungesababisha 'Anguko lake' ambalo nadhani si 'Anguko la CHADEMA' kama ilivyokwishatabiriwa... Niwahakikishie kuwa kwa kumlazimisha aondoe jina ni kupelekea Anguko la CHADEMA.
Napata wasiwasi ndiyo sababu iliyomfanya Kubenea kuamua kuingia ulingoni kwa kupitia CCM, hajaona 'difference'.
yaani mbowe anagombamnia peke yake,mtu kachukua form anaitwa kuhojiwa kwa nini umechukuwa form,lol hapa pananitisha ile mbaya,tunakataa ya ccm sasa yanakuja chadema. kweli ndio chama hiki kipo tayari kuchukua khatamu? naomba jawabu wakuu?
CHADEMA: Chama Cha DEMOKRSASIA na MAENDELEO
Huu ndiyo msingi mama wa Chama kama wanataka waeleweke ni chama cha namna hiyo. Kabla hawajafanya maamuzi yote kwa kivuli cha UMOJA wa CHAMA wakumbuke CHADEMA inasimamia nini ukiondoa individuals. I hope CHADEMA wanataka kujenga TAASISI huru na si UFALME.
Then kama ni hivyo wajiulize: DEMOKRASIA YA KWELI NI NINI?
Na MAENDELEO YA KWELI NI NINI?
Then si vibaya kujifunza kutoka USA ilikuwaje The CLINTONS magiant wa Chama wakapambana na The OBAMAS na je kwa kufanya hivyo walikigawa chama?