Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Si zamani sana tuliwashuhudia Chadema wakimsulubu Chacha Wangwe (RIP) kwa kutoa maoni tofauti na yale ya wazee wa chama. Leo hii tukafikiri watu walewale watakuwa na busara kuacha demokrasi ichukue mkondo wake lakini naona hawajabadilika.

Tukumbuke wote hawa wametoke CCM na walilelewa huko huko hadi wakafikia hapo walipo.
 
Something is seriously wrong somewhere.

kama ni kweli Zitto alichukua na kurudisha form kama 'mgombea binafsi' kama anavosema Ngurumo, ninapata shaka sana na mshikamano let alone collective responsibility ndani ya CHADEMA.

Hili bado lina kawingu flani hivi, kwa nini aliamua (Zitto) kufanya hivo, i.e kugombea kwa namna alivofanya? Nadhani hili linahitaji ufafanuzi wa kina ili kuniondolea wasi wasi ambao umeanza kujijenga dhidi ya nia yake hasa ya kugombea uenyekiti.
 
Hicho chama cha Wachaga na wakwe zao. Zitto mtu wa bara huko hawawezi kumruhusu aongoze hicho chama.

Wangwe alijitahidi lakini akaishia kufa.

Pole sana Zitto; ndio siasa za TZ hizo.
Mdau Mkulima,element ya Uislam unaionaje katika hii saga?
 
Pole sana Zitto; hilo lichama lina wenyewe. Wewe tumika tu kama kiongozi wa chini lakini kwenye nafasi za juu lazima uwe mchaga au uoe uchagani.

Wangwe alipigana na mambo hayo hayo akaishia kufa; wakasingizia ni CCM imemuua.

Mimi nashauri Zitto usikubali kuacha kugombea. Tunataka mabadiliko sio hawa wasanaii ambao ngoma ni ile ile, wimbo ni ule ule isipokuwa wamebadili majina ya band tu. Hawa wazee wote wamejaa mawazo ya CCM ndani yao. Hata kama wanapinga ufisadi sasa ni kwasababu wamenyimwa nafasi ya ulaji. Mtu anayeamini Mbowe anapinga ufisadi inatakiwa akapimwe akili yake kama ni nzima.

Zitto usikate tamaa na endelea kupigana tu.
 
Kinyang'anyiro CHADEMA: Zitto Kabwe ajitoa

  • Asema anataka kurudisha mshikamano CHADEMA

na Kulwa Karedia

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amejitoa kwenye mbio za kinyang'anyiro cha uenyekiti wa taifa wa chama hicho, Tanzania Daima Jumapili imethibitisha.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka ndani ya CHADEMA zinaeleza kuwa, Zitto aliwasilisha barua yake ya kujitoa katika mchuano huo jana asubuhi.

Chanzo cha kuaminika kiliieleza Tanzania Daima Jumapili kwamba, kabla ya Zitto kuwasilisha barua yake hiyo alikuwa ameitwa kuhojiwa na Baraza la Wazee wa chama hicho linaloongozwa na mwenyekiti mstaafu, Edwin Mtei.

"Zitto na Freeman Mbowe, ambao ndio waliochukua fomu za kugombea waliitwa ndani ya kikao cha Baraza la Wazee kuhojiwa kuhusu dhamira zao za kugombea uenyekiti na kila mmoja akaeleza makusudi yake.

"Wakati akiwa katikati ya mahojiano hayo, Zitto aliwasilisha barua yake ya kuamua kujitoa, akisema anafanya hivyo ili kurejesha umoja na mshikamano ndani ya chama, ambao unaweza kupotea kutokana na kugombea nafasi hiyo na mwenyekiti wake," kilisema chanzo hicho cha habari.

Tanzania Daima Jumapili ilipowasiliana kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibrod Slaa, jana jioni kuhusu taarifa hizo, alithibitisha kuiona barua hiyo ya Zitto kujitoa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti.

"Ni kweli nimepokea barua ya Zitto ya kujitoa kwenye uchaguzi," alisema Dk. Slaa na kuongeza:

"Katika moja ya sababu zake kubwa aliyoisema ni kwamba amechukua uamuzi huo kwa nia moja tu ya kuendeleza mshikamano wa chama chake," alisema.

Baada ya kutoa maelezo yake hayo, Dk. Slaa hakuwa tayari kuingia kwa undani kueleza kile kilichotokea.

Taarifa hizo za Dk. Slaa zilisababisha gazeti hili limtafute Zitto mwenyewe ili kupata taarifa za kina kutoka kwake.

Alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, Zitto alikiri yeye na Mbowe kuitwa katika kikao cha Baraza la Wazee, ambako walitoa maelezo yao binafsi kuhusu kugombea.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo kijana ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini hakuwa tayari kueleza kuhusu kuwasilisha barua yake ya kujitoa katika mchuano huo.

"Nani kakwambia nimejitoa? Ninachoweza kukueleza kwa sasa ni kweli kwamba, leo (jana Jumamosi) tuliitwa kujieleza katika Baraza la Wazee na taarifa kamili kuhusu mambo yote zitajulikana kesho (leo Jumapili)," alisema Zitto.

Hata hivyo, wakati Zitto akikataa kutoa maelezo yoyote kuhusu hilo, rafiki yake wa karibu aliyezungumza na gazeti hili alithibitisha kuhusu uamuzi huo wa kujitoa.

Uamuzi wa Zitto kujitoa katika mchuano huo umekuja siku kadhaa baada ya hatua yake ya kugombea kiti hicho kuzusha mjadala mkali ndani na nje ya nchi.

Kuibuka kwa mjadala huo kwa kiwango kikubwa kumetokana na hatua ya mwanasiasa huyo kuamua kukabiliana na Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Uamuzi huo wa Zitto ulionekana kuwashtua viongozi mbalimbali wa juu na wazee wa chama hicho.

Mbali ya hao, uamuzi huo wa Zitto ulikwenda mbele zaidi na kugusa mijadala ndani ya vyama vingine vya siasa, kikiwamo Chama Cha Mapinduzi (CCM), CUF, NCCR- Mageuzi na TLP.

Makada kadhaa wa CCM waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti juzi na jana walisema, mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA ni jambo linalofuatiliwa kwa karibu.

Ukikiacha chama hicho tawala, uamuzi huo wa Zitto kugombea uenyekiti na kuchuana na Mbowe ulionekana kuungwa mkono na wakati mwingine kushangiliwa na viongozi wa vyama vingine vya upinzani.

Gazeti moja lilimkariri Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, akimsifu Zitto kwa uamuzi wake huo, akimwelezea kuwa kijana shupavu na ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya kuviunganisha vyama vya upinzani.

Hata hivyo kikubwa kilichokuwa kikivuta hisia za watu wengi ni madai ambayo Zitto mwenyewe aliyakanusha mara kadhaa kwamba uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wa chama hicho ulikuwa na msukumo kutoka nje ya CHADEMA.

Chanzo:
Tanzania Daima


My Take: Kama ni kweli Zitto aliwasilisha barua jana Jumamosi kwa nini asiseme tu kuwa ni kweli?

Pili kama CCM wanafuatilia kwa karibu mabadiliko ya uongozi ndani ya Chadema, jibu ni moja kuwa kusambaratika kwa CHADEMA itakuwa ni furaha kubwa sana kwao. Lakini ni nani atakayebeba 'dhambi' hii?

Hadi Mrema naye! ya kwake na Mtungirehi ameyaweza?
 
Mdau Mkulima,element ya Uislam unaionaje katika hii saga?

Mimi ni Athiest na hayo mambo yenu ya dini ni mbalimbali kabisa. Tatizo hapa ni ukabila kuliko udini.

Angalia kule Kilimanjaro yaani viongozi wote wa CHADEMA ni kabila moja, kulikoni? Kuna makabila mengine mengi na wengi Wakristo lakini kupita kule itakuwa ni taabu.

Pia katika Wachaga kuna Waislam wengi sana na hawabaguani kwa dini ila ukiwa kule unagundua kabisa dharau ya Wachaga dhidi ya makabila mengine.

Mzee Mtei amejidhalilisha kuingia kwenye kulinda maslahi ya mkwewe.
 
yaani mbowe anagombamnia peke yake,mtu kachukua form anaitwa kuhojiwa kwa nini umechukuwa form,lol hapa pananitisha ile mbaya,tunakataa ya ccm sasa yanakuja chadema. kweli ndio chama hiki kipo tayari kuchukua khatamu? naomba jawabu wakuu?
 
Zitto: Sijitoi ng'o kwenye kinyang'anyiro

Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 29th August 2009


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kabwe Zitto, amesema hana mpango wa kuondoa fomu yake ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, kwa kuwa ni haki yake na ana sifa za kuwa Mwenyekiti.

Pia Zitto amekanusha taarifa kuwa fomu zake zilirejeshwa na watu wanaoshinikiza awanie nafasi hiyo kwa lengo la kukibomoa chama hicho na kusema kama ni shinikizo basi ameshinikizwa na wana Chadema na si mtu wa pembeni.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Zitto alikiri kuchukua fomu na kufuata taratibu zinazotakiwa na kama kuna tofauti ni mbinu za kisiasa.

"Hii ni staili tu, nisingeweza kuchukua mdundiko, kwanza nilikuwa jimboni kisha nilikuwa na safari ya Ujerumani hata fomu zenyewe nilijazia Uwanjani
(wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere)," alisema.

Alisema alichukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa na uwezo wa kukipeleka mbali chama hicho na hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ambapo inatarajiwa kuwapo vijana wapya wapiga kura wapatao milioni 6.3 hivyo ni vyema chama kijipambanue kwa kuongozwa na kijana.

"Nikiwa kijana kama wanavyodai, kwa nini niweze kuongoza kamati hiyo ila nishindwe chama chenye mapato ya Sh bilioni 72 kwa mwezi?
Hata hivyo binafsi sikupenda kugombea uenyekiti, lakini nimeombwa sana na wanachama na kujikuta najaza fomu hizi," alisema.

Aliwataka waliozusha na kutunga uongo dhidi yake, watambue kuwa yeye si mtu wa visasi, lakini pia uchaguzi unapita na maisha baada ya hapo yataendelea, lakini pia akasema haamini kama chama hicho kimetawaliwa na ukabila kama inavyodaiwa.

Hata hivyo, alionyesha masikitiko yake kwa gazeti linalotoka kila siku lililoandika habari dhidi yake ikionesha wazi kuwa linatumiwa, na hivyo kuleta dhana kwamba ukabila ndani ya chama hicho upo, kwa kuwa gazeti hilo mmiliki na mhariri wake ni Wachaga.

Habari zaidi na Habari Leo http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3409

Sasa kweli haya magazeti yetu haya!

Sijui nisemeje lakini nahisi katika haya mawili kuna moja linasema kweli na jingine labda linaspin.

Nimeshtushwa na mambo mawili,

kwanza eti Zitto alijazia form za kuwania uenyekiti wa CHADEMA uwanja wa ndege! kwa haraka aliyokuwa nayo, of course, swali ni kwamba ni lini alipata nia ya kugombea? kwa nini asingejaza hizo fomu kabla, akiwa ofisini nk, kuliko kuingiza safari ya ujerumani ambayo nayo alikuwa akiijua kuwa ipo? hapa inaonyesha kuwa aidha hakuwa serious na hili au ameshinikizwa, na hili linajidhirisha pale anaposema kuwa mwenyewe hakutaka ila "aliombwa sana" na wanachama! Kama habari leo limemquote vizuri.

Kama ni kweli hakutaka kugombea uenyekiti ila kwa 'kuombwa' maana yake ni kuwa alishajiassess akaona kuwa kwa nafasi hii na wakati huu kuenda yeye bado bado, kwa hiyo inatupa pia wasi wasi , kama tulivo na wasi wasi na Mbowe ambaye pia naye 'ameshinikizwa na wazee' kugombea tena kwa mujibu wa duru za habari.

Je, kuna nguvu za kutoke nje ya Chadema zinazo operate ndani ya Chadema? je Chadema kinaweza kuaminiwa kweli katika hali kama hii?

 
Nashindwa kuilewa misimamo ya Zitto! Siku si nyingi alikuja hapa ukumbini akizungumzia kustaafu siasa ili aweze kutumikia profession aliyoisomea, mara anagombea uenyekiti wa Taifa Chadema, sasa amejitoa sijui atakuja na lipi?
 
Nashindwa kuilewa misimamo ya Zitto! Siku si nyingi alikuja hapa ukumbini akizungumzia kustaafu siasa ili aweze kutumikia profession aliyoisomea, mara anagombea uenyekiti wa Taifa Chadema, sasa amejitoa sijui atakuja na lipi?

Mkuu hata mimi ndo ninaposhindwa kumwelewa,, lakini hili linazidisha wasi wasi tu dhidi yake, nadhani kama mwanasiasa inabidi kidogo ujenge trust kwa wafuasi wako..kwa hili la trust naona Zitto anafeli hii test mkuu!
 
Mimi ni Athiest na hayo mambo yenu ya dini ni mbalimbali kabisa. Tatizo hapa ni ukabila kuliko udini.

Angalia kule Kilimanjaro yaani viongozi wote wa CHADEMA ni kabila moja, kulikoni? Kuna makabila mengine mengi na wengi Wakristo lakini kupita kule itakuwa ni taabu.

Pia katika Wachaga kuna Waislam wengi sana na hawabaguani kwa dini ila ukiwa kule unagundua kabisa dharau ya Wachaga dhidi ya makabila mengine.

Mzee Mtei amejidhalilisha kuingia kwenye kulinda maslahi ya mkwewe.
Nimekupata Mkuu.
 
Zitto ataweza?

Maswali Magumu

Ansbert Ngurumo

[source tanzania daima jumapili]

Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.

Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.

Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.

Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.

Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyang'anyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.

Maelezo ya Ngurumo yamekaa kama vile Zitto mwaka 2005 alikuwa na uwezo mkubwa sana ndani ya chama. Sasa kama kitu kama hicho anachotaka kukifanya Zitto kilifanyika na Mbowe mwaka 2005, hapa tatizo liko wapi? Walifanya nini kuibadili hiyo hali? Waliweka MIIKO kwenye katiba ili kutokuruhusu WEZI na VIBAKA kuingia ndani ya chama?

Naamini wanaosema kuwa kwa hali ilivyo sasa, basi Mbowe pia angelijitoa kwenye uchaguzi huo. Na hapo angelibaki akiomba mambo yasiwe mazuri sana ndani ya CHADEMA kwani uchaguzi ujao angelifanya Bounce back ya Zuma. Angelirudi kuwa Mwenyekiti kwa NGUVU kubwa zaidi. Sasa kwa MWENDO huo nasema:

"Zitto kaa pembeni. Subiri uchaguzi ujao na kama Mbowe ataboronga basi kutakuwa na haja ya KUUBADILI uongozi wa KICHAGA au kuanzisha Chama kipya ambacho hakitakuwa KINA MWENYEWE ila cha WANACHAMA. Kuanzia mwanzo lazima ijulikane hivyo.

CCM ni cha Nyerere na WANAE/wajukuu wake .......
CHADEMA cha Wachaga (Mtei na wenzake na sasa wamempa Mbowe/mkwe)......
CUF cha Maalim Seif na kaka Lipumba kawekwa PICHA .......
Vyama vingine wala sina la kusema.......

Chama cha kweli cha WATANZANIA kinahitajika bila ya kuruhusu TAJIRI yoyote kukidominate.
 
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.

Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.

Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...

Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.

Katika hili, mmechemsha!

Mkuu Invisible, inawezekana kuwa uko sahihi. Lakini kuna mambo ya mbali sana tunayotakiwa kuangalia kuhusu uamuzi wa wazee kumshinikiza au kumuomba Zitto aondoe jina lake. Naamini kuwa wanafahamu nini maana ya Demokrasia, nini maana ya uchanguzi na wanafahamu uwezo, upungufu na manufaa yanayotokana na mmoja kati ya wanachama hao wawili kuwa mwenyekiti wa Chama.

Zitto mwenyewe amesema anakiri kuwa Mbowe ametoa mchango mkubwa kwa Chadema, na sisi wenyewe tumeona mchango za Zitto kwenye jimbo lake na kwa taifa. No doubt kuwa wowte wanauwezo.

Lakini, ukiangalia jinsi jamii yetu ilivyo na siasa zetu zinavyokwenda, naona kwa sasa Zitto can serve us better asipokuwa mwenyekiti wa chama. Ana uwezo mkubwa wa kuwa mwenyekiti lakini tukiangalia alama za nyakati na hali ya siasa za sasa inaonekana kama yeye anatakiwa front line, na sio kwenye desk, he is more of a fighter, and can serve the nation better as a fighter than kuwa mwenyekiti wa chama. By the way CHADEMA inatakiwa ioneshe muendelezo wa kipindi kilichopita, kujenga chama na kujitahidi kuwafikia zaidi wananchi na kutetea zaidi maslahi ya wananchi. Sina hakika kama hilo linaweza kufanikishwa vizuri na Zitto akiwa mwenyekiti.

By the way, kama kuna wazee CHADEMA that is a very good sign, kama kuna wazee ambao Zitto ameweza kuwasikiliza ni jambo zuri sana. Na ikumbukwe kuwa Zitto alisema ameombwa na wanachama agombee uenyekiti, sioni kama kuna ubaya aksema ameondoa jina lake kutokana na ombo la hao hao wanachama.
 
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.

Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.

Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...

Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.

Katika hili, mmechemsha!

Binafsi ningependa wagombea waruhusiwe katika vyama vyote;

Mh Shibuda asiwekewe zengwe akitaka kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM mwakani,
Zitto naye aendelee kugombea Chadema kwani ni haki yake kama mwanachama, ingawa nina wasiwasi na msimamo wake toka alipojaribu kwa kushirikiana na Waziri Ngeleja kuizunguka Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kula njama za kuuza mitambo ya Richmond/Dowans kwa Serikali kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma. Ni ushupavu wa Mh Shelukindo na Spika Sitta wa kusimamia Sheria ndio uliokoa njama hizo zisifanikiwe. Zitto alishikia bango ununuzi huo na alipoulizwa kama anamfahamu mmiliki wa Richmond/Dowans alisema hana haja ya kumfahamu. Je pesa za ununuzi huo alioutaka angelipwa nani?

Kama mafisadi wana mkono wao katika hili la sasa la kugombea uongozi Chadema basi wana-Chadema wawe makini sana.

Mkuu Invisible, hilo la wote wawili kuondoa majina yao (nime-highlight sentensi yako) halifai kabisa kwa Chadema, ingawa itakuwa habari njema kwa wapinzani wao. Acha wote wagombee. Mtu aondoe jina kwa hiari yake.

Mkuu je Shibuda akichukua fomu CCM utapendekeza wote yeye na Kikwete ambaye anategemea kugombea tena kupitia CCM waondoe majina yao kwenye kugombea?

Mrema naye anarukia treni wakati hataki wagombea wengine kwenye Chama anachokiongoza, ambacho kwa sasa ni TLP. Yeye na Cheyo wa UDP ni kati ya mifano hasi ya viongozi wa vyama vya upinzani.
 
Inaonekana Zitto alikuwa anapata shinikizo kutoka kwa watu mbalimbali agombee.

Haionekani kama mwenyewe alikuwa amedhamiria kikweli kutaka kugombania hiyo nafasi kama sio tu kuridhisha watu waliokuwa wanamshinikiza. Sina uhakika kama Zitto alikua anajua kama hao watu wanaomshinikiza dhamira zao ni kuisaidia CHADEMA au kujisaidia wenyewe! Hata hivyo kama Zitto amesikiliza ushauri wa wazee na kujitoa kugombea uenyekiti sio cha ajabu mbona alisema hatagombania ubunge baadae akaja akabadilisha akasema atagombania tena ubunge. Hio ni uamuzi wake!

Tunajuaje kama kuna watu walimshauri agombanie au asigombanie? Labda ni wazee pia lakini naona final decision inakua yake mwenyewe TUIHESHIMU. Hakukatazwa wala kulazimishwa kuondoa jina lake as far as we know! CCM lovers are very hurt by this decision kwani waliona ndio wameshinda sasa watafute mkakati mwingine.

THIS ONE IS A GONER
 
Kuna vijana kadhaa ndani ya CHADEMA walikuwa wamekomalia kuhakikisha Zitto haendi mbele, imenisikitisha sana. Na tuna nakala ya kila kilichoongeleka katika kikao cha jioni ya leo, baada ya kusikiliza mara kadhaa nimejikuta nakosa imani KABISA! Lakini, muda bado unaruhusu.... Mruhusuni Zitto agombee nafasi ya uenyekiti, acha unyanyasaji kwa kisingizio cha ujana!

Yawezekana kugombea kwake kama angeshindwa kungesababisha 'Anguko lake' ambalo nadhani si 'Anguko la CHADEMA' kama ilivyokwishatabiriwa... Niwahakikishie kuwa kwa kumlazimisha aondoe jina ni kupelekea Anguko la CHADEMA.

Napata wasiwasi ndiyo sababu iliyomfanya Kubenea kuamua kuingia ulingoni kwa kupitia CCM, hajaona 'difference'.

Binafsi siamini kama CHADEMA wanaweza kufanya haya wanayofanya ambayo ni utaratibu wa CCM. Hiyo demokrasia inayoimbwa ni ipi?? Kama issue hapa ni ufadhili wa Mbowe? basi akubali wapambane na kijana zito atakaye shinda basi awe mwenyekiti!!

Hivi mawazo ya kijima yataisha lini ktk siasa za Tanzania? Hapa naanza kuona ni jinsi gani Kibanda aliandika ile makala ya kumkashfu Zitto, huenda alitumwa na Mbowe.
 
yaani mbowe anagombamnia peke yake,mtu kachukua form anaitwa kuhojiwa kwa nini umechukuwa form,lol hapa pananitisha ile mbaya,tunakataa ya ccm sasa yanakuja chadema. kweli ndio chama hiki kipo tayari kuchukua khatamu? naomba jawabu wakuu?

Kwa kweli ni aibu kwa upinzani wa Tanzania. Lakini ukiangalia political struggle kote duniani haya mambo yamewahi kutokea, kenya ni mfano mmoja wapo.

Kubwa linalo onekana ktk siasa za Tanzania ni kutumia pesa binafsi kuanzisha na kuendesha vyama. Hili ndo tatizo CHADEMA na vyama vingine vya siasa. Inatakiwa tufike mahali ambapo michango ya wanachama au kikundi cha watu ndo ianzishe chama, hapo hakutakuwa na suala la ukabila, udini wala nini.

Viongozi watachaguliwa kutokana na wanachama pasipo mtu kusema yeye ana haki zaidi ya mwingine kwani waliungana ili kuanzisha chama.
 
Ndugu wana JF na Watanzania kwa ujumla, hebu tujiulize ni vyama vingapi vya kisiasa hapa duniani wanaendesha uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti kwa mgombea zaidi ya mmoja??? Kama vipo ni vichache sana na tena tunajua asilimia kubwa ya vyama hivyo vinavyomeguga.

Si nia yangu ya kuvitaja hapa bali kila mmoja ajaribu kuangaza huku na kule katika kumbukumbu zake na afanye tathmini. Principally, ni kweli ingependeza sana kama pangekuwa na free competition. Lakini wanaogopa nini au kwa nini hawafanyi hivyo??

Hata Ulaya na Amerika ambako tunaamini ni wanzilishi wa demokrasia hii lakini bado katika hili vyama vingi vimeshindwa. Kwa hiyo sidhani kama ni busara kubwa kukilaumu sana CHADEMA, unless watu mnapenda kulaumu tu na hii itakuwa hasa kwa watu wasiopenda kuangalia mambo kwa mapana zaidi.
 
Hongera Zitto kuleta ushirikiano kwa kujitoa Kugombea...ila wadau tusishangae Ushirikiano utakaoletwa na Akina Sitta na Wenzake. ktk Kikao cha Bunge lijalo October..!!!

Ila Chadema tuhuma za kuwapa Wanachama wenzenu kuwa wanatumiwa ni Mbaya sana...hazitofautiani sana na CCM ambao wamewatuhumu akina Sitta Kutumiwa...!!!
 
Last edited:
CHADEMA: Chama Cha DEMOKRSASIA na MAENDELEO

Huu ndiyo msingi mama wa Chama kama wanataka waeleweke ni chama cha namna hiyo. Kabla hawajafanya maamuzi yote kwa kivuli cha UMOJA wa CHAMA wakumbuke CHADEMA inasimamia nini ukiondoa individuals. I hope CHADEMA wanataka kujenga TAASISI huru na si UFALME.

Then kama ni hivyo wajiulize: DEMOKRASIA YA KWELI NI NINI?
Na MAENDELEO YA KWELI NI NINI?

Then si vibaya kujifunza kutoka USA ilikuwaje The CLINTONS magiant wa Chama wakapambana na The OBAMAS na je kwa kufanya hivyo walikigawa chama?

Mbowe na Ndesamburo ndo wafadhiri wa CHADEMA sasa hiyo demokrasia inakujaje?
Na hata siku CHADEMA ikichukua nchi ndo mtawajua ndugu zetu wa kaskazini walivyo. Hawa walimshida mwl. nyerere pamoja na kuwabana lakini angalia pesa za maendeleo zilikuwa zinaishia mikoa hiyo hasa kilimanjaro. Sasa wakishika madaraka tutakoma sisi wa kibondo ambao hata chini ya CCM tunakiona cha moto.

Sisemi wachaga kuwa na chama ni vibiya lakini tatizo ni kwamba chama (CHADEMA) walikianzisha kwa fedha zao, utawaambiaje leo eti demokrasia wakati walikukaribisha tu wewe na hukuchangia chochote???-hili ni swali kwa zitto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom