Chama chenu ci kafu au?kile chama cha mapalala
Mkuu Invisible, inawezekana kuwa uko sahihi. Lakini kuna mambo ya mbali sana tunayotakiwa kuangalia kuhusu uamuzi wa wazee kumshinikiza au kumuomba Zitto aondoe jina lake. Naamini kuwa wanafahamu nini maana ya Demokrasia, nini maana ya uchanguzi na wanafahamu uwezo, upungufu na manufaa yanayotokana na mmoja kati ya wanachama hao wawili kuwa mwenyekiti wa Chama.
Zitto mwenyewe amesema anakiri kuwa Mbowe ametoa mchango mkubwa kwa Chadema, na sisi wenyewe tumeona mchango za Zitto kwenye jimbo lake na kwa taifa. No doubt kuwa wowte wanauwezo.
Lakini, ukiangalia jinsi jamii yetu ilivyo na siasa zetu zinavyokwenda, naona kwa sasa Zitto can serve us better asipokuwa mwenyekiti wa chama. Ana uwezo mkubwa wa kuwa mwenyekiti lakini tukiangalia alama za nyakati na hali ya siasa za sasa inaonekana kama yeye anatakiwa front line, na sio kwenye desk, he is more of a fighter, and can serve the nation better as a fighter than kuwa mwenyekiti wa chama. By the way CHADEMA inatakiwa ioneshe muendelezo wa kipindi kilichopita, kujenga chama na kujitahidi kuwafikia zaidi wananchi na kutetea zaidi maslahi ya wananchi. Sina hakika kama hilo linaweza kufanikishwa vizuri na Zitto akiwa mwenyekiti.
By the way, kama kuna wazee CHADEMA that is a very good sign, kama kuna wazee ambao Zitto ameweza kuwasikiliza ni jambo zuri sana. Na ikumbukwe kuwa Zitto alisema ameombwa na wanachama agombee uenyekiti, sioni kama kuna ubaya aksema ameondoa jina lake kutokana na ombo la hao hao wanachama.
Kwani lidhiwani kikwete na kiwete inakuwaje au umemuona Lucy peke yake. Makamba na mwanae pale ikulu vipi?
Lunyungu said:Ndugu zanguni naona sasa tumeongea hata tunafika mahali nadhani inakuwa shida .Tatizo la Chadema sasa katika uongozi si la kwanza katika medani za Siasa Tanzania nahata Afrika .Lugha za kusema chama kina wenyewe nao ni wachaga ni kupotosha .Wazee walio kaa na Zitto na Mbowe ni hawa
Bob Makani
Mtei E
Ngaiza
Slaa
Pro.Baregu
na nadhani kuna 2 nimewasahau.
Hebu tuanze kuangalia wachaga ni wangapi hapa na familia moja ni ipi hapo .
Kuna jambo moja kwamba watu wanusuru Chama sasa tuombee mema maana hata Mbowe na Zitto wanajua nini tunataka , Mtei bahati njema anakuja humu anajua na si kwamba hawapati mijadala. Jana hawaja lala wote wanafuatilia tunasema nini ni wazi wamesha ujua msimamo wetu .Sote kabisa tuna nia njema kwamab Chadema iende mbele nadhani tuweke nguvu katika hilo na siamini kwamba mtu akusema turudi CCM ndiyo jibu sahihi .Lazima mambo mengine tuyasimamie kwa nguvu zetu bila kila kitu kurudi nyuma na kurusha lawama .
Lunyungu,
..ukikwepa shutuma za UCHAGA unaangukia kwenye shutuma za UDINI.
..wangemuachia tu Zitto na shutuma kwamba Chadema ni mali ya Wachaga na Wakristo zingekwisha.
NB:
..lakini pia namshangaa sana Zitto kuingia kwenye kinyanganyiro cha Uenyekiti kwa madai ya kutaka kukinusuru chama.
..halafu anageuka na kujitoa, akidai anataka kukinusuru chama.
..kwanza Zitto alidai anataka kupumzika ubunge na kwenda kusoma mpaka afikie PhD. siyo zaidi ya miezi mitatu iliyopita when that happened. sasa amebadilika anataka kutetea kiti chake cha ubunge, then amejaribu kugombea uenyekiti wa chama, na sasa amejitoa.
..kwa wanaomshauri wamwambie atulie anawachanganya wananchi.
Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.
Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...
Article ya Kibanda ilitosha kuwa shinikizo kwa Zitto...Kibanda si Mtu mdogo...
I'm speechless kwa haya yanayotokea Chadema...Bado tuna safari ndefu mno kufikia Demokrasia ya kweli....Kwa mwendo huu bado tutakuwa na taabu sana ya kuing'oa CCM!!
Zitto na vijana wengine wa Chadema... Karibuni CCM
Wakati CHADEMA mnapandishiana, ndipo CCM inapata nafasi ya kutia propasganda, na hata kuyeyushilia mbali skendo za ufisadi ambazo zimekuwa zinaibuliwa na CHADEMA hao hao: Pakacha kuvuja ndiyo nafuu kwa mchukuzi.
yote yana mwisho
Upinzani wa KWELI utatokea CCM.Period.
Hizi siasa za bongo miyeyusho tu
Tuliwaambia zamani sana ila hamkusikia, sasa yanatokea ndo mnashtuka.
Ansbrt Ngurumo said:
Nataka kumtetea Zitto kidogo. Naamini kwamba hatumiwi na CCM bila kujua. Kwangu mimi, Zitto ameshavuka viwango vya kutumiwa bila kujua. Zitto ni mjanja vya kutosha, kiasi kwamba akiamua kutumika, atafanya hivyo kwa hiari yake.
Kama wanakerwa na vikao vya siri anavyofanya na vigogo kadhaa wa CCM, waseme; na watutajie majina. Kama ni Joseph Sinde Warioba au Dk. Ahmed Salim au Rostam Azizi au Edward Lowassa au Rais Jakaya Kikwete au Lawrence Masha au William Ngeleja; waseme wazi.
Maana kinachozungumzwa sasa ni kwamba mojawapo ya ajenda za Zitto kuutaka uenyekiti ni ahadi aliyopewa na baadhi ya vigogo wa CCM kwamba wanatamani kujiengua na kujiunga na CHADEMA iwapo tu, ataweza kumwangusha Freeman Mbowe katika nafasi ya uenyekiti.
Uongo wanaotumia ni kwamba wakishajimega kutoka CCM wataiwezesha CHADEMA kupata wabunge wengi mwaka 2010, na hata kuipa uwezekano wa kuwa na waziri mkuu kutoka chama cha upinzani.
Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.
Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.
Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.
Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.
Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyanganyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.
Zitto amekuwa mmoja wa mashujaa katika vita dhidi ya ufisadi, lakini akiwa mkweli atatuambia bila kificho kuwa watu wale wale waliokuja kufahamika baadaye kuwa mafisadi, ndio waliokuwa wanaomba CHADEMA iwape nafasi walipokuwa hawajaipata CCM.
Ndiyo maana wengi wetu tunatarajia kwamba Zitto angepaswa kuwa mwangalifu sana anapoletewa masharti ya namna hii na vigogo wa CCM wanaomuahidi kujiunga CHADEMA kwa kishindo iwapo atamuondoa Mbowe.
Ndiyo maana Zitto alipojisahau akaanza kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans, akidhani umaarufu wake ungeweza kubadili mjadala wa kitaifa na upepo wa kisiasa, wapambanaji wenzake walimsikitikia sana, na tuhuma za waziwazi zikaanza kurushwa dhidi yake kwamba kuna waliomharibu.
Na katika siku za hivi karibuni, Zitto amesikika akizungumza katika Radio Sauti ya Ujerumani akidai kwamba tofauti ya msingi kati yake na Mbowe katika kinyanganyiro cha uenyekiti ni kwamba Mbowe ni bepari, Zitto ni mjamaa!
WEWE Ansbert Ngurumo UMELIPIWA ADA YA SHULE na Mbowe. Chochote utakachosema humu kwa mshindani wa Mbowe ni CONFLICT OF INTEREST.
Bado natafakari suala la DOWANS, Kujitoa na kurudi tena kuwania ubunge na hili la mwenyekiti.
Kimsingi sijawahi kukutana wala kuongea na Zitto, namwona tu magazetini, JF but sisi wafuasi wake tunapata shida kumsafisha kuhusu suala la Dowans. Siasa mtaji wake ni watu, Kumbuka kupigiwa makofi sio umaarufu.
Something is seriously wrong somewhere.
Nashindwa kuilewa misimamo ya Zitto! Siku si nyingi alikuja hapa ukumbini akizungumzia kustaafu siasa ili aweze kutumikia profession aliyoisomea, mara anagombea uenyekiti wa Taifa Chadema, sasa amejitoa sijui atakuja na lipi?
By the way CHADEMA inatakiwa ioneshe muendelezo wa kipindi kilichopita, kujenga chama na kujitahidi kuwafikia zaidi wananchi na kutetea zaidi maslahi ya wananchi. Sina hakika kama hilo linaweza kufanikishwa vizuri na Zitto akiwa mwenyekiti.
Kama mafisadi wana mkono wao katika hili la sasa la kugombea uongozi Chadema basi wana-Chadema wawe makini sana.
Wakuu, nimeamua kuchukua summary kwa ajili ya reference ya ambao wameanzia mjadala katikati...It can be plainly seen that Zitto's head is getting to big and he is unknowingly being used, by the few elites, to demolish Chadema.
Ndugu zanguni naona sasa tumeongea hata tunafika mahali nadhani inakuwa shida .Tatizo la Chadema sasa katika uongozi si la kwanza katika medani za Siasa Tanzania nahata Afrika .Lugha za kusema chama kina wenyewe nao ni wachaga ni kupotosha .Wazee walio kaa na Zitto na Mbowe ni hawa
Bob Makani
Mtei E
Ngaiza
Slaa
Pro.Baregu
na nadhani kuna 2 nimewasahau.
Hebu tuanze kuangalia wachaga ni wangapi hapa na familia moja ni ipi hapo .
Lakini na mimi japo nilimwamini zitto ktk hoja zake naanza kuingiwa na wasiwasi hasa nikijaribu kukumbuka alivyo handle issue ya dowans.
Zitto kajitoa rasmi -TBC news
Mnajua ndo maana namba wani (CCM) wataendelea kutamba miaka nenda rudi, Wa wapi NCCR, wa wapi CUF? Yaani, kila chama cha upinzani kinachoanza kujipatia jina wanaanza kurogana wenyewe kwa wenyewe ndani kwa ndani. Na wakati huo huo CCM wakiwa pembeni wanagongeana tano kwani kazi ambayo wangetakiwa waifanye wao inafanywa na watu wa hivyo vyama bila hata wakati mwingine CCM kutia mkono wao.
Sababu kama hizi ndo zinanesha jinsi gani bado CCM watandelea kuwa kidedea kwa miaka mingi.
Pia sitashangaa Zitto out of frustration akihamia CCM!, watch this space!!
Mimi nimesikitishwa na nikiwa kama mwamanchama wa CHADEMA nitarudisha kadi yangu rasmi, nimechoka kuona hivi vitimbi. Sasa kama uenyekiti wa chama tu inakua ni kwa kukwaruzana kihivi, je tukiwapa nchi si ndio watagoma kung'atuka madaraka na kuanza kubadilisha katiba ili watawale milele?
Kwani mbowe ameshushwa kutoka mbinguni kuja kuwa mwenyekiti wa CHADEMA? Je huo umri unaozungumziwa hapo, je katiba ya CHADEMA hapo wazi kusema umri ni miaka mingapi?
By the way, nini maana ya neno uchaguzi kama atagombea mtu mmoja, huo uchaguzi wa kuchagua utatokea wapi sasa? Je tunaweza kuita huo ni uchaguzi au ni kumsimika Mbowe "to annoit"? Na je kama watu hawataki kumchagua Mbowe watamchagua nani sasa? Hapa ndipo utaona dhahiri sasa ugumu wa kufikiria, ufinyu wa mawazo na upeo mdogo tulionao sisi watu wenye ngozi nyeusi...!
Kwa manufaa ya CHADEMA na kwa manufaa ya demokrasia ningeshauri hao CHADEMA wondokane na hio aibu kubwa kabisa ya kumnyima mtu kugombea madaraka. Infact, kama nia ni kugombea Uraisi ambao mbowe ndio anautolea macho sio lazima mwenyekiti wa chama tu ndio awe na uwezo wa kuteuliwa na chama kugombea uraisi, chama kinaweza kikamchagua mtu yoyote yule kusimama na kugombea uraisi endapo kitaamua kuweka mgombea, lakini kwa sasa naona itakua ni upotevu wa rasilimali endapo vyama vya upinzani vitasimamisha mgombea wa uraisi kwani bado hata Ubunge tu umewashinda, sembuse uraisi?
Lunyungu said:Unajua mie nachoka sana kila mara watanzania mnapo kuja hoja nyepesi .Huko CCM kuna ujinga kibao ikiwa ni pamoja udini kumea hadi nje lakini no talking about it .CCM ina miaka mingapi ukilinganisha na Chadema ? Jamani we all know kwamba wakati vyama vina anzishwa watu wengi kama ilivyo walikuwa ni watu w akudharau kwaba wapinzani ni wapuuzi hawawezi kufika popote .Leo wamefika mahala pamoja na shida zao na uchanga nk bad utasikia Michaga mara wadini .Hivi kama watu hawaendi kwenye Chama na kugombea nafasi mnataka kesho kitokee nini ?
Nadhani this is to low hakika .Uongozi wa Chadema juu kuna Mbowe hadi sasa haya tuje chini huku tuona kuna wachaga wangapi akina Zitto ni wakristo ama wachaga akina Slaa ? Hebu tuangalie shida iliyoko mezani muda huu na si zaidi ya kuleta habari za akina Tambwe .CCM ina ukabila udini na hata ukanda kama wabisha angalia viongozi wote wakubwa wa CCM wakwepo akina Tambwe wanatokea wapi linganisha na Chadema.
Chadema they made a mistake kwenye viti maalumu nadhani hawatakaa warudie lakini pia lazima watu wajitolee kushiriki siasa wapate hizo nafasi na si kulalama tu.
Kifupi sioni sababu kabisa ya nafasi nyeti ya chama kama Mwenyekiti Igombewe na wanachama kwa kutumia Demokrasia, bila kuzingatia ethics na hatua za makuzi ya fikra zinazokiongoza chama.. Yaani kwa mtazamo wangu huwezi kuwa Sheikh au Padre kwa kutumia Demokrasia isiyokuwa na kipimo cha elimu, umri na wokovu wa mhusika ktk imani hiyo. Na wala sii haki kutumia mtazamo wetu finyu kukosoa Uongozi wa Kanisa au msikiti kwa madai ya Demokrasia ikiwa utaratibu wa dini hiyo unahitaji elimu, umri au kupitia ngazi fulani kabla hujafikia kuchukua kiti cha Upadre au Kuongoza Msikiti..
Hata sikuelewi mkuu wangu, kama wewe huamini Sheikh au Padre wako ana Practice what he Preach, huo wokovu unautegemea vipi huko mbinguni au sijui wapi!..Mkuu heshima mbele, lakini nikukumbushe tu kuwa huwezi kuokoka hapa duniani.