Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Siku zote nilikuwa siamini chadema kama ni chama kweli cha siasa,nakiona ni chama mizengwe tu kama ilivyo ccm na tlp,and they prove me right.....
 
Mimi nimesikitishwa na nikiwa kama mwamanchama wa CHADEMA nitarudisha kadi yangu rasmi, nimechoka kuona hivi vitimbi. Sasa kama uenyekiti wa chama tu inakua ni kwa kukwaruzana kihivi, je tukiwapa nchi si ndio watagoma kung'atuka madaraka na kuanza kubadilisha katiba ili watawale milele?

Kwani mbowe ameshushwa kutoka mbinguni kuja kuwa mwenyekiti wa CHADEMA? Je huo umri unaozungumziwa hapo, je katiba ya CHADEMA hapo wazi kusema umri ni miaka mingapi?

By the way, nini maana ya neno uchaguzi kama atagombea mtu mmoja, huo uchaguzi wa kuchagua utatokea wapi sasa? Je tunaweza kuita huo ni uchaguzi au ni kumsimika Mbowe "to annoit"? Na je kama watu hawataki kumchagua Mbowe watamchagua nani sasa? Hapa ndipo utaona dhahiri sasa ugumu wa kufikiria, ufinyu wa mawazo na upeo mdogo tulionao sisi watu wenye ngozi nyeusi...!

Kwa manufaa ya CHADEMA na kwa manufaa ya demokrasia ningeshauri hao CHADEMA wondokane na hio aibu kubwa kabisa ya kumnyima mtu kugombea madaraka. Infact, kama nia ni kugombea Uraisi ambao mbowe ndio anautolea macho sio lazima mwenyekiti wa chama tu ndio awe na uwezo wa kuteuliwa na chama kugombea uraisi, chama kinaweza kikamchagua mtu yoyote yule kusimama na kugombea uraisi endapo kitaamua kuweka mgombea, lakini kwa sasa naona itakua ni upotevu wa rasilimali endapo vyama vya upinzani vitasimamisha mgombea wa uraisi kwani bado hata Ubunge tu umewashinda, sembuse uraisi?
 
Kuna vijana kadhaa ndani ya CHADEMA walikuwa wamekomalia kuhakikisha Zitto haendi mbele, imenisikitisha sana. Na tuna nakala ya kila kilichoongeleka katika kikao cha jioni ya leo, baada ya kusikiliza mara kadhaa nimejikuta nakosa imani KABISA! Lakini, muda bado unaruhusu.... Mruhusuni Zitto agombee nafasi ya uenyekiti, acha unyanyasaji kwa kisingizio cha ujana!

Yawezekana kugombea kwake kama angeshindwa kungesababisha 'Anguko lake' ambalo nadhani si 'Anguko la CHADEMA' kama ilivyokwishatabiriwa... Niwahakikishie kuwa kwa kumlazimisha aondoe jina ni kupelekea Anguko la CHADEMA.

Napata wasiwasi ndiyo sababu iliyomfanya Kubenea kuamua kuingia ulingoni kwa kupitia CCM, hajaona 'difference'.
Mkuu tunaomba ile mada ya Kibanda na Zitto irudishe ili tuwe na rekodi sahihi.vinginevyo utakuwa unabana demokrasia kama Chadema.
 
taarifa nilizonazo mimi ni kwamba, zitto aliwasilisha barua ya kujitoa hata kabla mahojiano hayajamalizika. Alichofanya baada ya kufanya hivyo alipendekeza na mbowe naye ajitoe ili kuleta mshikamano ndani ya chama chao. Hata hivyo wazo hili halijakubalika.
kibanda umeshinda kweli ngoma ya mtoto/kijana haikeshi zitto kawa kama arsenal ya wenger.
 
You are right invisible,

Idea ya zito yakuwa naye Mbowe ajitoeis best Idea ever!

Nimelowana na kunywea
 
Mkuu umepata PM yangu?
Mkuu nimeipata, nawasiliana na 'mmoja wetu' utaongea nae dakika si nyingi.

Tunashughulikia JF mpya kwa ajili ya Ramadhan ambayo inaweza kuwa tayari baada ya dakika kama 5 hivyo naomba muda kidogo mkuu
 
Chacha Wangwe alifariki dunia lakini maneno yake yanaendelea kuishi
 
...nimesikitishwa na nikiwa kama mwamanchama wa CHADEMA nitarudisha kadi yangu rasmi, nimechoka kuona hivi vitimbi.

Ukisharudisha hiyo kadi ndio uje utuambie jamani eeh, nimerudisha kadi ya chama. Haya ya kusema nitarudisha, nitarudisha, ni kama hasira za mkizi tu. Rudisha, njoo tuongee ....LOL!

Napata wasiwasi ndiyo sababu iliyomfanya Kubenea kuamua kuingia ulingoni kwa kupitia CCM, hajaona 'difference'.

Hii kitu una uhakika nayo hii Mkuu Invisible?

Jambo linalobeba jina la Invisible humu ndani linabeba credibility nzima ya forum. Una hakika na hiyo habari ya Kubenea kwenda CCM Mkuu?
 
Jambo linalobeba jina la Invisible humu ndani linabeba credibility nzima ya forum. Una hakika na hiyo habari ya Kubenea kwenda CCM Mkuu?
Ni dhamira ya Kubenea kufanya vile, ndo naangalia nakuta hata post hapa JF, nikagundua kumbe si siri tena...! Dhamira hii haijafikisha hata siku 4 nadhani lakini ishasambaa, possibly Kubenea anaweza ku-withdraw. Nitaongea naye usiku huu na kuandika alichoongea nami kama yeye.
 
Nilishasema hapa toka zamani hakuna upinzani BONGO, ni njaa tu mkabisha.

Haya ES, masanja na wengineo wenzangu wakumbusheni hawa.

Chadema ni chama cha wazee ni chama binafsi cha MTEI na wenzake.
 
Invisible huko ulipo hujalala tu au ndio asubuhi sana huko Australia au marekani sijui?

Sisi hapa Mbagala tupo macho!
 
chacha wangwe alifariki dunia lakini maneno yake yanaendelea kuishi

chacha wangwe alikuwa more inteligent than the perception most had about him,now inaonekana wazi kuwa kifo cha chacha hakikuwa ajali kwa asilimia mia,wapo waliofaidika na kifo chake,the question is what if zitto akikataa kujitoa kugombea?i dont want to speculate.............
 
Chadema ni chama cha wazee ni chama binafsi cha MTEI na wenzake.
Namheshimu mzee Mtei sana, ni mwanachama wa JF na amechangia mara kadhaa lakini hajataka kuwa Premium Member, ni mtu ambaye naamini anaweza kuja hapa na kutupa mwongozo, hata Dr. Slaa huenda akatupa zaidi ya kile tunachokiona na kukisikia... Ni kesho tu, nitawasiliana na mzee Mtei kujua ana kauli gani katika hili.

BTW, ndo kunaanza kucha huku nilipo, ni saa 12 na dakika kama 40 alfajiri
 
Zito amejitoa unconditionally kwenye kinyang'anyiro baada ya kukutana na wazee wa chama.

mbowe kamtumia kibanda kaona Zitto anakuja tu.akaamua kutumiwa wazazi wake wenye chama.Kibanda alisema kabla ya kujiunga na vyama tuwe tunafikiri mara mbili mbili kauli yake imethibiti.
KIBANDA uko OVER THE MOON.
 
Huu ni mtihani mkubwa sana kwa CHADEMA, itajitenga ama kujibomoa kwa kutofuata misingi midogo ya demokrasia, uhuru wa kumua na uhuru wa kujieleza, kugombea na kuchaguliwa. Hazina kubwa ya CHADEMA ni vijana wasomi wenye nia ya kuleta mabadiliko, sasa hili la kung'ang'ania Mbowe awe mwenyekiti milele linanipa shida. Wazee wa CHADEMA ushauri wenu umesikika wacheni Zitto agombee silazima ashinde ...sasa manapohisi anatumika kwa kunufaisha CCM...hili halina maana ...mbona Mbowe naye anahusishwa na ufisadi?

Nafikiri mara mbili uanachama wangu CHADEMA!
 
Halafu kuna MORONS humu wanasema CCM ina wenyewe nani kasema Chadema haina wenyewe????
 
namheshimu mzee mtei sana, ni mwanachama wa jf na amechangia mara kadhaa lakini hajataka kuwa premium member, ni mtu ambaye naamini anaweza kuja hapa na kutupa mwongozo, hata dr. Slaa huenda akatupa zaidi ya kile tunachokiona na kukisikia... Ni kesho tu, nitawasiliana na mzee mtei kujua ana kauli gani katika hili.

Btw, ndo kunaanza kucha huku nilipo, ni saa 12 na dakika kama 40 alfajiri

to be honest mimi nilikuwa nawaheshimu mno chadema enzi za mtei,walipompa mbowe uenyekiti nilishangaaa sana,na sasa haya ya sasa ndo nazidi kuwaona wababaishaji,huyo mtei kwa mizengwe ndo mwenyewe ,aliwahi kumzuia bob makani asigombee urais kwa chadema,baada ya yeye kushindwa,
ukiaangalia aina ya watu wanaoisapoti chadema jinsi walivyo na elimu na uelewa na ukimuangali mbowe na background yake
it is so funny to believe what they are trying to achieve,but ohhh common sense is not common sio?????
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom